Bei ya Bati imepanda mnooo! Punguzeni bei

rantheb

Member
Joined
Jun 27, 2018
Posts
86
Reaction score
45
Wanajamvi inakuwaje Bei ya Bati iko juu mnoo kuliko hata mlima Kilimanjaro? Maana pesa ni ngumu kuipata na ukiipata bei za bidhaa mbalimbali za Ujenzi ikiwemo bati zinakuwa juu mnooo!

Tatizo ni nini? Waziri anayeshughulikia biashara na waziri wa viwanda hili hamlioni????

Punguzeni bei za bati basi.
 
Hakuna siku vifaa vya ujenzi viliuzwa bei yenye kuridhisha mnunuzi/mhitaji.
 
Shida ni kodi wanazotozwa....

Huku kwenye transactions ndio shidaa...

Kutoa pesa chini ya elfu kumi makato sh 900 nimeshangaa sana kwa kweli tulipofikia ni hatari tutakuwa kwa stress
 
Ulipo bati bei gani?nilipo bati la kawaida geji 30 @22000.
 
Mbona awamu hii zimeshuka sana acha uchochezi. BATI zinanulika vizuri tu sema wewe ulizoea mteremko
 
Tulieni hii ni Tanzania ya Vi-wonder
 
Vifaa vya ujenzi ni ghali sana serikali inapaswa kuingilia kati mtanzania wa kawaida kujenga makazi bora inaweza kuwa ngumu tofauti na miaka ya nyuma kidogo
 
BEI YA BANDO 1 SIMBA DUMU NI TSH.330,000/
GSM WANA 315,000/
LAKINI NEEMA KUBWA NI KWMBA KUNA BATI ZA MGANDA(UGANDA)
Zinauzwa 250,000/ zote hizo ni GAUGE 30
Sasa zitoke Uganda Hadi bongo bado zinauzwa 250k je palepale Uganda itakuwa bei gani?
Zanzibar sukari kilo 1500 ukivuka maji kuja dar 2700 tutanakwama wapi?
 
Vifaa vya ujenzi ni ghali sana serikali inapaswa kuingilia kati mtanzania wa kawaida kujenga makazi bora inaweza kuwa ngumu tofauti na miaka ya nyuma kidogo
Umeona eeenhee! Hii nchi yetu sote ni lazima viongozi wetu walitazame hili......suala la vifaa vya Ujenzi kuwa juu wanasababisha watu kutokujenga.....na waliojenga nao wanaweka kodi juuu kama mlima Kilimanjaro!
 
Ni kweli mkuu,miaka kama 3,4 nyuma bei ya bati za kawaida za futi 10 geji 30 ilikuwa sawa na bei ya simenti,sasa hv simenti ipo chini,bati juu sana,mfano huku kwangu Moro mjini,sinent ni tsh.elf 13 na bati ni tsh.elf 17,tofauti ya elf4 ni kubwa sana kiuchumi
 
Halafu ukishajenga Lukuvi anataka akupangie kiwango cha kodi kwa wapangaji wako na tena pango lilipwe kwa mwezi WTF Kanda ya titi bei ndo balaa
 
BEI YA BANDO 1 SIMBA DUMU NI TSH.330,000/
GSM WANA 315,000/
LAKINI NEEMA KUBWA NI KWMBA KUNA BATI ZA MGANDA(UGANDA)
Zinauzwa 250,000/ zote hizo ni GAUGE 30
Na hizo gauge 30 ndio wanazolia nazo hao wazee wa viwango wanasema hazina ubora, zitolewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…