Bei ya mahindi Handeni zinashangaza

Eddy ruta

Member
Joined
Sep 25, 2016
Posts
61
Reaction score
94
Wakuu nimeamini sisi wakulima wadogo wadogo hatutokaa tupate utajiri kupitia kilimo kamwe,

Nimeshangaa bei za mahindi kwa huku Handeni mpaka sahivi eti gunia ni 35000 ukizingatia mahindi ya mwaka yanaiva kwahiyo mpaka kufikia mwezi wa 6 mwishoni mpaka wa saba watu watakuwa wanavuna.

Sasa je kama sahv gunia ni bei hiyo inamana kufikia mavuno bei itashuka mpaka 25000 kwa 20000 gunia?

Wakulima tuna moyo sana MUNGU atusaidie tu
 
Hifazi mkuu,njaa Haina baunsa yakipanda hata laki watu tutanunua!
 
Mazao ya Kisiasa, Mazao yanayo limwa na kila mtu hapa Tanzania, Binafisi Mahindi hunilimishi. Au lima lishia mifugo yako na faida utaionea kwenye mifugo yake.
 
Mzilankende Wakati Wake Alisema Mkulima Auze Bei Anayoitaka Yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…