Moja ya shuhuda nzito za kufunga mwaka,ni shuhuda za msaanii wa muziki wa injili Beatrice Mwaipaja akionesha vita vikali alivyokabiliana navyo na huenda ataendelea kukabiliana navyo dhidi ya ibilisi na majeshi yake.
Vita vikali mno lakini hatimae ninamtia moyo atashinda kwa jina ya Kristo kwani yeye Kristo alishinda vita hivi.
Niliwahi kumsikiliza Rose Mhando akisimulia vita vilivyomkabili hadi Mungu kwa njia ya Kristo Yesu kumshika mkono tena lakini kisa cha huyu Beatrice kimenilazimu niandike hapa.
Natamani nimwambie kuwa ,ijapo amefunguliwa kupitia mtumishi wa Mungu ambaye amemtaja kama baba yake wa kiroho,asije akaingia kwenye mtego mwingine wa imani yake kujengwa juu ya mtumishi yeyote hapa duniani.
Imani yake aijenge juu ya mwamba imara ambaye ni Kristo Yesu pekee.
Watoto wa Mungu wengi wameingia kwenye mtego wa ibilisi kwa kujenga imani zao juu ya watu ambao Mungu amewapa neema ya huduma mbali mbali za kiroho.
Wanasahau chanzo cha msingi wa wokovu ambaye ni Kristo Yesu. Na wengi wanamfanya Kristo Yesu kama namba mbili.Ila Mungu ni Mungu mwenye wivu mkubwa na sifa na utukufu ni vyake milele na milele Amima.
Soma Yohana 8:32 imeandikwa " Tena mtaifahamu kweli,nayo hiyo kweli itawaweka huru"
Uhuru kutoka vifungo vya giza,ni kuifahamu kweli.Ukiifahamu kweli,unawekwa huru.
Mungu baba,wa Yesu Kristo azidi kujifunua kwako.Naomba watumishi wa Mungu tutumie muda wetu kumuombea huyu dada ili asinase kwenye mitego ya hila ya ibilisi ambayo Mungu akikufunulia,utaogopa sana kwa kuwa huenda watumishi unaowaamini,ukagundua ni watumishi wa giza