Uchaguzi 2020 BBC Swahili wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa

Ni kweli kabisa, kama ilivyo kampeni za ccm za kuwaleta marais wa nje nyingine kuja kuwaombea kura, kinyume kabisa cha sheria za kimataifa, zinazokatisha nchi moja kutojiingiza kwenye siasa za nchi nyingine.
You are talking about sheria za kimataifa?! Unataka nilete humu ile video ya wazungu wa Lissu akiwemo Amsterdam na wenzake walichopanga dhidi ya Tanzania...wamepanga kuchochea maandamano na mauaji ili vurugu zitokee na kinachoitwa jumuiya ya kimataifa iitishe mkutano wa usuluhishi na Lissu...wazungu hao wanasema na kuropoka bila aibu kwamba ni lazima damu imwagike Tanzania...kuchomwa kwa ofisi za chadema ni miongoni mwa mikakati hiyo...
 
Kwa hyo mkuu kabudi ametuingiza chaka kuwa tutapata 50/50 ya mgawanyo?alafu mbona vyombo vya habari vya ndani havihoji ili jambo kuwa mkataba umesainiwa ikulu,hii imekaaje kiongozi wangu?
Vyombo vya Habari vipi tena Mkuu?? Vyote vilishawekwa mfukoni na mtu mmoja. Mfumo wetu wa Uongozi umeshanajisiwa na Mtu mmoja hivyo unahitajika kufumuliwa na kusukwa upya. Na hili litaweza kufanyika tu nje ya ccm na si vinginevyo.

Ukishakuta Kiongozi anaetumia mamlaka yake kuingilia uhuru wa Mihimili mingine kama Bunge na Mahakama basi usitegemee uhuru ktk kupata na kutoa Habari. Angalia magazeti Nchini yamepoteza mvuto. Hakuna wafuatiliaji wengi kama ilibyokuwa hapo awali. Vivyo hivyo ktk Vyombo vyetu vingine vya Habari.
 
Hata mimi mkuu nimeshangaa siku zote BBC walikuwa wapi?wanavizia kampeni ndio wanaanza kuhoji,Ila pia mimi kama mwananchi wa kawaida naishauri Serikali yangu mikataba kama hii iwe inajadiliwa bungeni na kuwekwa wazi,ili sisi wakaazi wa huku Busonzo tusisubiri mpaka BBC watuambie,
 
Wakuu Jana niliangalia BBC Swahili, wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa, hivi hiki chombo cha habari cha mabeberu kinatutafutia nini?

"Professorial rubbish". Alisema TL bungeni kuhusu tume ya makinikia ya Prof. Osolo. Mnakumbuka?
 
Wakuu Jana niliangalia BBC Swahili, wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa, hivi hiki chombo cha habari cha mabeberu kinatutafutia nini?

Ok
Hata lissu alisemea bbc kuwa tutapelekwa miga sijui mica
 
The power of dictatorships comes from the willing obedience of the PEOPLE they govern and if the PEOPLE can develop techniques of withholding their consent, a repressive regime will soon crumble. Happy Sabbath
Tyrants never give until disposition
 
Tundulisi si ana character zote za kibeberu , si bora jiwe ambaye hata kwao hataki kwenda
 
Kama ni waongo basi fungia Star TV ili watu tusisikie "uongo".
 
Ok
Hata lissu alisemea bbc kuwa tutapelekwa miga sijui mica
Hata mm nashangaa maana tuliambiwa na lisu kuwa tutashitakiwa MIGA matokeo yake hatujashitakiwa wala nn,pia tuliambiwa na Serikali kuwa makinikia hayataondoka na tutajenga smelter hapa hapa,lakini matokeo yake makinikia bado yanaondoka pia smelter haijengwa mpaka leo,Sasa sisi wakazi wa huku Katoro tuamini kuwa lissu alitudanganya na Serikali pia imetudanganya?au nyinyi wa huko mjini mnaonaje huko?
 
Wakuu Jana niliangalia BBC Swahili, wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa, hivi hiki chombo cha habari cha mabeberu kinatutafutia nini?

Tumepigwa kweli unadhani waongo?
 
Nilisikiliza taarifa yote ya habari...na mchambuzi huyu wa Chadema...very stupid indeed...BBC wamefanya hivyo makusudi kwa kumleta anayejiita mchambuzi kutoka Chadema..ni mkakati wa kampeni za Chadema
Lissu alisema ile report ya makinikia ni professorial rubbish sasa yametimia.
 
Issue ni kipi wanainchi wanakielewa zaidi kuhusu madini kwa awamu hii ya tano, hayo unayodai mapendekezo ndio yapo kwenye vichwa vya wananchi wengi kwa kuwa ndiyo yaliyosemwa sana au kuelezewa na hayo yaliyomo kwenyw mkataba wananchi wanahisi ndio yale yaliyokuwa yanapendekezwa.
Hivyo ni vema vipengele vilivyopo kwenye mkataba viwekwe wazi ili kutoa tafirsili iliyoshihi
 
Hoja ni je aliuosema yule mtaalam aliyekuwa anahojiwa ni uongo au ukweli? Jibu ni ukweli yaani Hadi kupigwa watu risasi ilikuwa ni kutafuta hisa 16% tuu? Huku si kupigwa ikizingatiwa watangulizi wa jiwe walifikisha umiliki Hadi adilimia 40 kwenye mgodi wa williamson,sasa jiwe ndio kafanyaje hapo? Labda alikuwa anatafuta pesa za kampeni almaarufu kushika uchumba maana mambo mengine yote yamesalia Kama zamani na mengine yamekiukwa kabisa kwa mujibu wa bbc na yule mtaalam waliomhoji
 
Ndio maana Lisu na cdm wamekuwa clear kwamba wao wanataka ubia na wawekezaji wenye uwezo na teknolojia sio vita,hapa ni Bora kuwesesha wazalendo kwa kuwapa mikopo ya mitaji kuliko kuwasubili wazungu kwa kila kitu
 
Kipi Bora kwako kuhoji sasa ili kuweka wazi ambacho hakiwezi kuhojiwa ndani au kukaa kimya tuendelee kupigwa bila kujua? Huoni Lisu alikuwa sahihi toka zamani Hadi sasa kuhusu madini?
 
Acha tu kuleta video, ilete na ikiwezekana omba airtime kwenye vyombo vyote vya habari ili kila mtu aone alichopanga Lisu na hao wazungu. Halafu nyie mkichezea matokeo ya box la kura, mtatuonyesha hao waafrika wanaowatuma tumwage maji.
 
Nilisikiliza taarifa yote ya habari...na mchambuzi huyu wa Chadema...very stupid indeed...BBC wamefanya hivyo makusudi kwa kumleta anayejiita mchambuzi kutoka Chadema..ni mkakati wa kampeni za Chadema
Acha ujinga basi kidogo! Alichozungumza Thabiti kinasikika kwa kila anayehitaji kusikia, hebu sasa wewe jibu hoja moja baada ya nyingine katika kile ambacho kimezunguzwa..
 
Acha ujinga basi kidogo! Alichozungumza Thabiti kinasikika kwa kila anayehitaji kusikia, hebu sasa wewe jibu hoja moja baada ya nyingine katika kile ambacho kimezunguzwa..
Kweli wewe ni Chadema ambao hawezi kuacha kutumia neno mjinga kwenye mijadala...
 
Wakuu Jana niliangalia BBC Swahili, wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa, hivi hiki chombo cha habari cha mabeberu kinatutafutia nini?

Mjadala wa Barrick imani yangu imefungwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…