Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Watumiaji wa bidhaa za mafuta Tanzania wataendelea kuugulia maumivu ya ongezeko la bei baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kutangaza bei kikomo zitakazotumika Machi mwaka huu.
Katika bei hizo, watumiaji wa mafuta ya dizeli wameshuhudia ongezeko la bei zaidi ikilinganishwa na wale wa petroli na mafuta ya taa.
Kwa mujibu wa taarifa ya EWURA, ongezeko hili la bei litagusa mafuta yanayoingia kupitia bandari zote za Tanga, Dar es Salaam na Mtwara.
Kuanzia leo Machi 4, 2026, bei ya rejareja ya petroli jijini Dar es Salaam imeongezeka hadi Tsh. 2,864 kwa lita kutoka Tsh. 2,788 ya Februari, ikiwa ni ongezeko la Tsh. 76.
Dizeli imepanda kwa kasi zaidi ikiwa na ongezeko la Tsh. 157, ambapo itauzwa Sh2,858 kutoka Tsh. 2,701, huku mafuta ya taa yakiongezeka kwa Sh186 ambapo itauzwa Tsh. 2,932 kutoka Tsh. 2,746.
⛽️ Dar es Salaam
Petrol: Tsh. 2,864 kwa lita (ongezeko la Tsh. 76 kutoka Tsh. 2,788 Februari)
Dizeli: Tsh. 2,858 kwa lita (ongezeko la Tsh. 157 kutoka Tsh. 2,701)
Keroseni: Tsh. 2,932 kwa lita (ongezeko la Tsh. 186 kutoka Tsh. 2,746)
⛽️ Tanga
Petrol: Tsh. 2,925 kwa lita (ongezeko la Tsh. 76 kutoka Tsh. 2,849)
Dizeli: Tsh. 2,919 kwa lita (ongezeko la Tsh. 157 kutoka Tsh. 2,762)
Keroseni: Tsh. 2,993 kwa lita (ongezeko la Tsh. 186 kutoka Tsh. 2,807)
⛽️ Mtwara
Petrol: Tsh. 2,956 kwa lita (ongezeko la Tsh. 75 kutoka Tsh. 2,881)
Dizeli: Tsh. 2,951 kwa lita (ongezeko la Tsh. 157 kutoka Tsh. 2,794)
Keroseni: Tsh. 3,025 kwa lita (ongezeko la Tsh. 187 kutoka Tsh. 2,838)
EWURA imeeleza kuwa bei za rejeleo (FOB) katika soko la Ghuba la Kiarabu zimepanda kwa 6.2% kwa petrol, 9.8% kwa dizeli, na 7.4% kwa keroseni mwezi Machi, jambo lililosababisha ongezeko la gharama za kuagiza na kuathiri bei za pampu nchini.
Ongezeko hili lina athiri gharama za usafirishaji, biashara ndogo, na matumizi ya kila siku ya wananchi. Wataalamu wanashauri madereva kupanga matumizi yao ya mafuta ili kupunguza athari za kiuchumi.