Bei ya Mahindi 2024 itamnyanyua au itamnyanyasa Mkulima?

Mimi ni mwanachuo nimeamua kuanza kilimo ili baada ya kumaliza chuo niwe na mtaji wa kujiajiri. Nililima eka nne eka mbili zimefeli kutokana na changamoto za shambani na mtaji. Bado sijavuna maana nilichelewa kupanda. Bei ndio masikitiko. Ikipanda angalau 50 junia nipumue, angalau niiludishe mtaji msimu ujao nijipange upya
 
Okay mkuu naomba nikuulize, mfano umeitwa na kamati ya bunge useme bei halali, unapendekeza gunia la mahindi liuzwe kiasi gani? [emoji848]
 
Bei ya mahindi mwaka huu Iko chini....lakini hakuna kukata tamaa....hata mwakani tulime Tena.....bei inaweza kuwa nzuri
 
Mahindi sio biashara,ni chakula.
Kama kweli ni chakula pekee wakulima wakiamua kulima kwaajili ya chakula kwaajili yao tu watu watakufa njaa Tz hii, Mahindi ni chakula pia ni biashara
 
Hapo Hapo hujakutana na guguchawi la mahindi, haliskii dawa
 
Nimeshangaa kununua unga kilo 900, nikajiuliza ndugu zangu wakulima wanahali gani huko mashambani
 
Tatizo ni kutozingatia kanuni , kanuni inatakiwa create demand before supply Ili commodity iwe scarce ipelekee rise of price .hapo tutamaintain mambo unless otherwise we still struggling
 
Uko mbeya ndoo ya Lita 20 ni elfu 5000 hiyo gunia la debe 6 ni 30000 elfu
 
mahindi yashuke bei watanzania wajikite kwenye kutafuta mboga zaidi
 
Mkuu ngoja nikushauri kitu kidogo unaweza fata au ukaona inakuaje,, hapo usilime eka 4 lima eka 3 au 2 pekee kama haupo mwenyewe shambani eka hizo zinaweza kulinda mtaji na hela nyingine jiwekeze mdogo mdogo ila ukimaliza sasa ingia mwenyew field kapige kazi kweli kweli mkuu nina experience na hilo.
 
Haitazidi 80k kwa gunia la debe 6! Kila kona ya nchi kuna mahindi ya kutosha! Tuombe Rais afungue mipaka kwa wanunuzi wa nje!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…