Salim Rashid Mohammed: Tunachojua kufikia sasa kuhusu mtuhumiwa wa ugaidi wa Kenya aliyekamatwa DRC
31 Januari 2022
CHANZO CHA PICHA,NATION MEDIA GROUP
Kenya itawasilisha ombi kwa serikali ya DRC kumrudisha mtu mmoja aliyekamatwa katika taifa hilo kuhusiana na tuhuma za ugaidi , vyanzo vya usalama vimesema.
Salim Rashid Mohammed alias Chotara au Turki Salim alikamatwa na jeshi la DR Congo kwa tuhuma kwamba ni mmoja wa waasi wa kundi la ADF ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi kaskazini mwa DRC na karibu na mpaka wa Uganda.
Mohamed ni mkaazi wa Mombasa na mshukiwa wa ugaidi ambaye Kenya ilikuwa imetoa $100,000 kwa yeyote yule ambaye angetoa habari kumuhusu.
Lakini ni nini haswa tunachokijua kufikia sasa kuhusu Salim Rashid?
Salim alikamatwa Ijumaa iliopita katika mji wa Beni uliopo mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
Kukamatwa kwake kunatokana na tuhuma za kuwa mwanachama wa kundi la ADF , kundi la wapiganaji wa Kiislamu linalofanya operesheni zake katika mpaka wa Uganda na DRC.
Katika kanda ya video ambayo imekuwa ikisambaa katika mitandao kijana huyo kutoka eneo la Mombasa nchini Kenya anadai kwamba alihusika katika mauaji ya mwanajeshi mmoja wa FARDC aliyetekwa nyara na wapiganaji hao wa kiislamu wa ADF.
Chombo cha redio nchini DR Congo RTGB kinadai kwamba kijana huyo alikamatwa baada ya kuondoka katika kambi ya ADF iliopo mashariki mwa DRC, katika mkoa wa Kivu.
Chombo hicho kimeongezea kwamba Mohamed, 28, alikuwa akisimamia propaganda za kundi hilo , ambazo zilishirikisha kusambaza kanda za video za mashambulizi yanayotekelezwa katika mikoa ya Kivu na Ituri..
Alikataa kujiunga na chuo kikuu kusomea uhandisi Kenya
Vyombo vya habari nchini Kenya vinasema kwamba operesheni za kigaidi za Mohammed zilianza 2015 , kabla ya kuondoka nyumbani kwao katika mji wa pwani wa Mombasa 2016 ili kusomea somo la uhandisi wa tarakilishi nchini Uturuki.
Alikuwa amekataa kujiunga na chuo kimoja kikuu nchini Kenya ili kusomea Uhandisi na akawacha kusoma baada ya mwaka mmoja.
CHANZO CHA PICHA,DCI/KENYA TWITTER
Maelezo ya picha,
Mamlaka nchini Kenya ilimshtaki Muhammed kwa kuwa mpiganaji wa Islamic State.
Baadaye aliishi Uturuki kwa muda mfupi , na akarudishwa nyumbani baada ya kupatikana katika mpaka wa Syria, kulingana na chombo cha Habari cha Nation.co.ke
Mamlaka nchini Kenya ilimshtaki Muhammed kwa kuwa mpiganaji wa Islamic State lakini akawachiliwa kwa ukosefu wa ushahidi.
Alikamatwa katika uwanja wa ndege Mombasa
Kijana huyo hatahivyo haikuchukua muda kwani alikamatwa tena katika uwanja wa ndege wa Mombasa 2019 na kushtakiwa kuwa mwanachama wa kundi la wapiganaji wa al-shabab nchini Somalia mbali na kumiliki vilipuzi.
Chombo cha Habari cha Citizen kiliripoti tarehe 30 mwezi Januari kwamba Muhammed alikuwa anaelekea nchini Sudan wakati alipokamatwa katika uwanja huo wa ndege.
Aliachiliwa kwa dhamana lakini akatoweka tena tarehe 5 mwezi Disemba 2020.
Tarehe 9 Novemba 2021, mamlaka nchini Kenya ilitangaza $90,400 kwa mtu yeyote ambaye alikuwa na habari za Muhammed kulingana na chombo cha habari cha the Standard nchini Kenya.
Polisi wa Kenya wanasemaje?
Maafisa wa polisi wanasema kwamba alituhumiwa kujiunga na wapiganaji wa IS nchini Msumbiji kufuatia kutoweka kwake 2020.
Wapiganaji wa IS baadaye walilichukua kundi la ADF 2019 chini ya "Central Africa Province" (ISCAP) kundi ambalo limedai kutekeleza mashambulizi nchini Msumbiji katika mkoa wa kaskazini wa cabo Delgado na kusini mwa Tanzania.
Kundi la ADF limehusishwa na mashambulizi hatari katika mji mkuu wa Kampala , mashambulizi mengi ya Kampala yamedaiwa kutekelezwa na IS.
Kenya itawasilisha ombi kwa serikali ya DRC kumrudisha mtu mmoja aliyekamatwa katika taifa hilo kuhusiana na tuhuma za ugaidi , vyanzo vya usalama vimesema.
www.bbc.com
MY TAKE
Huyu jamaa asirudishwe Kunyaland atatoroka tena! BTW nawashangaa askari wa DRC kwann wasimmalize kabisa?