Nashauri profesa Mkenda na naibu waziri Bashe anzisheni soko la alizeti la kitaifa singida au dodoma na liweke Bei kila siku kama masoko ya madini ili watu wengi wahamasike kulima alizeti wakijua kuna maslahi , na ikiwezekana viwanda vya mafuta kama Mount meru nk wakopeshe mbegu , mbolea , dawa kwa wakulima wengi iwezekanavyo Kwani wakiwekeza bil 10 wakapata bil 50 au 100 kuna tatizo?
Namna Hii itasaidia kwa haraka kupunguza ile gapu ya lita laki 2 au 3 zinazoagizwa nje ya nchi na kupunguza dola, itasaidia kupata lita za ziada na ku export nje na kuleta dola na gdp kupanda .