mbotoro kivoi
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 2,018
- 3,009
🚛🚛🚛
Haya maneno ni kama unajiambia wewe na nafsi yako ili kujifariji mkuu. Kwani ni nani aliyesema kuwa dunia itafika mwisho; kwamba maisha hayataendelea??Mwanzoni tutashangaa, lakini baadaye tutazoea; na wataalam mbalimbali watazidi kuingia kwenye tafiti ili kupunguza matumizi ya mafuta kwenye mitambo mbalimbali. Matatizo na shida, huamsha akili ya mwanadamu.
Mwaka 1961 bei ya petrol USA ilikuwa $0.29 per gallon, yaani $0.08 per litre au shilingi 200 kwa litre. Mwaka 2025 litre hiyo hiyo ya mafuta ilikuwa $0.82 per litre yaani shilingi 2,050 kwa lita. Hii ni zaidi ya mara 10 kwa absolute numbers. Lakini maisha yameendelea.
Mafuta yanaweza kupanda hata yakafika shilingi 10,000 kwa litre, itaumiza lakini maisha yataendelea. Ongezeko la ghafla litatutesa, kila kitu kitapanda, lakini maisha yataendelea.
Wamiliki wa daladala wameingia mkenge kwenye hiliDaladala juzi wameingezewa 100 leo mafuta yamepanda kwa 300
Nchi ingekuwa inajielewa ingekuja na "mkakati kabambe" wa kuelekea EVs
Majamaa wamepigwa K.O moja matata sana. Siku nyingine watakuwa na akili timamu.Daladala juzi wameingezewa 100 leo mafuta yamepanda kwa 300
Ikiwa hivi itabidi mishahara ipande. Huwezi mwambia mtu aje kazini unamlipa 300,000 kwa mwezi halafu nusu ya mshahara ni gharama za usafiri.Jamaa hawawazi kuweka ruzuku ili mafuta yabaki kwenye bei fulani kwa muda maana wakifika 6000 kurudi chini ni ngumu bei itakua elekezi ni hiyo hiyo hata Iran mafuta yakiuzwa Tsh 1300 kwa lita hapo baada ya vita kuisha..
Hio tzs 100 kwenye daladala inagawanywa/kuzidishwa kwa abiria 30+Daladala juzi wameingezewa 100 leo mafuta yamepanda kwa 300