Msimu huu hakuna cha mahindi wala maharage, maharage mapya yameshuka mpaka Tsh 15,000/ kwa debe kule Lupembe wakati ambapo msimu huu mwaka jana ilikuwa 35,000/ bila chenga. Mahindi ndio hayo Tsh 3,500/ mpaka 4000/ ukibahatika.
Hao hao Wanalizombe waliotia nguvu kwenye Tangawizi maeneo ya Madaba, bei imeshuka mpaka Tsh 500/ toka Tsh 4,000/ ya 2015.Na wale waliojishaua kulima Mbaazi, nadhani kila mtu anajua. Na sisi tuliootesha miti ya mbao maeneo ya Madaba biashara imedoda mbaya, hata wale wakuuza miche wanatoa macho, hakuna wa kununua.