Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

Utakuwa ulivutiwa na bei, sikunyingine nunua zilizo kwenye stock za japan na si vinginevyo. Hapo shida ni mnunuzi kutokuwa makini.
Suala sio bei, hizo zote ni gari zipo kwenye kampuni ya Be forward. Singapore ni tawi la Beforward na wale ni wao wenyewe. Hata pesa nillipa kupitia account ya Be forward Japan. Na kama gari wameona ina shida kwanini hawakuandika kwenye statement yao au kwenye mawasiliano niliyodanya nao watu wa Japan???
 
Gari mpaka kufika 26M, mbali ya ushuru. Ilipofika tu service kwenye yard ya Be Forward ilikwenda zaidi ya 250,000 maana TBS walikataa kurelease gari. Baada ya gari kutoka nimelipeleka gereji nyingi sana na nimetumia zaidi ya 10,000,000 kujaribu kulirepair lakini wapi. Mpaka nilinunua Gear Box mpay lakini wapi.!
Duh..
Pole mkuu
 
Kama 26m ni kabla ya ushuru maana yake imekula kama 40m including ushuru. Pole sana
Ndio hivyo na gari ipo juu ya mawe, inaniumiza sana. Mbaya zaidi Be forward hawakutaka kunisaidia kwa lolote. Imenikatisha sana tamaa ya kutumia Be forward, na sifahamu sana mitandao mingine ambayo ni genuine ya kuagiza magari
 
Suala sio bei, hizo zote ni gari zipo kwenye kampuni ya Be forward. Singapore ni tawi la Beforward na wale ni wao wenyewe. Hata pesa nillipa kupitia account ya Be forward Japan. Na kama gari wameona ina shida kwanini hawakuandika kwenye statement yao au kwenye mawasiliano niliyodanya nao watu wa Japan???
Alphard Mil 26???? Na bado umeuziwaa garasaa aisee mbonaa balaaa.. Bongo naona alphard used namba D zimesimama bei mil 15 na less.. Pole sana mkuu mil 10 kutumia kwenye matengenezo sio mchezooo
 
Gari mpaka kufika 26M, mbali ya ushuru. Ilipofika tu service kwenye yard ya Be Forward ilikwenda zaidi ya 250,000 maana TBS walikataa kurelease gari. Baada ya gari kutoka nimelipeleka gereji nyingi sana na nimetumia zaidi ya 10,000,000 kujaribu kulirepair lakini wapi. Mpaka nilinunua Gear Box mpay lakini wapi.!
Duh! Pole sana aise, hiyo naona hasara kubwa kwa kweli! Ila ndiyo maisha na changamoto zake!
 
Ndio natafuta gari ya familia, iwe kuanzia 2014
Kwa izo Kia, kuanzia 2010 ni kali sana kuona mbadala ngumu.

Ila kama tu family car, ungeanza kwa kujiuliza unataka minivan (mfano Alphard) au SUV (kama Harrier), hafu issue ya engine size (kwaajili ya fuel consumption) na mwisho ndio ije matumizi yako sana sana ni yapi?

Unaweza nunua gari la familia (mfano Alphard) kwaajili ya Familia kutoka out ambapo ni Jumapili kanisani, na December mnaenda Moshi na mara moja kwa mwezi kwenda beach.

So siku zingine unakua unatembea na bonge la gari kwenda na kurudi kazini peke yako, ukipambana na challenge za parking, na driving kwenye barabara zetu finyu
 
Wakuu natumai mu wazima!

Kuna wimbi la Be Forward kuleta magari mabovu ambayo yanasabibisha usumbufu mkubwa kwetu sisi wateja.

Nimenunua Alphard- nikaambiwa imefanyiwa mpaka na Inspection, na tena Be Forward Tanzania ndio walifanya clearance. Sasa cha ajabu gari imefika inavuja oil, pia imepigwa rangi nyeusi kumbe Original color ilikuwa ni Nyeupe, ikabidi tena ifanyiwe service hapa Tanzania kwenye yard ya Be Forward ndio TBS wakaipitisha.

Lakini gari bado ina matatizo mengi sana ya check engine, rejeta, masega na Engine box. Nimejaribu kufuatilia Be forward Tanzania wananijibu sababu niliagiza moja kwa moja Japan na Singapore hiyo haiwahusu. Nimefuatilia ilipotoka wananizungusha bila majibu ya kueleweka. Sasa nimeishia kupaki gari sababu haina nguvu na injini inachemsha.

Naomba mnisaidie kama kuna mwenye ushauri wa nini cha kufanya.

Asanteni wakuu.
Pole sana mkuu sikuhizi ushindani ni mkubwa sana sie wengine tumeamua kabisa kuwa na watu wetu japan kwa ajili ya kukagua gari moja kwa moja.

Pili kuna documents ulinyimwa iwe ni kwa kutokujua au kwa kujua na mwisho alphard kwa singapore mpka inafika dar inaweza kufikia mpka 22m au hata 18m sababu gari za kule nyingi ni low ended car mtu akiagiza gar singapore ana tofauti ndogo sana na aliyeagiza gari Zanzibar.

Mwisho kama ni mkazi wa dar ziko kampuni nyingi sana sku hizi zinauza magari hapa hapa dar kwa bei kama ya japan unakagua chuma yako unajiridhisha unatumia ipo alphard ofisini hapa mwaka 2007 ungekuwa na 25m tungekupa au kama utaongeza hela tuje ikagua hyo yako tuvunje uongeze hela tukupe hii
 
Duh hii lazima iwe 2nd generation sfter facelift kuanzia (2012-2014), na iwe Auction Grade 4.0 kwenda juu.

Pole sana mkuu. Pesa nyingi sana.
Ni ya 2014, gari haiwezi kwenda hata Kariakoo inachemsha! Naomba ushari nifanyeje na hii gari. Je Toyoto Tanzania wanaweza nisaidia, maana gereji za mitaani hii imewashinda
 
Kwa izo Kia, kuanzia 2010 ni kali sana kuona mbadala ngumu.

Ila kama tu family car, ungeanza kwa kujiuliza unataka minivan (mfano Alphard) au SUV (kama Harrier), hafu issue ya engine size (kwaajili ya fuel consumption) na mwisho ndio ije matumizi yako sana sana ni yapi?

Unaweza nunua gari la familia (mfano Alphard) kwaajili ya Familia kutoka out ambapo ni Jumapili kanisani, na December mnaenda Moshi na mara moja kwa mwezi kwenda beach.

So siku zingine unakua unatembea na bonge la gari kwenda na kurudi kazini peke yako, ukipambana na challenge za parking, na driving kwenye barabara zetu finyu
Mitsubishi Outlander SUV 7 seaters unaizungumziaje mkuu?
 
Ni ya 2014, gari haiwezi kwenda hata Kariakoo inachemsha! Naomba ushari nifanyeje na hii gari. Je Toyoto Tanzania wanaweza nisaidia, maana gereji za mitaani hii imewashinda
Mkuu, unataka kupeleka Toyota Tanzania? No way.. Kwa humu JF namjua fundi mmoja mzuri sana JituMirabaMinne ungeanza nae. Kwasababu gari la kisasa 2014 lazima lifanyiwe diagnosis. Na yeye ni Master.
 
Back
Top Bottom