Pastory Kimaryo
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 967
- 668
Kwahiyo tuambie, ng'ombe unao wangapi na uliwanunua wapi, na unawatunzaje na maziwa unayauza kwenye diaries au kawaida kawaida in short soko limekaaje coz hapo ndo kwenye dhamira ya kufuga ng'ombe wa maziwa?Bei ya Ng’ombe wa Maziwa inategemea vitu vingi aina kuna Freshian, Jersey , Aryshire lakini pia Matunzo zipo aina katika hizo zinaweza kuhimiri mazingira yetu. Wapo Ng’ombe wana uwezo wa kutoa lita10,16,20,30 kwa siku inategemea matunzo na malisho yako. Bei ni kuanzia 1.5 milion na kuendelea kulingana na uwezo wa Ng’ombe, Mimba kama amepandishwa au anakamuliwa Ng’ombe wa lita 20-30 bei lazima iwe juu .Mimi ni graduate niliona fursa hyo hapo nyuma Nilitafuta sana Ng’ombe wa kufuga ad kuja kupata nilikutana na madalali na matapeli pia humu humu JF . Kuhusu soko la Maziwa inategemea na eneo ulipo mfano mimi Nipo DODOMA demand ya Maziwa ipo juu sana lita ni 2000 na ni kutafuta. NIKUSHAURI UWE NA USIMAMIZI MZURI KWENYE MALISHO USIWAACHIE VIJANA PEKEE.
Vizuri, we uko wapi sasa?Ng’ombe wa kisasa hatunyonyeshi unakamua unampa pembeni ndama kukamua ni endelevu non stop, Soko la Maziwa ni bill na reja reja (soko inategemea na ulipo wewe).Mimi nilinunua kwa mzee alihamishwa kikaz nilimpa ela kiasi akanipa Ng’ombe watano wengine nilinunua kwa mtu
Mi nafugia DODOMAVizuri, we uko wapi sasa?
Tupe uzoefu wa faida na hasara katika ufugaji wa ng'ombe wa maziwa, nipo KIBAHA mkoa wa Pwani, natamani kufuga ng'ombe wa maziwa.Mi nafugia DODOMA
Samahani n'gombe akiwa na mimba ndio unaanza kumkamua?Ng’ombe wa kisasa hatunyonyeshi unakamua unampa pembeni ndama kukamua ni endelevu non stop, Soko la Maziwa ni bill na reja reja (soko inategemea na ulipo wewe).Mimi nilinunua kwa mzee alihamishwa kikaz nilimpa ela kiasi akanipa Ng’ombe watano wengine nilinunua kwa mtu
Ng’ombe anapandishwa akishika mimba baada ya miez 9 atazaa unasubir kama week na Cku kadhaa Maziwa yakiwa saf unaanza kukamua hii inategemea na Rotation yakwenye Banda mfano mm nakamua baada ya muda nampandisha tena wakati naendelea kukamua ad mimba inapokua kubwa naacha wakati huo kuna Ng’ombe wengine wanazaa hii ni ku-maintain soko la Maziwa. Kuhusu malisho ni ww na aina ya chakula kuna vyakula vinaongeza utoaji wa maziwa ,pumba,na kama ni Ng’ombe wa Maziwa akishiba vizur lishe na madini uwez kukosa Maziwa yakutoshaSamahani n'gombe akiwa na mimba ndio unaanza kumkamua?
Na kukamua ukianza unaachwa akizaa au ni kukamua tu forever au kuna wakati hukamui ?
Na anakuwa anafaa kupandishia kila baada ya muda gani na ukimpandishia unasubiri muda gani ukamue ?
Na ndama akizaliwa inamchukua miaka au miezi mingapi afae kupandishia?
Na fact ya malisho na matunzo ikizingatiwa anaweza toa wastani lita ngapi per day kulingana na hizo AiNa au general?
Ng’ombe wanafaida nzuri tu na risk yake pia ni ndogo wengi wanatamani lakini mazingira hayaruhusu kama una nafasi tafuta ng’ombe.Tupe uzoefu wa faida na hasara katika ufugaji wa ng'ombe wa maziwa nipo KIBAHA mkoa wa pwani natamani kufuga ng'ombe wa maziwa.
Ni tumaini langu utatusaidia wengi kupata ufahamu bora wa faida ili tuwekeze nguvu huko kama ujuavyo hakuna ajira biashara ni ngumu ila kwenye kilimo na mifugo wengi wanadai ni nafuu tatizo ni elimu ya kutufanya tuvutiwe kuingia huko.
Asante
Nafasi ninayo nina mashamba heka 5 yanaweza kutosha kufanya ufugaji ng'ombe zaidi ya 10?Ng’ombe wanafaida nzuri tu na risk yake pia ni ndogo wengi wanatamani lakini mazingira hayaruhusu kama una nafasi tafuta ng’ombe.
Eneo ni kubwa maana nafasi ya Banda ni ndogo tu kwa Ng’ombe wa kisasa ni Zero - grazing labda sehemu ya kuhifadhi mbolea na Nyasi za akibaNafasi ninayo nina mashamba heka 5 yanaweza kutosha kufanya ufugaji ng'ombe zaidi ya 10?
Ok, labda sikuwa specific mimi nipo Morogoro sehemu inaitwa Lupiro mbele ya Ifakara karibu na Mahenge, by the way thanks for yo advice, kudos!uko morogoro still hujui pa kuwapata??
nenda sua wapo wengi, nenda solomoni mazimbu camps wako wengi Sana, nenda sangasanga Kuna ngombe wa maziwa kibao kule, nenda mzumbe wako weeeeengi utadhani Ranchi ya taifa.
kuhusu maziwa inategemea na malisho na utunzaji wake.
Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
Good advice, though kufuga nguruwe ni kitu nimefikiria kufanya pia.Bora ukafuga hata kitimoto endapo utakuwa mkiristo kuliko hao ngombe.(samahani)
usipowaogesha dawa na wao wakangatwa na kupe anayesababisha ugonjwa wa (ndagama) mwezi mmoja Ni mwingi Sana utaamka na mzoga.
wanahitaji matunzo ya Hali ya juu ili watoe faida unayoitaka wewe kinyume na hapo utakuwa umejiongezea majukumu yasiyo na msingi.
Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
Halafu, katika hili hili, naweza kutafuta eneo kama heka mbili hv nikapanda magugu kwaajili ya ng'ombe?Eneo ni kubwa maana nafasi ya Banda ni ndogo tu kwa Ng’ombe wa kisasa ni Zero - grazing labda sehemu ya kuhifadhi mbolea na Nyasi za akiba
aaah kumbe. sawa chief watu tumezoea MTU akisema Niko morogoro Ina maana Yuko hapa hapa mjini.Ok, labda sikuwa specific mimi nipo Morogoro sehemu inaitwa Lupiro mbele ya Ifakara karibu na Mahenge, by the way thanks for yo advice, kudos!
aaah kumbe. sawa chief watu tumezoea MTU akisema Niko morogoro Ina maana Yuko hapa hapa mjini.
huko mwingine tunaita morogoro vijijini au wilayani.
Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app