BBC: Korea Kaskazini kupata tani 700,000 za mchele kwa kupeleka silaha na wanajeshi Urusi

BBC: Korea Kaskazini kupata tani 700,000 za mchele kwa kupeleka silaha na wanajeshi Urusi

Urusi hana jeshi ila Ukraine analo na hizo habari umezipata kutoka wapi unategemea kabisa kwamba balozi wa Korea kusini ainenee mema Ukraine kweli kama wanajeshi hata wa NATO wapo pia pale Ukraine kwa mgongo wa mercenaries
Hakuna mwanajesh wa NATO yupo ukraine lakini nakubali silaha zinaingia kama njugu Ukraine kwa ajili ya kutokomezwa vamizi russia., swali liko pale pale tu, kama russia ana jeshi la kutosha kwanini ilibidi wabadilishane na Noth Korea? Noth Korea wapewe mchele russia apewe wanajeshi?
 
Hakuna habari njema utaiona BBC, CNN au Washington Post kuhusu Urusi pamoja na Korea Kaskazini. Kama tu Trump anakwambia hawa jamaa ni fake news je mimi huku! Propaganda programs zipo kazini.
 
Naona umeamua sasa kuonesha sura yako halisi hemu leta sehemu Russia alisema kwamba op itakua ni ya siku tatu pia kama kuchukua mercenaries ndio kushindwa vita hata Iraq kule walikuwepo mercenaries pia israhell nae ana mercenaries kushinda vita tunaangalia mwenendo wa field na huko field anajulikana nani anateseka
Anayeteseka na vita ni Russia 100%, Zelensky anasema wanapigana na wanajeshi 50,000 katika maeneo ya Kurks wanajeshi 10,000 ni kutoka North Korea.,

Unavamia wewe halafu unarudishwa nyuma unavamiwa wewe kwenye eneo lako, nani anateseka?
 
Hakuna mwanajesh wa NATO yupo ukraine lakini nakubali silaha zinaingia kama njugu Ukraine kwa ajili ya kutokomezwa vamizi russia., swali liko pale pale tu, kama russia ana jeshi la kutosha kwanini ilibidi wabadilishane na Noth Korea? Noth Korea wapewe mchele russia apewe wanajeshi?
Wewe unabisha wakati viongozi wa NATO wenyewe walikiri kuwepo huko ila endelea kubisha kama marekani ana jeshi la kutosha kwa nini hakuenda kuivamia Iraq peke ake
 
Anayeteseka na vita ni Russia 100%, Zelensky anasema wanapigana na wanajeshi 50,000 katika maeneo ya Kurks wanajeshi 10,000 ni kutoka North Korea.,

Unavamia wewe halafu unarudishwa nyuma unavamiwa wewe kwenye eneo lako, nani anateseka?
Imerudishwa nyuma wapi kaiangalie mauriopol kaiangalie soledar bila kusahau bakhmut hakuna sehemu inaendeshwa chini ya Ukraine huko kursk
 
Imerudishwa nyuma wapi kaiangalie mauriopol kaiangalie soledar bila kusahau bakhmut hakuna sehemu inaendeshwa chini ya Ukraine huko kursk
sasa kaa mauriopol na bakhmut ipo chini ya russia kwanini Putin analalamika kwamba yeye anataka vita iishe lakini Ukrean imuachie hayo majimbo 4., kwanini na yapo chini yake??

ww huna ujualo ukisikia russia imechukua mauriopol ni partial yaani baadhi ya vijiji na maeneo lakini maeneo mengine mengi yapo chini ya ukraine vita inaendelea mkuu, hii movie ni ndefu sana mkuu usikurupuke sasa mwaka 3 na russia aliahidi operation yake itaisha kwa saa 72 tu.
 
Wewe unabisha wakati viongozi wa NATO wenyewe walikiri kuwepo huko ila endelea kubisha kama marekani ana jeshi la kutosha kwa nini hakuenda kuivamia Iraq peke ake
Wewe na putin nani anajua zaidi? Putin alisema siku NATO wakiingiza jeshi lao ukraine vita itabadilika na kuwa vita ya nuclear.

Russia anapambana na vidume vya Ukraine peke yake,
Mkuu mziki wa NATO ukiingia kazini pale full nchi 32 unafkiri Russia si litabaki vumbi tu na jangwa
 
Propaganda za west at its best...taifa lenye technology ya nuclear na rocket lishindwe kujilimia chakula?

Raia wote wa North korea wamepitia mafunzio ya jeshi. Ni skilled labor, hawawezi kushindwa kujilisha.
 
Hizo ni propaganda!

Jeshi bila uzoefu wa vita halisi bado linakuwa si jeshi kamili.

Kutumia mazoezi na mbinu walizofundishwa kwenye eneo halisi la vita ndipo jeshi linaimarika.

Korea ya Kaskazini mwisho wa kupigana vita halisi na vya kisasa ni kwenye vita vya wakorea wenyewe.

Korea ya kaskazini imeomba wapeleke wanajeshi wake kwenye vita ya Ukraine ili wapate uzoefu wa vita hususani ya kisasa inapigwanaje na kuangalia ubora wa zana zap upoje kwenye vita kamili.

Si Korea bali hata China ilipeleka vijana wake hususani kwenye urban warfare.

Hii hali inamuogopesha Korea ya Kusini ndiyo maana anatapa tapa!
Good analysis,
Wazandiki wanajaribu kupotosha Kila wanapopata nafasi.
Lkn ulichoandika ndio uhalisia wenyewe.
Hata hili suala wanaloita njaa ya KOKA kimsingi ni njaa iliyotokana na vikwazo onevu kutoka nchi mabebebru.
Laiti kama KOKA isingekua na vikwazo pengine Leo ingekua kama Malaysia.
Angalia pia nchi za Cuba na Iran nazo zinapitia uonevu wa vikwazo.

Kwa kumalizia Urusi imeamua kuisaidia KOKA ili ipate uzoefu utaona pia ni wataalamu wa jeshi la Urusi ndio wanawapa mafunzo ya awali wa anajeshi Wa KOKA kabla ya kuingia uwanja wa vita,Sasa Urusi itaombaje msaada wa kijeshi kwa nchi halafu ianze kulifundisha jeshi analoliomba msaada?
Mabeberu na wafuasi wao kwa kubadilisha mada ni hawajambo.
Hata hivyo wote tunafahamu humu kua Kila upande una allies (washirika)wake,Sasa inakuaje west anapeleka washirika wake vitani lakini Urusi akipeleka washirika wake inakua nongwa?
Zamani kulikua Kuna NATO na Warsaw Pact,WP ikavunjika je Urusi Hana haki ya kua na Allies wengine?

USA hata akipigana na kikundi kama Al-Qaida na Watalabani TU anachukua kundi la Allies wake pamoja na NATO je Urusi Hana haki ya kua na marafiki?
West waache uoga
 
Back
Top Bottom