Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

Mkuu tuna mtu Japan next time unakuja hapa unaomba ushauri kabla ya kuagiza hiki kisima cha busara ingawa wahuni wapo humu pia ungeunganishwa kule angeikagua kabla ya kuja usingejuta ka unavyojuta sasa.
Nasikia mandinga huko ni bei chee sana mnadani ni kweli au ?
 
Tafuta boya mkubwa zaidi yako umbambikie akafe nalo mbele.
 
Duh mkuu kweli umetoboka sana
 

Ni bora uende kwenye showrooms zetu za hapa Bongo itafute gari na ujiridhishe km ilizotenbea kama ni sawa uchukue.

Hayo makampuni kama ya Befoward, SBT siku hizi magari mengi wanayoyauza yako kwa Third Party. Kabla ya kulipia omba upewe condition report ujiridhishe na hali ya gari kabla ya kulipia. Ndio maana wanakupa DEPOSIT INVOICE kwa SBT ama INVOICE kwa Befoward na ukisoma masharti yaliyoandikwa kwenye hizo Invoice unaweza ogopa kulinunua gari. Ukopata gari nzuri ni bahati na ukipata gati lenye matatizo inakuwa bahati mbaya.

Magari kama yapo kwenye Stock yao watakupa COMMERCIAL INVOICE na hayo magari yanakuws kwenye hali nzuri.
 
Walikupa invoice imeandikwa INVOICE ama COMMERCIAL INVOICE?

Kama imeandikwa INVOICE ilo gari haliko kwao, lipo kwa THIRD PARTY na magari hayo unaweza ukayaona kwenye website zaidi ya moja yaani Befoward, SBT nk.
 
Customer care ya Be foward ni ya hovyo mnoo
 
Wote wahuni.

SBT kwa magari yapo kwa Third Party omba invoice, utaona gari ni ya grade gani, kama 1, 2, 3 hachana nalo.
Angalau kuanzia grade 4.

Kwa magari yapo kwenye Stock yao watakupa condition report.
 
Ungeomba ushauri kabla ya kwenda front na kuagiza kupitia be forward.
 
Unanunuwa gari zinazongoja kwenda scrap yard huko Japan halafu unakuja kulalamika? Ujinga huo.

Usinunuwe gari yenye zaidi ya miaka mitano ni ugonjwa wa moyo tu.
 
Naona hujaupenda ukweli, wenzenu Kenya siku nyingi walipiga marufuku gari chini ya miaka mitano kuingizwa Kenya, labda liwe la kuingia na kutoka tu.
Watanzania wangapi wana uwezo wa kununua gari za chini ya miaka mifano? Au unataka kufurahisha kijiwe mkuu? Hebu anagalia Vitz ya 2019 bei na ushuru wake na useme wangapi wataona heri kununua hiyo.
Gari ya miaka 10 kama imetunzwa vizuri haina shida kabisa. Na ndio maana kuna grading ya gari za mtumba bila kujali mwaka wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…