stakehigh
JF-Expert Member
- Aug 9, 2019
- 40,702
- 41,213
Kwa wale ndugu zetu wa trading, hasa wa DSE na MT4/5, ulishawahi kujiuliza bei ya hizo securities zinapatikana vipi?
>Bitcoin ni nini? Kuna majibu 2
Kwa lugha nyepesi, ni mfumo wa cryptography unaobeba data zinazoitwa Bitcoin.
>Bitcoin yenyewe halisi ni nini?
Unapokuwa unamiliki Bitcoin, basi unakuwa unamiliki kafile kadogo ambacho kina taarifa zinazohusiana na transactions zako katika mfumo mzima!
Chukulia mfano wa akaunti ya benki inavyorekodi taarifa zako kuanzia salio mpaka miamala unayofanya, ila tofauti yake ni kwamba badala ya hii miamala kuongozwa na benki, huku miamala inaongozwa na mfumo mzima wa cryptography unaohusiana na Bitcoin.
Mfumo huu unaweza kuudownload na kuona taarifa za miamala yote inayofanyika na salio za kila mtu bila kuficha. Tofauti yake ni kwamba huku hatuna akaunti zenye majina ya watu bali tuna address za akaunti.
Hisa ni nini?
Hisa ni cheti (asset) kinachokutambulisha kama mmiliki wa biashara fulani kwa asilimia zako. Mfano, hisa moja ya CRDB inauzwa 790/=, basi ukinunua hisa 1 utakuwa unamiliki CRDB ila kwa nguvu ya hisa.
Hata hivyo, umiliki halisi wa CRDB unakuwa wa asilimia. Kupata hii asilimia, basi itabidi ujue CRDB walifloat hisa ngapi kwa ujumla, halafu ugawanye kwa ulichonunua. Pia ikumbukwe mara nyingi hisa hutolewa kwa ajili ya kukuza mtaji wa kampuni na si kwa ajili ya wewe kuwa bosi wa benki.
Hivyo basi, CRDB wanaweza wakawa wameuza asilimia 49% ya kampuni kwa wanahisa, hivyo bado hawana sauti kamili kwenye biashara nzima.
>Tofauti ya CRDB (hisa) na Bitcoin ni nini?
Tofauti yake ni kwamba Bitcoin unamiliki imani, ila CRDB unamiliki biashara. Biashara ya benki ikifa, basi na hisa zako (mostly) lazima zife pia. Same way, biashara ikifanya vizuri, basi na wewe hisa zako zitafanya vizuri — but si LAZIMA. Kampuni inaweza kufanya vizuri sana na hisa zikafail. Nitaelezea mbele.
> Kwanini umesema Bitcoin ni imani?
Kwa sababu kiuhalisia, Bitcoin ni pyramid scheme iliojificha. Ili bei ya Bitcoin ipande, watu wanatakiwa kuipigia kampeni sana kila sehemu. Sometimes watakutisha, "Umechelewa, zamani ilikuwa $3, sasa hivi ungekua billionaire."
Na ni kweli wanayo point katika hayo maneno kwa sababu lengo la Bitcoin ni kutafuta yule "mjinga wa mwisho" kistaarabu. Namaanisha yule ambaye atakuja atanunua Bitcoin halafu wengine wafaidike.
> Wanafaidika vipi?
Hapa sasa ndiyo mlinganisho wa Hisa na Bitcoin unafuatana. Katika masoko yote ya mtandaoni huwa tunauza kwa wanaotaka kununua.
Kwa mfano, ukiwa na laki yako unataka kununua hisa za CRDB, ni lazima awepo mtu anayetaka kuuza hisa za CRDB katika soko la hisa ama benki yenyewe ndipo biashara ifanyike. Lazima awepo mtu naye anataka kuuza hisa zake ili upewe wewe — yeye apate hiyo laki yako. Hivi ndivyo biashara zote za masoko ya mtandaoni zinavyofanyika.
Hata hivyo, kuna tofauti kidogo:
> Tofauti katika manunuzi
Masoko ya online yana tofauti pia. Makubwa yanayojulikana ni: SPOT pamoja na FUTURES
SPOT:
Ni uuzaji na ununuaji wa hapo hapo, same as unavyonunua kitu Kariakoo — unampa cash, anakupa bidhaa (nguo, simu, etc.)
FUTURES:
Aina ya ununuzi na uuzaji unaofanyika na broker ama exchange. Yeye ndiye ananunua au kuuza muda wowote unaotaka. Hata hivyo, wewe unanunua kwa cash ila yeye anakuuzia CONTRACT (kwa Kiswahili mnaita MKEKA).
Kwa kuwa anakuuzia kitu ambacho hakipo, basi ana uwezo wa kuongeza ama kupunguza ukubwa wa mkeka anavyotaka. Mfano, unaweza kuwa na $10 ila akakuongezea balance ikafika mpaka $100k — kutoka dola kumi mpaka milioni 200.
Kwa masharti nafuu: hakuna withdrawal mpaka ufunge biashara!
Kwa lugha nyepesi, iko hivi: umeweka mkeka wako kama betting, anakwambia “timu zikishinda utapewa mil 500,” ila sheria ni mpaka mechi ziishe.
Hapa ndiyo tunapojaribu kuwaambia kila siku watu wa forex kuhusu betting, ni kwa sababu hawaelewi nini kinafanyika nyuma ya pazia.
> Unaweza kudhani mbona ni kitu kizuri kuongezea mtaji?
Uko sahihi kabisa, kwa sababu ukiweza kufuga trade upande uliobashiri vizuri basi utapata faida kubwa sana. Mfano, milioni 200 kwa trade moja, ina maana faida yako ni kuanzia milioni 200 kwenda juu kwa only small market movements.
Hata hivyo, this turns out to be the worst idea you can have. Sheria ya kupata hii pesa kitaalamu inaitwa LEVERAGE, kwamba unapewa kikomo cha kukaa na hiyo salio. Sheria zake zipo hivi:
Tunakupa milioni 200 lakini bei ikishuka kidogo tu — tunachukua $10 yako.
Mahesabu yake yapo hivi…
kwa msiopenda hesabu kifupi ni kwamba, ukipewa LEVERAGE kubwa basi price ikienda chini kidogo wanachukua mtaji wako, ukipewa kidogo basi price itabidi iende chini sana kabla hawajakukaba! same way bei inabidi iende juu sana uweze kupata faida nzuri kwa sababu utalipa (FEES + INTEREST ya leverage) kwa lugha nyepesi tuiite mkopo:
ITAENDELEA..
>Bitcoin ni nini? Kuna majibu 2
- Bitcoin ni aina mpya ya pesa inayotumia cryptography kama njia ya usalama wakati wa kuthibitisha miamala. Pia, wengine wanaweza kusema ni asset inayopanda ama kushuka thamani wakati wote.
- Maana halisi ya Bitcoin:
Bitcoin ni aina ya mfumo wa cryptography unaojitegemea kwa ajili ya kubeba documents zinazohusiana na Bitcoin.
Kwa lugha nyepesi, ni mfumo wa cryptography unaobeba data zinazoitwa Bitcoin.
>Bitcoin yenyewe halisi ni nini?
Unapokuwa unamiliki Bitcoin, basi unakuwa unamiliki kafile kadogo ambacho kina taarifa zinazohusiana na transactions zako katika mfumo mzima!
Chukulia mfano wa akaunti ya benki inavyorekodi taarifa zako kuanzia salio mpaka miamala unayofanya, ila tofauti yake ni kwamba badala ya hii miamala kuongozwa na benki, huku miamala inaongozwa na mfumo mzima wa cryptography unaohusiana na Bitcoin.
Mfumo huu unaweza kuudownload na kuona taarifa za miamala yote inayofanyika na salio za kila mtu bila kuficha. Tofauti yake ni kwamba huku hatuna akaunti zenye majina ya watu bali tuna address za akaunti.
Address za akaunti ni sawa sawa na akaunti namba, ila tofauti ni kwamba benki ukiwa na akaunti namba unaweza kujua taarifa za mwenye akaunti. Ila huku, address (akaunti namba) ndiyo taarifa pekee unayoweza kuiona — hakuna cha zaidi.