BBC waipongeza JamiiForums, wadai ndio tegemeo pekee la habari za uhakika nchini Tanzania, wampongeza Melo na watendaji wake

Bila ku-sacrifice kwa huyu Melo, sijui hali ya upatikanaji wa habari hapa nchini ungekuwaje

Kwa kuwa tunajua kuwa Serikali hii ya awamu ya tano, wanataka kutulazimisha watanzania wote tujiunge na "Praise and worship team for Magufuli"
 
Wacha uongo Bagamoyyo ni mara ngapi tumeandika hapa kwamba Jamii Forum imenunuliwa, umbeya huo.

Siyo Nyumbani Tanzania tu bali Kimataifa pia JamiiForums inatambulika kwa kuwa ni chanzo cha watu-huru kupata haki ya kujadiliana, kupashana habari kwa uwazi na ukweli na kukubaliana kutofautiana kwa hoja, msingi mkubwa ukiwa information is power. Power hii hutufanya kufanya maamuzi sahihi ya kijamii, kibiashara, kiuchumi na kisiasa kwa ajili ya kuchochea maendeleo ktk sekta zote.
21 Nov 2019
CPJ is honored to present its 2019 International Press Freedom Award to Maxence Melo Mubyazi, a champion of online freedom of expression in Tanzania. He is the co-founder and managing director of Jamii Forums, a popular East and Central African website and discussion forum that is a source of breaking news. He has been charged under the country's restrictive Cybercrimes Act and, in 2017, appeared in court 81 times.
Source: Committee to Protect Journalists CPJ
 
Hivi hiyo tuzo aliyopata, kuna chombo chochote cha habari cha ndani kinaweza fanya mahojiano naye? Au hata hilo wanaliogopa?
Wachilia mbali kuhojiana naye, hata kuripoti tu hiyo habari, hivi vyombo vya habari vya habari vya hapa nchini, vitaona kama vinatenda kosa la jinai.......

Badala ya kuuona huo upokeaji wa tuzo kama ukombozi kwa vyombo vya habari hapa nchini, ambavyo vinapitia katika mazingira magumu sana ya utendaji kazi wao
 
Bila ku-sacrifice kwa huyu Melo, sijui hali ya upatikanaji wa habari hapa nchini ungekuwaje

Kwa kuwa tunajua kuwa Serikali hii ya awamu ya tano, wanataka kutulazimisha watanzania wote tujiunge na "Praise and worship team for Magufuli"

Wacha majungu wewe, wewe ulikwa mfaidika wa rushwa ambayo ilikithiri sasa unalialia nyau unataka huruma ya wananchi. JF tangu mwanzo tunapinga sana a bunch of imbeciles ambao kazi yao ni kupotosha tu kwa sababu ya matumbo yao. Ni matumaini yangu sasa JF will clean its act na kuondoa watukanaji wakuu ambao wamo humu kwa upotoshaji.
 
Hili nilshalizungumzia hapa,JF ndio forum yenye kutumiwa na kila mtanzania,wenye nyadhifa zao na wasio kuwa nazo, wote wanapita humu kila iitwayo siku.Hongera JF na hudumu ili watoto na wajukuu wetu wakutumie wakati wao ukifika.Hongereni members wote kwa mada zenu tunaziona humu kila siku.
 
Tumefika pabaya sana mkuu
 
Where we dare say truth .
I disapprove what you say but i will defend to death your right to say it.
JF oyee.
 
Maxence: you a a true inspiration and a beacon of hope to millions of Tanzanians. Via you we have this platform where we can air our views without fear. Please don’t let us down, hommie!!
God be on your side hommie
 
Ni kweli vyombo vingi vya habari vimekua "Heavily Compromised" kiasi kwamba vimekuwa ni kero tu, vinasifia hata vitu ambavyo havipo.

Sisi wengine local information outlet iliyobaki ni hii Jamii Forums, hayo mengine yaliyobaki yamebakia umbeya tu na kuumiminia huu utawala sifa feki.
LONG LIVE JF.
 
Humu sio huru Pia, sema mwenye hii forum anamisimamo ndio pona yetu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…