Bei ya suti za Sheria Ngowi

Bei ya suti za Sheria Ngowi

Jibu kashapewa huko zinaanzia $1700! Cif ya Verossa hio 🙂🙂🙂

CIF ya Verosa ni kwako wewe na mimi.

Kwa mwingine mwenye hela anaona hawezi kushuka kwenye Range Rover kavaa suti ya 70,000/=

Lazima tuelewe diversity za consumers, uwezo, tastes na vipaumbele. Mwingine anaona hawezi kununua suti ya $500 lakini ana iPhone ya $1,000 mfukoni, bei ya ardhi Mkuranga! Personal priorities.
 
Zina free WiFi haha by the way suti ya kushona haiwez kuwa sawa na ya dukan coz unashonewa unavotaka na customs made

Kuna a lot of generalizations here.

Inategemea fundi wa ubora gani amekushonea na imeshonwaje. Si lazima suti ya kushonesha iwe bora kuliko ya dukani just because umepimwa. Ingekuwa hivyo mafundi cherehani wote wangekuwa wote ma designer wa majina makubwa kuliko maduka.
 
Harafu kama ni mzuri wa kuchagua size zako unaweza toka bomba ile mbaya kuliko hizo za malaki matano na kuendelea!!

Halafu. Sio "harafu..."

Ukivaa suruali na shati limenyooka na unaongea Kiswahili kizuri mbele za watu unaweza kuonekana makini, maridadi na professional kuliko kuvaa suti kubwa unatema Kiswahili kama afande Tarime.

Hii ndio be ghari.?

Na wewe pia, wekeza kwenye kuongea lugha iliyonyooka kabla ya kutafuta suti AGHARI!
 
Mbuzi hula majani kutokana na urefu wa kamba. Wewe kama pesa zako ni kidogo nunua suti ya mtumba elfu kumi tu. Kama unazo kidogo shona kwa hao jamaa unaowapigia debe kwa laki moja hadi laki tano. Kwa walionazo waache washone suti za mamilioni. Mbona hata vyakula hatulingani ulaji. Kuna wanao kunywa chai na andazi au mkate mkavu. Kuna wanao kunywa chai namikate iliyopakwa jam na siagi. Napo wanao kunywa chai na vitafunwa vingi kama mkate uliopakwa jam na siagi, nyama ya kukaanga, mayai, matunda na juice. Kipato kitakufanyia daraja la mahitaji yako. Tusiharibu soko la biashara ya mtu kwa kumkashifu na kumsifia mwingine papo hapo. Huo sio ungwana
 
Yeap naagiza au nikienda nanunua. its cheap,suit nzuri GBP 100-150, unavizia SALE.
It's cheap kwa nani?

Mtu makini, muelewa, hasemi jumla jumla tu British pound 150 "its cheap." Kuna watu ambao hawana access au uwezo wa kwenda au kuagiza suti ya pound 150. Cheap ni kitu ambacho kiko chini ya ordinary market price, kama suti ya 70,000/=
 
Kwa ufupi kwa hela hiyo heri uvae suit za maana toka ulaya!!
Tunazipataje hizo suti za Ulaya?

Kuliko kununua ule uchafu kwa gharama zile ni heri ununue suit kali za ulaya tu ijulikane moja

Suit hazi balance kabisa!!
Tununue suti za Ulaya, tuko Ulaya hapa? Thread inahusu suti za Sheria Ngowi. Which means tunaongelea Tanzania. Ukisema duka liko Ulaya tuambie tunazipate au tunafikaje huko Ulaya?
 
mkuu Tindikali naona umeamua kuja kupitisha kifimbo cheza kwenye nyanja zote...endelea mkuu!
Ninao hawa leo.

Wana exposure ya kukaa kaa nje kujua majina ya maduka, wamesoma soma lakini wamejaa generalizations, hawajui kabisa kwao TZ kuna raia wa makundi gani ya vipato. Totally out of touch. Ngoja niwawahi kabla sijafungiwa.
 
Unawaambia tu kiuno 34, inakuja suruali na koti utafikiri walikupima!

Toka lini ukataja size ya kiuno tu halafu ukajulikana automatically una mabega size gani, mapaja, upana wa kifua, shingo, in-seam (urefu wa eneo la uume), urefu wa mikono, urefu wa blazer...nk?

Duka gani hilo au fundi gani huyo? Si ndio kamba hizo sasa tunazozikataa?
 
Sana aisee.... yaani wewe ni size tuuu kwisha kazi...

Mi huwa nawashauri watu kuliko kununua uchafu kwa bei kubwa heri waagize tu ulaya

Suti ya kuagiza Ulaya ambayo hujajipima, hujaiona kabla ya kununua nayo inaweza kuwa kituko kuliko suti ya kushonesha Mwenge. Hakuna hard and fast rule ya kununua au kushonesha suti.
 
Bei ya suti nnayovaa nikikutajia utaumia bure moyo....

Ila jua tu hizo suti za elf 70 ni china tuu na hazina quality kabisaaa.... but kwa wanaoanza maisha si mbaya!!

Ukitaja bei ya suti unayovaa sisi tutaumia kwani sisi tumekununulia? Acha ushamba. Anaeanza maisha anavaa nepi, ki-jumpsuit na kikofia kichwani, sio suti. Acha dharau.
 
Ya mtumba ni nzuri kwasabababu kwenye mtumba ndio unapata originals.

"Original" ambayo ni mtumba is not necessary bora zaidi. Inaweza kuwa imeanza kupauka pauka na kuwa frayed on the edges.

Hakuna formula inayosema suti ya mtumba au ya kupima au ya kununua dukani kwa bei fulani ndio bora zaidi.
 
Ninao hawa leo.

Wana exposure ya kukaa kaa nje na kujua majina ya maduka, na wamesoma soma lakini wamejaa generalizations, hawajui kabisa kwao Tanzania kuna raia wa makundi gani ya vipato. Totally out of touch. Ngoja niwawahi kabla sijafungiwa.


Angalia usitukane tu. au kumkashifu mtu (defamation) ni makosa ya jinai.
 
"Original" ambayo ni mtumba is not necessary bora zaidi. Inaweza kuwa imeanza kupauka pauka na kuwa frayed on the edges.

Hakuna formula inayosema suti ya mtumba au ya kupima au ya kununua dukani kwa bei fulani ndio bora zaidi.
Kazi ipo kwako kuhakikisha ina ubora. Au nimesema kwasababu ya mtumba unabeba tu?
 
Toka lini ukataja size ya kiuno tu halafu ukajulikana automatically una mabega size gani, mapaja, upana wa kifua, shingo, in-seam (urefu wa eneo la uume), urefu wa mikono....?

Duka gani hilo au fundi gani huyo? Si ndio kamba hizo sasa tunazozikataa?
Wewe sio mimi, mimi ndio ninavyofanya. Nishataja maduka huko juu sina sababu ya kurudia.
 
Its cheap kwa nani?

Mtu makini, muelewa, hasemi jumla jumla tu British pound 150 "its cheap." Kuna watu ambao hawana access au uwezo wa kwenda au kuagiza suti ya pound 150. Cheap ni kitu ambacho kiko chini ya ordinary market price, kama suti ya 70,000/=
Its cheap kulinganisha na za Sheria Ngowi zinazozungumziwa kwenye hii mada. Hivi nimekwambia mimi ni makini,mwelewa?
 
Back
Top Bottom