Bei ya Umeme yapanda. Naipongeza Serikali kwa kuliona hili bei ilikuwa ndogo sana

Bei ya Umeme yapanda. Naipongeza Serikali kwa kuliona hili bei ilikuwa ndogo sana

Status
Not open for further replies.
Bei ya Umeme yapanda na kuwa sh.357 kwa unit 1. Naipongeza serikali kwa hatua hii

Ni miaka mingi imepita bei ilikua haijapanda, huku gharama za uendeshaji zikiongezeka maradufu.

Pia hii sh.357 ni ndogo sana, serikali ilipaswa kuweka sh 700 kwa unit 1 ili kuweza kuleta tija kwenye shirika hili la Tanesco. Hivyo nitoe ombi kwa serikali kuongeza zaidi bei kufikia sh.700 kwa unit 1.

Nimpongeze waziri kwa ubunifu huu wa kuongeza bei ye umeme.
ikipendeza wafanye hata 6500 kwa unit 1, ili akili zitukae sawa
 
Weka screenshot ya umeme ulionunua alafu nikuambie unit moja ilikua sh ngapi. Ili tusibishane sana
Sikukimbia hesabu mkuu, 357×25.2=9000, ndio maana nimesema hayo mabadiliko yapo tangu miezi kadhaa, hayajaanza leo.
 
Kwa mwendo huu Makamba amejihakikishia kupata urais 2030.
Hawa mawaziri waliopita walikua wazembe Sana, Bei ilikua chini Sana hata mafisadi walishindwa kabisa kufanya ufisadi.
Kipindi chote Cha awamu ya tano hatukuona ufisadi mkubwa TANESCO.
Big up TANESCO.
Wapigaji kaeni mkao wa kugawa pesa kwenye sandarusi.
 
Bila kubishana sana, weka screenshot ya umeme ulionunua kabla alafu nikuambie ilikua sh ngapi.
Nimenunua juzi wala sijaona hilo ongezeko la Bei, labda Kama Bei imepanda Jana au Leo hapo nitaelewa,
Screenshot_20220609-134403.jpg
 
Bei ya Umeme yapanda na kuwa sh.357 kwa unit 1. Naipongeza serikali kwa hatua hii

Ni miaka mingi imepita bei ilikua haijapanda, huku gharama za uendeshaji zikiongezeka maradufu.

Pia hii sh.357 ni ndogo sana, serikali ilipaswa kuweka sh 700 kwa unit 1 ili kuweza kuleta tija kwenye shirika hili la Tanesco. Hivyo nitoe ombi kwa serikali kuongeza zaidi bei kufikia sh.700 kwa unit 1.

Nimpongeze waziri kwa ubunifu huu wa kuongeza bei ye umeme.
Ni lini Ewura imetowa hilo tangazo? Au unadhani umeme ni mafenesi unajipangia bei tu?
 
Mbona bei ni hiyo hiyo tangu mimi naanza kununia umeme

Unit 1= 357tsh/= au wamepandisha kutoka hiyo 357/=

Maana mwezi uliopita nilinunua umeme wa elf10 nikapewa unit 28

10000÷28=357.1

sasa imepanda lini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom