KERO Begi langu limepotea Airport Dar, naomba mamlaka husika ichukue hatua stahiki kulingana na taratibu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
 
Pamoja mnapandapanda ndege hizo bado kwenye cm yako huna namba ya wakili
 

Katika vitu ambavyo vimewekewa sheria ya kuvilinda ni pamoja na Bank na ndege (flights).
hata siku moja usijekukimbilia Mahakamni bila kupata ushauri wa kisheria... unaweza kuishia kupoteza hela zako bure...
 
Katika vitu ambavyo vimewekewa sheria ya kuvilinda ni pamoja na Bank na ndege (flights).
hata siku moja usijekukimbilia Mahakamni bila kupata ushauri wa kisheria... unaweza kuishia kupoteza hela zako bure...
Unaongelea Tanzania ama nchi gani?

Unaelewa kuwa hata Tanzania nayo ina mikataba ya kimataifa ya banking na mambo ya anga, kama mambo ya Montreal Convention, kwa hiyo sheria hizi si za nchi moja, ni mikataba ya kimataifa inayotambulika karibu dunia nzima?

Hata Tanzania kuna wakili ali sue ndege, nafikiri ilikuwa Precision, iliyokuwa cancelled bila kumuarifu akashinda. Sasa hizo sheria za kulinda ndege zilikuwa wapi?

Haki ni haki tu, bank au shirika la ndege kulindwa dhidi ya kuwajibika taasisi hizo zinapokosea si haki.

Na of course mtu hatakiwi kukimbilia mahakamani bila ya ushauri wa mwanasheria, popote pale, kwa kesi yoyote ile, so that goes without saying.

Hii hapa kesi ya Hassan Othman Hassan, official wa Simba SC aliishitaki Turkish Airlines akashinda kesi mahakama ikaamuru alipwe shilingi milioni 36.


Hii hapa kesi nyingine Martin Kisyanju vs Emirates Airlines

Martin Kisyanju alishinda kesi akalipwa shilingi milioni 106.

 
Mkuu, nina hakika umenizidi umri mpaka kipato, ila kama mdogo wako naomba nishauri jambo.

Nilishawahi kukutana na kadhia hii ya kupotelewa na mzigo na nimeshakaa sana vikao kule TCAA.

Kiufupi kwanza siijui iimani yako, ningeomba kama ni mtu wa imani jambo hili lihame kutoka kwenye ushindani wa kisheria na ukubali kuna kupata na kukosa. , ruhusu hali ya utulivu wa nafsi ifanye kazi.

Sitaki nioneshe kwamba vitu vilivyopotea havina thamani kwako, naelewa kuna muda mzazi unatamani zawadi ifike kwa mhusika ili ueendelee kujenga bonds na watotot na kuwakuza vile upendavyo. Hivyo uchungu na thamani ya hivyo vitu naelewa mno.

Turudi kwenye jambo lako, Hiyo montreal convention, inataka ndani ya siku 7 tangu kupotelewa mzigo uwe umejaza form pale lost and found, nakumbuka nilipewa na watu wa swissport.

Kama ndani ya huo muda hukujaza pia shida inaanzia hapo, japo kama unaushahidi walisema mzigo utafika nina imani watakupa haki ya fidia

Pia kama mzigo ni checkin baggage hautalipwa vilivyokuwemo ndani, utalipwa kama fidia ya kupotelewa kwa mzigo.

Mzigo utalipwa thamani sawa na kilichomo kama uliuclaim value yake kwenye shirika husika, otherwise hutolipwa hata uende wapi utapewa tu fidia hata hiyo 400usd ni nyingi

Kingine vikao vya kusikiliza kesi pale TCAA vitakuchukua muda huwa vinafata procedure mpaka upangiwe tarehe unajikuta mda unazidi kupotea.

Hivyo sijui kama uliuclaim huo mzigo ila ninachokuomba funika kombe mwanaharamu apite. Ni mitihani kama mitihani mingine. Ila kama unaamini utaweza kupata haki yako, bado nakuombea.
 
Sahihi kabisa, ajaribu kwanza Swissport wautrack kama ulitoka, na point ya mwisho umeonekana wapi. Ila kama hakuna data za hlo bag kuna asilimia kubwa limebaki S.A
 
Sahihi kabisa, ajaribu kwanza Swissport wautrack kama ulitoka, na point ya mwisho umeonekana wapi. Ila kama hakuna data za hlo bag kuna asilimia kubwa limebaki S.A
Hakuna ushirikiano ataupata kwa hao Swissport kwa sababu hawana mawasiliano ya moja kwa moja na SA mimi nineacha beg mara nyingi sana nikiwaagiza watu wanayapata kule baada ya kupakia ndio hawa Swissport wanakua na taarifa mteja wangu juzi kaacha beg SA kesho wanapakia linakuja aliponipa taarifa nikamwambia tumtumie hela ya mafuta dogo mmoja Jhb kaenda leo kakuta beg aliweka engine kit ya hilux wakaamua kulipitisha Scanning kwa utaratibu huo lazima lichelewe kwenye flight unayosafiri nayo..
 
Sure, kama mtoa mada ataona post yako ninaimani atapata pa kuanzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…