HOJA Bei ya Saruji inazidi kupanda kila siku, Serikali iingilie kati suala hili

HOJA Bei ya Saruji inazidi kupanda kila siku, Serikali iingilie kati suala hili

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

MeckClux

New Member
Joined
Dec 22, 2013
Posts
4
Reaction score
2
Nakumbuka mwezi Julai mwaka huu, kiongozi mmoja pamoja na mtumishi wa kiwanda maarufu cha saruji jijini Dar es Salaam walijitokeza kuzungumzia kupanda kwa bei ya saruji. Wakati huo, mzalishaji mkuu alidai kuwa hajapandisha bei na hakuwa na ufahamu kuhusu chanzo cha ongezeko hilo.

Soma: Twiga Cement: Bei zetu na za mawakala wetu hazijabalika ziko vilevile, Bei za wauzaji wa rejareja za kuanzia 21,000 kwa mfuko hata sisi tunazishangaa

Inasikitisha kuona kuwa wananchi wameendelea kupanda kwa bei ya saruji kila kukicha, kana kwamba wanachukuliwa kuwa hawana uelewa wa kinachoendelea. Hata kama ongezeko hilo linachangiwa na kupanda kwa bei ya mafuta au gharama nyingine za uzalishaji, bei ya saruji imekuwa kubwa na isiyomudu kwa wananchi wengi.

Ombi langu kwa Serikali ni kuingilia kati na kulifanyia kazi suala hili ili kuhakikisha saruji inapatikana kwa bei nafuu. Tuna vijana wengi wanaotamani kujenga makazi yao, hivyo ni muhimu kuweka mazingira yatakayowezesha upatikanaji wa vifaa vya ujenzi kwa bei rafiki, badala ya kuangalia maslahi ya upande mmoja pekee.
 
Similar discussion
105320.jpg
 
Back
Top Bottom