Wakuu nataka kununua godoro bora, na sio la kuumiza mgongo, katika kutafuta taarifa humu nikagundua Magodoro ya Tanfomu na QFL magodoro Dodoma ndo the best,
Kama kawaida nikaingia mtaani kusaka godoro la inch 8, 5×6..
Kwa kampuni zote mbili, Wengine wanauza 260000, wengine wanauza 300000, nilipomuuliza anayeuza 300000 kuwa kwa nn wengine wanauza 260000 na yeye kangangania piga ua mwisho 300000, akadai hayo ya 260k ni fake,
Naomba msaada kwa waliowah kununua haya magodoro upande wa bei, je bei ya 300k kwa inch 8 , 5×6 ndo bei yenyewe au miyeyusho,
Natanguliza shukrani