Bei ya mahindi nchini inasikitisha

Bei ya mahindi nchini inasikitisha

EJay

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Posts
693
Reaction score
172
Wakuu ni masikitiko makubwa kwa wajasiriamali wote waliohifadhi mahindi ghalani kwa kuwa mwaka huu hakuna bei kabisa na inaonekana kuna chakula cha kutosha pia katika mizunguko yangu katika mikoa mbalimbali nimeona mahindi yamestawi vizuri sana; sasa wadau kwa nini serikali isiruhusu wafanyabiashara kuuza nje? na kwenye mashirika kama WFP wakapeleke Somalia na CAR? kwa kweli inasikitisha kwani mipango ya wengi inakwama
 
Mkuu serikali imeruhusu mazao yauzwe nje na maeneo mengi bei za mahindi zimepanda
 
Kwa kweli mna changamoto sana mnaotumia WRS, serikali haijafanya tafiti za kutosha ama hao waendeshaji wa WRS hawajajua kufanya strategic marketing.
 
Kenya wanaanza kununua mahindi from tanzania on may, so waliohifadhi wanaweza kufanya biashara nzuri tu
 
Export ban ya chakula hususan mahindi imeshaondolewa na Wizara kama miaka miwili au mitatu iliyopita. Tatizo hakuna taarifa sahihi zinazofikia walengwa!!! Kenya wananunua sana mahindi ya Tanzania!!! Walishaongeza thamani wanarudisha katika supermarket zetu. Nakumatt na Uchumi sasa ndo zenyewe!!!
 
Ulienda kuuza mahindi yako wapi ukakataliwa kuyauza?
 
Kwani bei ya sasa ni kiasi gani, na wewe kwenye hesabu zako ili upate faida ingebidi iwe kiasi gani ?
 
Ulienda kuuza mahindi yako wapi ukakataliwa kuyauza?

tunataka bei ifike mpaka sh.700-800 kwa kilo then gunia iwe kati ya 70 to 80,000 tsh per gunia tofauti na sasa kg 400 wakati ulinunua sh.480 kwa kg
 
Kenya wanaanza kununua mahindi from tanzania on may, so waliohifadhi wanaweza kufanya biashara nzuri tu

maneno ya busara sana mkuu ngoja tusubiri mkuu
 
tunataka bei ifike mpaka sh.700-800 kwa kilo then gunia iwe kati ya 70 to 80,000 tsh per gunia tofauti na sasa kg 400 wakati ulinunua sh.480 kwa kg
duh kama ni hivyo basi huu sio wakati wa kuuza bali kununua
 
Fanya unga. Utalipa zaidi.
 
duh kama ni hivyo basi huu sio wakati wa kuuza bali kununua

yaani mkuu juzi nimetembea kucheki ya shambani yamestawi vizuri huku ya mwaka jana yamedoda stoo ni hatari sana mengine tulinunua kwa hela za mikopo
 
Tena hapo inabidi kununua dawa kwa haraka na kuhakikisha wadudu pia hawafanyi uharibifu wao.., jaribu kutafuta masoko sehemu ya mbali na ulipo, ulizia bei sehemu mbali mbali au weka tangazo humu pia kwa bei unayotaka kuwauzia watu kwa jumla (ila kuwa mwangalifu na matapeli). Ila kama umeweka dawa vizuri na kuna sehemu ya kuyaweka basi usiwe na haraka subiri mpaka msimu wa kuuza ufike
 
asante mkuu kwa ushauri
 
yaani mkuu juzi nimetembea kucheki ya shambani yamestawi vizuri huku ya mwaka jana yamedoda stoo ni hatari sana mengine tulinunua kwa hela za mikopo

Hizo ni neema msikasirike.

Toeni sadaka, mtapata barka zaidi.

Hamkupigia hesabu za Kilimo Kwanza? mlifikiri Kilimo Kwanza ni utani.
 
Baraka na neema ni kwa mkulima kupata masoko ya bidhaa zake pindi anapovuna kama kifutia jasho cha pesa na nguvu alizoweka (yeye kazi yake kwa kiasi kikubwa amemaliza) kwahio ni jukumu la serikali (ambayo inaamini kilimo ni uti wa mgongo na wakulima ndio moja ya nguvu kazi kubwa) kuhakikisha kwamba kuna miundo mbinu ya either huyu jamaa kufikisha mazao yake sokoni kwa urahisi, au kununua mazao ya huyu jamaa kwa bei nzuri sana (ili asikate tamaa) na kutafuta masoko nje ya nchi n.k. (ili jamii na nchi nzima ifaidike)
 
Mkulima unatakiwa ujuwe namna ya kuongeza thamani ya mazao yako, nimekwambia fanya unga, usitegemee kuuza mahindi makavu tu.

Kwa mahindi nnavyoyajuwa, hata ukiuza 400 kilo bado hauna hasara, labda wewe si mkulima ni mlanguzi.
 
Wewe unaongelea mkulima mmoja mmoja mimi naongelea wakulima kwa ujumla (kukosa wanunuzi wa kuaminika na wenye bei nzuri) sio makosa yao ni makosa ya wale wanaowahimiza kulima wakati hakuna miundombinu ya kutosha au kuwasaidia kutafuta masoko.., unaongelea kutengeneza unga.., kweli mkulima mwenye magunia na magunia huko kijijini unamwambia atengeneze unga.., huo muda na hizo gharama atazitekeleza vipi ? pia atengeneze unga upi sembe au ? huoni kwamba atakuwa amepoteza wale wanaotaka mahindi ili wale makande au wakoboe..? Cha muhimu kuwasaidia hawa ndugu zetu ni kuwapa elimu za kuanzisha vyama vyao vya ushirika (ili wapate bargain power na kuweza kuongeza value) au kama vipi wakiacha kulima mahindi na kuhamia kwenye mazao yanayoingiza faida kubwa kwa wakati huo (kama Kenya kilimo cha passions) watu msilalamike.
 
Back
Top Bottom