SI KWELI Bei elekezi ya ARV ni Tsh. 76,000 baada ya USAID kusitisha misaada

SI KWELI Bei elekezi ya ARV ni Tsh. 76,000 baada ya USAID kusitisha misaada

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu

Nimeona taarifa inayoeleza kuwa bei elekezi ya ARVs ni shilingi elfu sabini na sita kwa mujibu wa wizara ya afya. je, ni kweli?

1738735399575.jpeg
View attachment 3225724
JAMII CHECK_ITV_SIKWELI.jpg
 
Tunachokijua
ARV inasimama kwa niaba ya antriretroviral hizi ni dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (Upungufu wa Kinga Mwilini) kwa waathirika. Dawa hizi zimekuwa zikitolewa kwa waathirika wa ugongwa kulingana na amelekezo ya wataalamu wa afya.

Taaarifa iliyotolewa na waziri wa afya kwa wakati huo (2023) ilieleza kuwa Kiwango cha Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) na wanatumia dawa za Kufubaza VVU (ARV) ni asilimia 97.9 kulinganisha na asilimia 93.6 mwaka 2016/17. Aidha, kiwango cha wanaotumia dawa na wamefubaza VVU ni asilimia 94.3 mwaka 2022/23 kulinganisha na asilimia 87 mwaka 2016/17.

Waziri alieleza pia kuwa anashakuru mashirika ya kimataifa kwa kuunga mkono juhudi hizo za kupambana na UKIMWI likiwemo shirika la USAID. USAID ni shirika la Marekani kwa ajili ya maendeleo ya kimataifa, shirika hili linakadiriwa kuwa na budget ya dola Billion 40 za Kimarekani sawa na Shilingi zaidi ya Trilioni 100 za Kitanzania (101,151,160,000,000 Tsh).

Baada ya utawala mpya wa Donald Trump kuanza kazi January, 2025 nchini Marekani kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika nyanya mbalimbali ikiwemo kusitishwa kwa muda huduma za USAID, jambo ambalo limekuwa na athari kubwa ikiwemo kwenye kada ya afya kwani walikuwa awafadhili pia wa dawa za kufubaza makali ya UKIMWI.

Madai

Kupitia mtandao wa Facebook mtu mmoja alichapisha taarifa akieleza kuwa Wizara ya Afya Tanzania imetoa na kutangaza bei ya dawa za ARV baada ya USAID kusitisha huduma zake;

“WIZARA YA AFYA TANZANIA IMETOA NA KUTANGAZA BEI YA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA VIRUSI VYA UKIMWI (ARV) KUWA NI SHILINGI ELFU SABINI NA SITA IMETOLEA UFAFANUZI KUWA DAWA IZO AWALI ZILITOLEWA BURE NA WAISANI AMBAO NI (US AIDS) AMBAO KWASASA WAMEJIONDOA RASIMI IVYO DAWA IZO KWA SASA ZINAZALISHWA LAKINI ZITAUZWA NA KUTOLEWA USHURU KAMA BIDHAA NYINGINE KUTOKANA NA KUSHUKA NA KUPANDA KWA THAMANI YA DOLA YA MAREKANI”

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia Taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli na ina lengo la kupotosha Umma. Ufuatiliaji umebaini kuwa grafiki iliyotumika imehaririwa na siyo halisi kutoka kwa Millard ayo updates aidha ITV live Tanzania inayoonekana siyo ukurasa rasmi wa ITV Tanzania.

Aidha JamiiCheck imebaini mapungufu katika uandishi wa taarifa hiyo mathalani neno izo badala ya hizo, ivyo badala ya hivyo, waisani badala ya wahisani, US AIDS badala ya USAID, matumizi ya herufi kubwa tupu.

Vilevile kiungo (link) iliyoambatanishwa na Taarifa hiyo inaelekeza kwenye kundi la ITV YETU. NA MATUKIO la Facebook, ilhali kituo cha ITV Tanzania kinatumia ukurasa (Page) na siyo kundi (Facebook group) na ukurasa rasmi wa ITV ni ITV Tanzania.

Wizara ya Afya kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii walikanusha kuhusu taarifa hiyo. Tazama hapa

Februari 8, 2025, Wizara ya Afya ilitoa taarifa kueleza kuwa inawahakikishia wananchi kuwa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI haizuzwi na zipo za kutosha. Tazama hapa
Tanzania is a sovereign state, tunalipa kodi, kwa nini tutegemee kodi za wananchi wa marekani kuendesha na kusimamia mifumo yetu ya afya???

Mbona Kodi zetu zinatosha kununua ndege ya Raisi, V8 new models za viongozi wa Kiserikali kila mwaka, tunaweza kununua magoli yanayofungwa na timu zetu Simba na Yanga kwenye michezo ya kimataifa n.k.

Siku tukiamka tukakuta marekani imetoweka kwenye uso wa dunia huo ndio utakuwa mwisho wetu pia???!!!
 
Tunaokuka pipi Kila siku ndoto za parapanda ni nyingi kichwana.

Nawaza kufuata dozi mwaka, za waliokufa na kukimbia matibabu.

Tafadhali sana, Dr mwigulu anzisha tozo ya arv kwenye vocha, umeme, mafuta na miamala yote.
 
Trump kaza hapo hapo mwanawane....wacha waafrika wafe tuu hawana maana yoyote hapa duniani.
Yaani kwanza trump unapaswa na kuwazibia waafrica marais kuingia states kwa mwaka mmoja wafanye mambo nchini mwao. Wale watakao onyesha kustaarabika ndio unawaondolea kikwazo kwa sharti la kuingia state kwa ndege za abiria sio private jets
 
Kama ni kweli basi tutarajie vifo vitakavyo tokana na slim & juliana vitaongezeka, maana hakuna familia ambayo haijaguswa na HIV
 
Kama MUNGU yupo na anataka watu wake waishi mlango mwingine utafunguliwa,

Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu amfanyaye kuwa kinga yake.

MUNGU wetu ni mwaminifu na warehema sana .
 
Tena Trump akazie ili watu wajiheshimu.!!

Cc; mzabzab Balqior mmeona sasa endeleeni kutafuna mipira iliyokufa na kina maafisa utamu..!! 😹
Mm sina HIV coz naiogopa mno, kwahiyo mara nyingi natumia Kinga, na miaka yangu 31, sijui ladha ya papuchi ya mwanamke bila condom ikoje Lamomy
 
Back
Top Bottom