Wakuu ni masikitiko makubwa kwa wajasiriamali wote waliohifadhi mahindi ghalani kwa kuwa mwaka huu hakuna bei kabisa na inaonekana kuna chakula cha kutosha pia katika mizunguko yangu katika mikoa mbalimbali nimeona mahindi yamestawi vizuri sana; sasa wadau kwa nini serikali isiruhusu wafanyabiashara kuuza nje? na kwenye mashirika kama WFP wakapeleke Somalia na CAR? kwa kweli inasikitisha kwani mipango ya wengi inakwama