SI KWELI Bei elekezi ya ARV ni Tsh. 76,000 baada ya USAID kusitisha misaada

SI KWELI Bei elekezi ya ARV ni Tsh. 76,000 baada ya USAID kusitisha misaada

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu

Nimeona taarifa inayoeleza kuwa bei elekezi ya ARVs ni shilingi elfu sabini na sita kwa mujibu wa wizara ya afya. je, ni kweli?

1738735399575.jpeg
View attachment 3225724
JAMII CHECK_ITV_SIKWELI.jpg
 
Tunachokijua
ARV inasimama kwa niaba ya antriretroviral hizi ni dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (Upungufu wa Kinga Mwilini) kwa waathirika. Dawa hizi zimekuwa zikitolewa kwa waathirika wa ugongwa kulingana na amelekezo ya wataalamu wa afya.

Taaarifa iliyotolewa na waziri wa afya kwa wakati huo (2023) ilieleza kuwa Kiwango cha Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) na wanatumia dawa za Kufubaza VVU (ARV) ni asilimia 97.9 kulinganisha na asilimia 93.6 mwaka 2016/17. Aidha, kiwango cha wanaotumia dawa na wamefubaza VVU ni asilimia 94.3 mwaka 2022/23 kulinganisha na asilimia 87 mwaka 2016/17.

Waziri alieleza pia kuwa anashakuru mashirika ya kimataifa kwa kuunga mkono juhudi hizo za kupambana na UKIMWI likiwemo shirika la USAID. USAID ni shirika la Marekani kwa ajili ya maendeleo ya kimataifa, shirika hili linakadiriwa kuwa na budget ya dola Billion 40 za Kimarekani sawa na Shilingi zaidi ya Trilioni 100 za Kitanzania (101,151,160,000,000 Tsh).

Baada ya utawala mpya wa Donald Trump kuanza kazi January, 2025 nchini Marekani kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika nyanya mbalimbali ikiwemo kusitishwa kwa muda huduma za USAID, jambo ambalo limekuwa na athari kubwa ikiwemo kwenye kada ya afya kwani walikuwa awafadhili pia wa dawa za kufubaza makali ya UKIMWI.

Madai

Kupitia mtandao wa Facebook mtu mmoja alichapisha taarifa akieleza kuwa Wizara ya Afya Tanzania imetoa na kutangaza bei ya dawa za ARV baada ya USAID kusitisha huduma zake;

“WIZARA YA AFYA TANZANIA IMETOA NA KUTANGAZA BEI YA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA VIRUSI VYA UKIMWI (ARV) KUWA NI SHILINGI ELFU SABINI NA SITA IMETOLEA UFAFANUZI KUWA DAWA IZO AWALI ZILITOLEWA BURE NA WAISANI AMBAO NI (US AIDS) AMBAO KWASASA WAMEJIONDOA RASIMI IVYO DAWA IZO KWA SASA ZINAZALISHWA LAKINI ZITAUZWA NA KUTOLEWA USHURU KAMA BIDHAA NYINGINE KUTOKANA NA KUSHUKA NA KUPANDA KWA THAMANI YA DOLA YA MAREKANI”

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia Taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli na ina lengo la kupotosha Umma. Ufuatiliaji umebaini kuwa grafiki iliyotumika imehaririwa na siyo halisi kutoka kwa Millard ayo updates aidha ITV live Tanzania inayoonekana siyo ukurasa rasmi wa ITV Tanzania.

Aidha JamiiCheck imebaini mapungufu katika uandishi wa taarifa hiyo mathalani neno izo badala ya hizo, ivyo badala ya hivyo, waisani badala ya wahisani, US AIDS badala ya USAID, matumizi ya herufi kubwa tupu.

Vilevile kiungo (link) iliyoambatanishwa na Taarifa hiyo inaelekeza kwenye kundi la ITV YETU. NA MATUKIO la Facebook, ilhali kituo cha ITV Tanzania kinatumia ukurasa (Page) na siyo kundi (Facebook group) na ukurasa rasmi wa ITV ni ITV Tanzania.

Wizara ya Afya kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii walikanusha kuhusu taarifa hiyo. Tazama hapa

Februari 8, 2025, Wizara ya Afya ilitoa taarifa kueleza kuwa inawahakikishia wananchi kuwa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI haizuzwi na zipo za kutosha. Tazama hapa
Kwa sasa wanaotumia ARV kwa Tanzania ni 1.6 Million.
Kwa sasa inadaiwa bei za ARV ni Tsh. 300,000 kwa mwezi (Full doze). Wizara yetu ya AFya ni Tsh. Trilioni 1.3. Kwa ujumla hii kitu hatuwezi ila kama tukiamua serikali ikaanza kununua magari yaliyogunduliwa na Kipanya basi tutaweza.
 
Kwa sasa wanaotumia ARV kwa Tanzania ni 1.6 Million.
Kwa sasa inadaiwa bei za ARV ni Tshs 300,000 kwa mwezi (Full doze). Wizara yetu ya AFya ni Tsh. Trilioni 1.3. Kwa ujumla hii kitu hatuwezi ila kama tukiamua serikali ikaanza kununua magari yaliyogunduliwa na Kipanya basi tutaweza.
1.3trion inakusanywa na Tra ndani ya mwezi moja tu, vipaumbele vyetu sio afya ya raia, pia hatuna planners kiwanda cha kutengenexa ARV akiwezi kumaliza 10bn shilling na dawa zitakua bei nafuu kama bei ya panadol.
 
Kwa sasa wanaotumia ARV kwa Tanzania ni 1.6 Million.
Kwa sasa inadaiwa bei za ARV ni Tsh. 300,000 kwa mwezi (Full doze). Wizara yetu ya AFya ni Tsh. Trilioni 1.3. Kwa ujumla hii kitu hatuwezi ila kama tukiamua serikali ikaanza kununua magari yaliyogunduliwa na Kipanya basi tutaweza.
Kama una shamba andika tu URITHI wasismbuke pa kuzikia
 
Unapiga kavu ukitegemea msaada wa marekani kumbe marekani yenyewe ilishapita humohumo ili kupunguza watu... Misheni yao imekamilika sababu walileta kama msaada ili watu wawe wazembe wa ngono alafu wakishakua wengi wanakata msaada ghafla.
Miaka miwili hadi mitatu mbele kutakua na janga kwa yale mataifa yaliyokuwa yanafurahia kutembeza bakuli wakati wamarekani wapo kijeshi zaidi.... Naam, hili ni jambo baya lakini ni zuri kuliko ubaya wenyewe
Hawakuleta msaada ili watu wawe wazembe, ounguza consipiracy theory.
Before msaada wao hali ilikuwa mbaya saba kuliko.
Na USAID ilitengenezwa makusudi maana ugonjwa ulianza kuingia nchini mwao, idea was kuustop ugonjwa ukiwa huko huko kabla haujafika nchini mwao

Haya masuala sijui ya kupunguza watu, wangetaka wangeacha kuleta dawa na mngepungua vile vile
 
Hawakuleta msaada ili watu wawe wazembe, ounguza consipiracy theory.
Before msaada wao hali ilikuwa mbaya saba kuliko.
Na USAID ilitengenezwa makusudi maana ugonjwa ulianza kuingia nchini mwao, idea was kuustop ugonjwa ukiwa huko huko kabla haujafika nchini mwao

Haya masuala sijui ya kupunguza watu, wangetaka wangeacha kuleta dawa na mngepungua vile vile
Kwamba walivyoleta hizo dawa huko kwao ulikua haujafika?
 
Inawezekana kwa sababu dingi yangu mdogo alikamatwa kwa kosa la kuiba arv na kuuza mtaani kwa wafugaji walimpigia bei ya 1500 kwa kidonge😀😀 kesi ilikua ya moto kweli kweli
 
Kwamba walivyoleta hizo dawa huko kwao ulikua haujafika?
Ulikuwa umeshafika but haukuwa threat kama afrika , Wao wameanza kutumia 1987, succesful waka contain maambukizi. Wakati africa hakukuwepo na dawa aina hiyo. due to migration za waafrika kwenda america waliona ni bora waka u contain nje kabla haujafika kwao ( wakiamini utakuwa ngumu kuuzuia)
Na wamefanikiwa

Wakat tz arv zimeanzq kutumia early 2000s, before the hali ilikuwa mbaya
 
Inawezekana kwa sababu dingi yangu mdogo alikamatwa kwa kosa la kuiba arv na kuuza mtaani kwa wafugaji walimpigia bei ya 1500 kwa kidonge😀😀 kesi ilikua ya moto kweli kweli
Aisee pole sana. Kesi iliishaje? Maana kwenye hayo mambo serikali dont play games kabisa
 
Back
Top Bottom