Bei ya Mafuta Imepandaje wakati Serikali ilisema kuna akiba hadi Julai 2026

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
images-3.jpeg

Waati Serikali ya Tanzania ikitaja vita vinavyoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran kuwa ndiyo chanzo cha ongezeko la bei za mafuta kuanzia Aprili 1, 2026, utata umegubika suala hilo kutokana na kauli za viongozi wa Serikali waliowahakikishia Watanzania kuwa kuna mafuta ya kutosha hadi Julai, 2026.

Bei hizo zimepanda kwa Zaidi ya Sh1,000 kwa lita, ambapo kwa Dar es Salaam petrol imepanda hadi kufikia Sh3,820, dizeni Sh3,806 na mafuta ya taa Sh3,684 kwa lita, huku bei ya juu ikiwa Mkoa wa Kagera (Bukoba) abako petrol ikiuzwa kwa Sh4,070 dizeli Sh4,056 na mafuta Sh3,935 kwa lita.

Bei hiyo imepanda kutoka Sh2,864 kwa lita kwa Mkoa wa Dar es salaam kwa Machi 4 ,2026.

Taarifa iliyotolewa Aprili 1, 2026 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA, Dk James A. Mwainyekule imesema mabadiliko ya bei za mafuta nchini kwa mwezi Aprili 2026 yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mzozo unaoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, ulioanza Februari 28, 2026.

“Mashambulizi kwenye visima vya mafuta, vituo vya kuhifadhia mafuta, na mitambo ya kusafishia mafuta, pamoja na hatua ya Iran kufunga Mlango wa Bahari wa Hormuz (Strait of Hormuz) unaopitisha takriban asilimia 20 ya mafuta yote yanayosafirishwa duniani, yameathiri uzalishaji wa mafuta katika Mashariki ya Kati—ambapo Tanzania hupata sehemu kubwa ya bidhaa zake za mafuta,” amesema.

Alisema ongezeko la bei za mafuta ni tatizo la kimataifa, na Tanzania ikiwa sehemu ya mfumo huo, inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini unaendelea kuwa salama, huku ikijitahidi kudumisha bei nafuu ili kupunguza athari za kiuchumi na kijamii,” amesema.

Utata

Hata hivyo, Machi 23, 2026, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dk James Mataragio, aliwahakikishia Watanzania kuwa Nchi ya Tanzania ina akiba ya kutosha ya mafuta hadi Julai 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mbele ya Waziri wa Nishati, Deo Ndejembi, Mataragio alisema Serikali ilichukua hatua za mapema kwa kushirikiana na Taasisi zake, ili kuhakikisha kunakuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta na kwa gharama himilivu.

Naye Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi alisisitiza kuwa Nchi ina usalama mkubwa wa mafuta na kwamba Serikali imejipanga vizuri kuhakikisha Wananchi katika maeneo yote wanapata huduma bila vikwazo hivyo EWURA anapaswa kuhakikisha hakuna mafuta yanayofichwa katika maghala ya kuhifadhi.

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo, Abdul Nondo amehoji mikakati ya Serikali ya kulinda hifadhi ya mafuta iliyopo.

“Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk James Mataragio, alitoa kauli ya faraja kwa kusema kuwa nchi ina akiba ya kutosha ya mafuta inayoweza kutosheleza mahitaji hadi mwezi Julai 2026.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dk James Mataragio, taarifa ya Serikali Mafuta yaliyopo nchini kwenye matenki, petrol tuna lita 95,256,342; mafuta ya petrol yaliyowasili nchini ni lita 1,466,337; mafuta yaliyopo njiani kwenye meli ni lita 138,737,332. Hivyo, jumla ya mafuta ya Petrol yatakayokuwepo ni lita 380,677,011, na yanatosha kwa matumizi ya siku 61.”

“Vipi tena leo baada ya siku saba uhimilivu wa bei hakuna? Kipi kimekwenda tofauti na mikakati tuliyokuwa nayo ya kudhibiti kupanda kwa bei? Mafuta yaliyopanda bei ni ambayo yameingizwa na Meli sasa au ni hayo ambayo ni akiba tuliyo nayo hadi Julai?” amehoji Nondo.

Amesema kutokana na ongezeko hilo gharama za maisha zitapanda kwa kasi sana,na waathirika ni Watanzania wengi wa kipato cha chini.

“Nauli zitapanda gharama za usafiri zitapanda, hivyo vyakula pia vitapanda bei (Mfumuko wa bei za bidhaa) sababu ya kupanda kwa gharama za usafiri,” amesema.

Amesshauri Serikali kuchukua hatua za haraka ikiwa pamoja na kuchangia gharama na mwananchi, kwa kila lita moja Serikali itoe angalau Tsh.300 kama ruzuku ili kupunguza makali ya bei.

“Serikali iondoe Kodi/tozo zenye Jumla ya Sh500 katika kila lita katika tozo za Serikali zinazotozwa kwenye bidhaa ya mafuta ili kupunguza ukali wa bei na hivyo kusaidia kupunguza kupaa kwa gharama za maisha na mfumuko wa bei za bidhaa.Jumla ya tozo na Kodi ambazo zipo kwenye mafuta ni zaidi ya tozo na kodi 19 zenye thamani ya Sh1,113 kwa kila lita,” amesema.

Kuhusu hatua za muda mrefu, Nondo ameitaka Serikali iboreshe na kujenga miondombinu mingi na mikubwa ya kuhifadhia mafuta mengi ili kusaidia kudhibiti kupanda kwa bei hasa katika kipindi kama hiki.

“Serikali iweke msisitizo mkubwa katika matumizi ya gesi, kwa kuongeza miondombinu,vituo vya kujaza na uwezeshaji kurahisisha utekelezaji. Kwa kuanzia magari yote ya serikali yawe na mfumo wa gesi,” amesema.

Ufafanuzi wa Serikali

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Nishati Maci 31, imefafanua utaratibu uagizaji wa mafuta wa pamoja (Bulk Petroleum System (BPS), unaoratibiwa na Petroleum Bulk Procurement Agency (PBPA).

“Mfumo huu wa “M+2” unamaanisha kuwa mafuta yanayoagizwa sasa hutumika miezi miwili ijayo, jambo linaloipa Tanzania akiba ya muda mfupi ya miezi miwili hadi mitatu,” imesema.

Ikieleza sababu ya bei za mafuta kupanda, taarifa hiyo imesema EWURA hupanga bei kwa kutumia mfumo wa M-1, unaotegemea gharama halisi za mafuta yaliyoagizwa mwezi uliotangulia.

“Kutokana na mchanganyiko wa mafuta yaliyonunuliwa kabla na baada ya kuanza kwa vita, bei za mwezi Aprili zinatarajiwa kupanda kwa kiwango fulani lakini si kwa kasi kubwa kutokana na “balance” ya bei za Februari na Machi.

“Kutokana na zabuni zilizofanyika Februari 2026 kabla ya kupanda kwa bei, nchi imehakikishiwa utulivu wa bei hadi angalau mwezi Mei 2026,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema zaidi ya asilimia 60 ya mafuta yanayoagizwa Tanzania yanatoka Mashariki ya Kati ambapo katika miezi sita iliyopita, mafuta mengi yalitoka United Arab Emirates (37%), India (40%), huku Saudi Arabia, Oman, Kuwait na Bahrain zikichangia kiasi kilichobaki.

Kutokana na hatari iliyopo, taarifa hiyo imesema kwa hatua ya dharura, Serikali imeielekeza Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) kuanza kuagiza mafuta kwa pamoja kwa wingi ili kupata bei nafuu na kuhakikisha upatikanaji wa uhakika.

“Hatua hiyo inalenga kudhibiti bei kuanzia Mei hadi Julai 2026, kipindi ambacho kinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa wa mafuta duniani.

“Imeelezwa kuwa bei ya mafuta imepanda kutoka wastani wa dola 50–60 kwa pipa mwezi Februari hadi kufikia takribani dola 114 kwa sasa, hali inayoongeza presha kwa nchi zinazoagiza mafuta,” imesema taarifa hiyo.

Bunge laiagiza Serikali kuitisha kikao cha dharura

Akitoa matangazo bungeni jijini Dodoma Aprili 1, Spika wa Bunge Mussa Zungu amemwagiza Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi kukutana na Kamati ya Bunge ya Nishati ili kujua mwenendo wa mafuta nchini.

Alitoa taarifa hiyo kufuatia hoja za baadhi ya wabunge waliotaka ufafanuzi kuhusu ongeeko la bei ya mafuta nchini.

“Kuanzia leo wakutane na Kamati ya Nishati kujua mwenendo wa mafuta nchini, gharama na uhakika wa mafuta kupatikana katika taifa kwa sababu bila mafuta tunawez akukwama katika mipango ya maendeleo nchini,” alisema.

Zambia yachukua hatua, yafuta VAT, Ushuru wa Biadhaa

Wakati Serikali ya Tanzania ikijivutavuta, Serikali ya Zambia imeidhinisha kuondolewa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) pamoja na kusimamishwa kwa ushuru wa bidhaa (Excise Duty) kwa uagizaji wa petroli na dizeli kwa kipindi cha miezi mitatu, kuanzia tarehe 1 Aprili 2026.

Hatua hii imekuja kufuatia kikao maalum cha Baraza la Mawaziri kilichoitishwa na Rais Hakainde Hichilema katika Ikulu, kwa lengo la kujadili masuala ya kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wa Zambia.

Waziri wa Habari na Vyombo vya Habari, Cornelius Mweetwa, amesema kuwa hatua hizo ni za muda mfupi kwa ajili ya kupunguza athari za kupanda kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la kimataifa kwa uchumi wa Zambia.
 
Wahuni Hawa Kwani Wangesemaje Sasa
Njia Ya Muongo Ni Fupi, Sasa Wana La Kusema Zaidi Aibu
Muongo Muongoze Mpaka Uongo Wake Uwe Hadharani

Tunataka Sasa Kuona Isiyokongwe Haivushi
 
Kuiamini serikali na mamaduro ni ujuha tu kama ujuha mwenginewe!
 
View attachment 3565659

😥😥
 
Back
Top Bottom