Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wacha uongo Bagamoyyo ni mara ngapi tumeandika hapa kwamba Jamii Forum imenunuliwa, umbeya huo.
Wachilia mbali kuhojiana naye, hata kuripoti tu hiyo habari, hivi vyombo vya habari vya habari vya hapa nchini, vitaona kama vinatenda kosa la jinai.......Hivi hiyo tuzo aliyopata, kuna chombo chochote cha habari cha ndani kinaweza fanya mahojiano naye? Au hata hilo wanaliogopa?
Bila ku-sacrifice kwa huyu Melo, sijui hali ya upatikanaji wa habari hapa nchini ungekuwaje
Kwa kuwa tunajua kuwa Serikali hii ya awamu ya tano, wanataka kutulazimisha watanzania wote tujiunge na "Praise and worship team for Magufuli"
Wachilia mbali kuhojiana naye, hata kuripoti tu hiyo habari, hivi vyombo vya habari vya habari vya hapa nchini, vitaona kama vinatenda kosa la jinai.......
Badala ya kuuona huo upokeaji wa tuzo kama ukombozi kwa vyombo vya habari hapa nchini, ambavyo vinapitia katika mazingira magumu sana ya utendaji kazi wao
Ni kweli chombo pekee huru cha habari kilichobaki Tanzania ni JamiiForums.
Ambapo ni vigumu kununulika maana kuna mamia ya watu huru walio member na wageni wanaochangia mada bila hofu yoyote.
Vyombo vingine ama vimenunulika kusifia au vimeamua kujiweka mbali na habari ambazo wanahisi zitawaudhi watawala.
Mfano ni vigumu vyombo vya habari kufanya taarifa za uchunguzi, kuhoji au kukumbushia matukio yanayoiannika serikali kweupe.
Mfano vyombo vya media wataripoti wabunge wa CHADEMA ni watoro Bungeni bila kukumbushia kuwa wamefunguliwa kesi nyingi za utata na utawala wa awamu ya 5 ili wasiweze kuwepo Bungeni kwa muda mrefu.
Lakini JamiiForums habari kama hiyo ya 'watoro' wataongeza na angalizo, historia , video clips ,matamko ya watawala n.k ndiyo yamewafanya wapinzani kuwepo ktk hali ngumu na hatari kisiasa.