Bei ya Mafuta ya kupikia bado iko juu sana

Bei ya Mafuta ya kupikia bado iko juu sana

Hatutaki kusumbua wafanyabiashara wasije kufunga biashara.
#KaziIendelee
 
Singida bei zikoje, ni aina gani?
Kama ni ile alizeti yetu siipendagi kale kaharufu huwa kananikera.

Shida siyo alizeti issue ni machine

Kuna sehemu wanachuja na kuchemsha (vinu vipo hivyo)
Hayo yanakuwa kama yanaelekea kwenye weupe

Kuna Yale wanakamua tu hayachemshwi Ndo yenye harufu

Mara ya mwisho bei ilifika 3,500 per lita
 
Singida bei zikoje, ni aina gani?
Kama ni ile alizeti yetu siipendagi kale kaharufu huwa kananikera.
Weka kikombe ki1 cha maji mix na hayo mafuta yako bandika jikoni..yatapiga keleleee ukiona yametulia kimya jua yameiva..unaweza tupia na hiliki..husikii tena harufu..hakikisha yametulia ndo yale maji yanakua yamekakamiA
 
Shida siyo alizeti issue ni machine

Kuna sehemu wanachuja na kuchemsha (vinu vipo hivyo)
Hayo yanakuwa kama yanaelekea kwenye weupe

Kuna Yale wanakamua tu hayachemshwi Ndo yenye harufu

Mara ya mwisho bei ilifika 3,500 per lita
Oooh sawa, ahsante kuna jamaa anatokea Mwanza nitamuagiza, make hii bei ya sasa tunakoelekea ni kula michemsho chukuchuku
 
Nashauri profesa Mkenda na naibu waziri Bashe anzisheni soko la alizeti la kitaifa singida au dodoma na liweke Bei kila siku kama masoko ya madini ili watu wengi wahamasike kulima alizeti wakijua kuna maslahi , na ikiwezekana viwanda vya mafuta kama Mount meru nk wakopeshe mbegu , mbolea , dawa kwa wakulima wengi iwezekanavyo Kwani wakiwekeza bil 10 wakapata bil 50 au 100 kuna tatizo?

Namna Hii itasaidia kwa haraka kupunguza ile gapu ya lita laki 2 au 3 zinazoagizwa nje ya nchi na kupunguza dola, itasaidia kupata lita za ziada na ku export nje na kuleta dola na gdp kupanda .
 
Back
Top Bottom