Mwanzoni tutashangaa, lakini baadaye tutazoea; na wataalam mbalimbali watazidi kuingia kwenye tafiti ili kupunguza matumizi ya mafuta kwenye mitambo mbalimbali. Matatizo na shida, huamsha akili ya mwanadamu.
Mwaka 1961 bei ya petrol USA ilikuwa $0.29 per gallon, yaani $0.08 per litre au shilingi 200 kwa litre. Mwaka 2025 litre hiyo hiyo ya mafuta ilikuwa $0.82 per litre yaani shilingi 2,050 kwa lita. Hii ni zaidi ya mara 10 kwa absolute numbers. Lakini maisha yameendelea.
Mafuta yanaweza kupanda hata yakafika shilingi 10,000 kwa litre, itaumiza lakini maisha yataendelea. Ongezeko la ghafla litatutesa, kila kitu kitapanda, lakini maisha yataendelea.