Uchaguzi 2020 BBC Swahili wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa

Uzushi na upuuzi mtupu!
 
Kama ni waongo basi fungia Star TV ili watu tusisikie "uongo".
No BBC sio waongo, bali wamejikanganya kwa kuwategemea watu fulani fulani walio wadanganya makubaliano ya 2017 yamesainiwa, kitu ambacho sii kweli, that was only a draft, makubaliano yaliyosainiwa ni mkataba mmoja tuu!.
P
 
No BBC sio waongo, bali wamejikanganya kwa kuwategemea watu fulani fulani walio wadanganya makubaliano ya 2017 yamesainiwa, kitu ambacho sii kweli, that was only a draft, makubaliano yaliyosainiwa ni mkataba mmoja tuu!.
P

P kuna baadhi ya hoja za wadau humu umeshindwa kuzijibu nikusaidie mkuu?

Nimeshubiri sana ujibu hoja ya Teamanaconda kwenye post #30. Nilitaka kumjibu nikaona sio ustaarabu kudandia ingali nakuona bado kwenye uzi.

Itapendeza pia kumjibia muheshimiwa barafuyamoto naye naona ametoka kabisa, ile mimi imenitoka kidogo
 
Kuna wakati nalazimika kuamini kuwa hizi hasara tunazopata kama taifa sio kwamba viongozi hawajui(mbumbumbu) au labda inatokea kwa bahati mbaya HAPANA.
Hawa jamaa wanasaini mikataba makusudi kabisa wakijua % ngapi itaingia serikalini na % ngapi itaingia mifukoni mwao. Na ndio maana mtu anaingia kwenye nafasi za juu serikalini kachoka kachakaa, miaka mi-5 ukimwangalia anatoka ana pesa chafu hatari.
Halafu kuna nzi wa kijani wanakomaa na sisi humu kwenye mitandao wakijidai kutetea na kujidai kwamba ni wazalendo, hivi wanaujua uzalendo???
Leo hii sema posho zote zinafutwa na mishahara inapunguzwa, uone kama kuna atakayebaki na kung'ang'ania central zone. HAKUNA MZALENDO HATA M'MOJA PALE LUMBUMBA, WAMEJAZANA WAPIGAJI TUPU.
 
Kuna chochote kilichobadilika kwenye yale mapendekezo na mkataba uliosainiwa 2019?

Je utekelezaji wa mkataba umefikia hatua gani ?

By the way naipongeza serikali kwa kuanzisha masoko ya madini
 
Awamu ya tano walikuwa wanatengeneza regime mpya ya kuwawezesha kuiba wao wenyewe tu siyo kwa manufaa ya watanzania.

Wangekuwa na dhamira njema wangeshapeleka mikataba ya madini kujadiliwa bungeni kama sheria inavyotaka
 
Mkuu haya weka hapa tujionee wenyewe.
 
Hapo kwenye manufaa ya kiuchumi ya 50/50 ndipo tunahitaji ufafanuzi. Iweje tuwe na hisa ya 16% tupate manufaa ya kiuchumi ya 50/50?
Ni economic benefits not profits
 

Mkuu nitakujibu huja zako zote ngoja wenzangu watangulie kwanza. Kwenye hili Raisi amepambana haswa tuache kubeza..

Hata ile kuyazuia kwa muda makinikia japo yalikuja kuendelea kutoka, ilitosha kuwatia presha barrick na kuwaleta kwenye makubaliano mapya bila kuathirika na mikataba tuliyosaini kimakosa huko nyuma.

Kuhusu smelter nadhani hizo zilikuwa hoja za kuwapa hope wanachi na kuwafanya kuwa positive katika kile tunajaribu kufanya. Hata unapofungua biashara yoyote nadhani kuna hopes unakuwa nazo na hata kuziandika kabisa katika strategic plan japo kuna uwezekano usizifikie labda mpaka baada ya muda mrefu.
 
..barrick wametupiga.

..serikali ilisema tumeibiwa usd 191 billion.

..baada ya "majadiliano" tukakubali kulipwa usd 300 million.

..hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuibiwa 191 billion halafua akaridhika kulipwa 300 million.

..hapo ndipo barrick walipotupiga.
 
Ni kweli tumerudi kuwapigia magoti mabeberu, oooh tutachenjua mchanga hapahapa, kiko wapi sasa?
 
Mkuu nisaidie kuelewa kidogo hapa. Economic benefits tutakazogawana 50/50 ni zipi tofauti na hii share of profit?
Mambo mengi yaliyoanishwa kwenye hii 50/50 economic ni mambo yanayofall kwenye corporate social responsibility tu.
 
Mkuu haya weka hapa tujionee wenyewe.
Nikiweka hapa itakuwa issue kubwa mno...binafsi nimeiangalia ile video nikashangaa na kuogopa namna wazungu wale walivyoandaa mipango...yaani bila hata aibu wanataka watu wafe Tanzania ili iwe vurugu kubwa ...
 
Video ?.
 
Nikiweka hapa itakuwa issue kubwa mno...binafsi nimeiangalia ile video nikashangaa na kuogopa namna wazungu wale walivyoandaa mipango...yaani bila hata aibu wanataka watu wafe Tanzania ili iwe vurugu kubwa ...
Niwekee PM au nipe link niitafute.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…