BBC: Urusi imeipa Korea Kaskazini mapipa milioni moja ya mafuta

5523

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2014
Posts
2,275
Reaction score
2,410
Ni mwendo wa kula uliwe

Untitled.jpg

Urusi inakadiriwa kuipatia Korea Kaskazini zaidi ya mapipa milioni moja ya mafuta tangu Machi mwaka huu, kulingana na uchambuzi wa picha za satelaiti kutoka kwa Open Source Centre, kikundi cha utafiti kisicho cha faida chenye makao yake makuu nchini Uingereza.

Mafuta hayo ni malipo ya silaha na wanajeshi Pyongyang wameituma Moscow kuendeleza vita vyake nchini Ukraine, wataalam wakuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy, wameiambia BBC.
Uhamisho huu unakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa, ambavyo vinapiga marufuku nchi kuuza mafuta kwa Korea Kaskazini, isipokuwa kwa kiwango kidogo, katika jaribio la kukandamiza uchumi wake ili kuizuia kuendeleza silaha za nyuklia.

Picha za satelaiti, zilizoshirikiwa pekee na BBC, zinaonyesha zaidi ya meli kumi na mbili tofauti za mafuta za Korea Kaskazini zikiwasili kwenye kituo cha mafuta Mashariki ya Mbali nchini Urusi jumla ya mara 43 katika kipindi cha miezi minane iliyopita.

Picha zaidi, zilizochukuliwa za meli hizo baharini, zinaonekana kuonyesha meli hizo zikiwasili zikiwa tupu, na kuondoka zikiwa zimekaribia kujaa.

Korea Kaskazini ndio nchi pekee duniani ambayo hairuhusiwi kununua mafuta kwenye soko la wazi. Idadi ya mapipa ya petroli iliyosafishwa inaweza kupokea inapunguzwa na Umoja wa Mataifa kuwa 500,000 kila mwaka , chini ya kiwango kinachohitajika.
 
Awa BBC kwanza tunataka warepot kuusu Netanyahu kutakiwa kukamatwa popote alipo. Hii habari ya hana lkn adi leo wameichunia kuna Uzayuni mulendani sio kwa kimyaichi.
 
Shida Mrusi karamba mchanga Ukraine inabidi akodi askari North korea
Fita ni fita kikubwa mtu anachezea kichapo na pande la nchi analibeba,,,,,,,na kwa sasa NATO mje wazi tu uwanja wa mapambano badala ya kuvizia vizia tuone upande upi ni wa vidume na upi wa taarabu
 
Pia inasemekana yale makombora hatari mapya ambayo putin anajitamba nayo na yenyewe yametoka Korea kaskazini.
 
Fita ni fita kikubwa mtu anachezea kichapo na pande la nchi analibeba,,,,,,,na kwa sasa NATO mje wazi tu uwanja wa mapambano badala ya kuvizia vizia tuone upande upi ni wa vidume na upi wa taarabu
Yaani NATO waingie vitani nchi 32 kule urusi si litabaki vumbi tupu.,!

Ukraine tu taifa maskin na ata hawajulikami kwenye medani za vita sasa mwaka 3 russia hajatoboa anakodi askari toka north korea
 
Ni mwendo wa kula uliwe

View attachment 3158412

Urusi inakadiriwa kuipatia Korea Kaskazini zaidi ya mapipa milioni moja ya mafuta tangu Machi mwaka huu, kulingana na uchambuzi wa picha za satelaiti kutoka kwa Open Source Centre, kikundi cha utafiti kisicho cha faida chenye makao yake makuu nchini Uingereza.

Mafuta hayo ni malipo ya silaha na wanajeshi Pyongyang wameituma Moscow kuendeleza vita vyake nchini Ukraine, wataalam wakuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy, wameiambia BBC.
Uhamisho huu unakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa, ambavyo vinapiga marufuku nchi kuuza mafuta kwa Korea Kaskazini, isipokuwa kwa kiwango kidogo, katika jaribio la kukandamiza uchumi wake ili kuizuia kuendeleza silaha za nyuklia.

Picha za satelaiti, zilizoshirikiwa pekee na BBC, zinaonyesha zaidi ya meli kumi na mbili tofauti za mafuta za Korea Kaskazini zikiwasili kwenye kituo cha mafuta Mashariki ya Mbali nchini Urusi jumla ya mara 43 katika kipindi cha miezi minane iliyopita.

Picha zaidi, zilizochukuliwa za meli hizo baharini, zinaonekana kuonyesha meli hizo zikiwasili zikiwa tupu, na kuondoka zikiwa zimekaribia kujaa.

Korea Kaskazini ndio nchi pekee duniani ambayo hairuhusiwi kununua mafuta kwenye soko la wazi. Idadi ya mapipa ya petroli iliyosafishwa inaweza kupokea inapunguzwa na Umoja wa Mataifa kuwa 500,000 kila mwaka , chini ya kiwango kinachohitajika.
Vikwwzo vya umoja wa Mataifa vimfikie Israel na Hamas pia
 
Yaani NATO waingie vitani nchi 32 kule urusi si litabaki vumbi tupu.,!

Ukraine tu taifa maskin na ata hawajulikami kwenye medani za vita sasa mwaka 3 russia hajatoboa anakodi askari toka north korea
Hao NATO wenyewe wanajua mziki wa Hitler ulitulizwa na nani,,,maana karibia ulaya nzima ilishabebwa ila mjerumani akaja kupata wakati mgumu urusi,,,,,,,hao NATO nchi zao kulinganisha na Urusi hawana ubabe wowote kwenye medani za vita, zaidi wamezoea kupigana na vitaifa vya kuunga unga,,Ukraine mrusi anajua ni ndugu zake, wenye shida ni hao viongozi tu waliowekwa na wamagharibi ndo maana lazima itumike mbinu tofauti, unadhani angetaka afanye kama alichofanya Israel kule Gaza angeshindwa? Watu mipango tu ila angetaka kiev sahivi ingebaki magofu kama gaza
 
Ni kwel kabisa
 
Ni mwendo wa kula uliwe

View attachment 3158412

Urusi inakadiriwa kuipatia Korea Kaskazini zaidi ya mapipa milioni moja ya mafuta tangu Machi mwaka huu, kulingana na uchambuzi wa picha za satelaiti kutoka kwa Open Source Centre, kikundi cha utafiti kisicho cha faida chenye makao yake makuu nchini Uingereza.

Mafuta hayo ni malipo ya silaha na wanajeshi Pyongyang wameituma Moscow kuendeleza vita vyake nchini Ukraine, wataalam wakuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy, wameiambia BBC.
Uhamisho huu unakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa, ambavyo vinapiga marufuku nchi kuuza mafuta kwa Korea Kaskazini, isipokuwa kwa kiwango kidogo, katika jaribio la kukandamiza uchumi wake ili kuizuia kuendeleza silaha za nyuklia.

Picha za satelaiti, zilizoshirikiwa pekee na BBC, zinaonyesha zaidi ya meli kumi na mbili tofauti za mafuta za Korea Kaskazini zikiwasili kwenye kituo cha mafuta Mashariki ya Mbali nchini Urusi jumla ya mara 43 katika kipindi cha miezi minane iliyopita.

Picha zaidi, zilizochukuliwa za meli hizo baharini, zinaonekana kuonyesha meli hizo zikiwasili zikiwa tupu, na kuondoka zikiwa zimekaribia kujaa.

Korea Kaskazini ndio nchi pekee duniani ambayo hairuhusiwi kununua mafuta kwenye soko la wazi. Idadi ya mapipa ya petroli iliyosafishwa inaweza kupokea inapunguzwa na Umoja wa Mataifa kuwa 500,000 kila mwaka , chini ya kiwango kinachohitajika.
Rafiki wa kweli utamjua wakati wa shida!
 
Hao NATO wenyewe wanajua mziki wa Hitler ulitulizwa na nani,,,maana karibia ulaya nzima ilishabebwa ila mjerumani akaja kupata wakati mgumu urusi,,,,,,,hao NATO nchi zao kulinganisha na Urusi hawana ubabe wowote kwenye medani za vita, zaidi wamezoea kupigana na vitaifa vya kuunga unga,,Ukraine mrusi anajua ni ndugu zake, wenye shida ni hao viongozi tu waliowekwa na wamagharibi ndo maana lazima itumike mbinu tofauti, unadhani angetaka afanye kama alichofanya Israel kule Gaza angeshindwa? Watu mipango tu ila angetaka kiev sahivi ingebaki magofu kama gaza
Mkuu kabla hujenda mbali mrusi alikuja kupata msaada kutoka US ndio akafanikiwa vita ya Hitler, na Putin anajua hivyo vizuri
 
Mbona hao uingereza, ufaransa walipewa msaada na bado walichapika?? US hakumsaidia Urusi tu aliwasaidia wote waliokua wanapambana na Hitler ila Urusi tu ndo alieweza kumtuliza Hitler
 
Back
Top Bottom