Beginners: Tujifunze kufanya Diagnosis ya Magari wenyewe kabla hatujaenda Gereji!

Mkuu, hii OBD naweza tumia kwenye Rav 4 yangu pendwa old model ya 1996?
Akikujibu unitag. Mana mie huwa natumia diagnosis yenyewe kwa kuunga E1 na T4. Then una count check engine blinks ndio codes kisha unasolved. Ila nikiipata hiyo ya kusoma OBD1 Itakaa vizuri. Ni vyema aelewe pia diagnosis box ya hii gar pendwa ipo mbele kwenye hood
 
Hii njia kuna mtu alinielekeza napenda siku utoe somo mkali ya kucount blinks.
 
Mkuu nini kinaweza kuwa kinasababisha engine ku vibrate sana, wakati wa kuwasha gari, ila engine ikipata joto inapunguza mtikisiko?

Na pia ikiwa speed 90+ steering inacheza cheza/ vibrate

NB chuma ni carina
 
Mkuu nini kinaweza kuwa kinasababisha engine ku vibrate sana, wakati wa kuwasha gari, ila engine ikipata joto inapunguza mtikisiko?

Na pia ikiwa speed 90+ steering inacheza cheza/ vibrate

NB chuma ni carina
Happ sababu mkuu zinaweza kua nyingi sana, kuanzia issue za engine, mechanical au ikawa issues ndogo tu ya matairi hapo inapokua kwenye mwendo.

Nashauri, anza na service ndogo kwenda kubwa.

Mfano angalia oil, plug, na coils, kisha angalia alignment na balance kwenye iyo issue ya pili.
 
Tunazipataje Mkuu? Nipe location na namba pia
 
Naitaka sana hii kitu
 
Mkuu Mad Max naomba unifahamishe the best multi-diagnostic kwa sie vihiyo wa mechanics, ili tuondokane na kudanganywa kila wakati
 
Hamna kitu kibaya kama kwenda kwa Dr na ugonjwa wako kichwani. Nazijua sana diagnosis machine. Unaweza kupima ikakwambia tatizo ni kitu fulani. Lakini kama sio mzoefu na hio gari au ufundi wa hio gari utabadilisha hicho kitu na tatizo lisiishe. Kumbe kuna jitu kingine kidogo kinasababisha hicho kikubwa kisome fault.
Kuna wajinga niliwapelekea gari yangu ikazingua AC, wakapima wakasema expansion valve imekufa, nikawapa hii hapa wekeni. Kuweka hola AC bado haifanyi kazi. Wakasema kwasababu kifaa kingine basi system haisomi mpaka tufanyie reset , nikawaambia sawa. Wakafanya wafanyavyo bila bila.
Nikaondoka na gari yangu nikampelekea jamaa ambae ndio huwa anaitengeneza mambo ya kawaida nikamwambia AC inazingua nikamwachia. Kesho yake asubuhi ananipigia njoo uchukue gari tayari. Wala hakuniambia kuwa kabadili kitu chochote wala sikumuuliza tatizo lilikuwa nini nikamlipa hela aliosema nikaondoka.
Kwahio unatakiwa ujue kutafsiri codes, na kujua kuna codes ni scapegoat tu ila tatizo linaweza kuwa kitu kingine kabisa ndio kinasababisha code ikambie ni kitu hiki.
 
Mkuu habari,
Nina toyota Allex, changamoto yake ni kuwa, nikiwasha, engine ikipandisha temperature inakuwa fresh, sema ikitokea nimezima, aiseee.. kuwaka inakuwa na changamoto sana, yaani hadi niiache ipoe kabisaaa... changamoto inaweza kuwa nini!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…