BBC Swahili ni idhaa ya shirika la utangazaji la Uingereza inayorusha matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili, ikilenga kuzifikia nchi za Afrika Mashariki zinazotumia lugha hiyo. Pamoja na na kuripoti taarifa kutoka maeneo mengi duniani pia imekuwa ikitilia mkazo dhidi ya masuala mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Ipo taarifa inayosambazwa kupitia vikundi vya mtandao wa Facebook kuwa BBC Swahili wamechapisha taarifa yenye kichwa cha habari 'Wafahamu wanaharakati maarufu kwa kuchochea machafuko nchini mwao' huku ikitumika picha ya
Maria Sarungi katika Chapisho hilo.
Je, ni uhalisia wa taarifa hiyo?
Kupitia utafutaji wa kimtandao kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) JamiiCheck Imejiridhisha kuwa taarifa hiyo imepotoshwa uhalisia wake kutoka taarifa rasmi
iliyochapishwa na BBC Swahili.
Chapisho hilo lilihaririwa kwenye kichwa cha habari ili kupotosha uhalisia, kwani BBC Swahili katika taarifa
iliandika 'Wafahamu wanaharakati maarufu Afrika Mashariki' ikiambatana na utangulizi wenye maneno 'Wanaharakati maarufu wanaozikosesha usingizi nchi zao Afrika Mashariki'
Aidha katika taarifa kamili iliyochapishwa katika tovuti ya BBC Swahili, ilitaja orodha ya wanaharakati ambao wanaonekana mwiba kwa mataifa yao Afrika Mashariki na kati ya hao ikimtaja Maria Sarungi kama mwanaharakati aliyejikita zaidi kwenye kutaka mabadiliko akitumia mitandao ya kijamii zaidi kutekeleza azma hiyo.
Inataja Kampeni iliyompa umaarufu zaidi ni
"Change Tanzania iliyoanza kama hashTag kwenye mtandao wa Twitter, na kwa sasa akiendesha mijadala mikubwa inayohusisha maelfu ya Watanzania kupitia jukwaa la "Space" la Twitter.
Mijadala hii kwa kiasi kikubwa inakosoa mamlaka kwenye maeneo mbalimbali, lakini pia inachochea ushawishi wa masuala mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya katiba ya nchi, kuondolewa kwa sheria kandamizi na kuchochea uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari."