Bei mbovu kuwahi kutokea ya zao la mpunga yadumu misimu miwili Tanzania

Mauzo ya mchele yataendelea kushuka mwaka huu mchele mwingi bado upo wa msimu wa mwaka jana na mwaka huu pia wanatarajia kuvuna mchele mwingi
 
Tunauza bei ya juu 45k gunia hakuna shida
 
Oooh mie mwaka huu ndio naanza kuweka ghalani.

[emoji38] kupanga ni kuchagua
 
So ndio vizuri.[emoji34][emoji34][emoji34].
Sisi wapenda mchele tupate mteremko
 
Kwanza ujue kwamba mpunga hautapanda ila utazidi kushuka bei....

1. Stock ya msimu ulopita imejaa maghalani na mavuno yameanza

2. Wanunuzi kutoka nje hawapo na soko la ndani limeshiba.

3. Kuongezeka kwa wakulima wanaozalisha mpunga. 50% ya wakulima wa pamba kwa sasa wanalima mpunga

4. Kuongezeka kwa maeneo ya uzalishaji kahama, geita, mara,moro, tabora, rukwa, katavi, bukoba kwa sasa wanajitegemea na wanaitafuta mbea kwa kasi kwenye kilimo hiki

Kwetu sisi tunategemea by mwezi wa nne kilo itakua kat ya 700-900
 
Mlichekelea kwa wafanyakazi na wafanyabiashara.zamu yenu kuisoma namba.
 
My babe tena kwenye siasa si unakumbuka wajumbe walichokua wanakifanya ? mwendo wa kukata tu yaani ungepata kura 2 usingeamini 😀😀bora kwenye mpunga ni kama nimetunza kipesa changu kile kile hakijaongezeka tu. Ila siasa mmh
 
Mambo ya kutunza nafaka gharani, kutegemea bei ipande, ni biashara za kizamani sana!!!
Aisee nimejifunza sasa, ila kama mambo yangeenda vizuri bei huwa inapanda faida yake ni hadi nusu ya bei uliyonunulia and for me niliamua kununua kama sehemu ya kusave pesa yangu pia maana nisingenunua ningekua nishaitumia hiyo pesa kwa vitu vingine ila safari hii🙌
 
Bora bei iendelee kushuka wengine makwetu pakipikwa ubwabwa hakuna anayetoka yaani ni anasa.
 
Ukilima eneo kubwa inarudisha mtaji na faida kiasi
Sijaelewe mantiki ya faida kiasi.Kwa sababu kuna tabia ya watu kufanya ulanguzi kwa kuweka mazao na kujenga uhaba ili tu wapate super profits.Hata hivyo kama inarudisha gharama na faida ambayo ni fairly reasonabl sioni tatioz ila kama inafanya kilimo kiendelee kuwa utumwa basi nafikiri serikali inabidi itafuta namna ya kutatua hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…