Bei za mabasi

Bei za mabasi

Wazee ninakapesa fulani Mungu amenipatia lakini nataka kuwekeza kwenye biashara ya basi za abiria. Hivyo wapendwa wangu naomba ushauri
1. Bei za marcopolo ni TSHS ngapi? na bei ya YOUTONG ni kiasi gani?
2. Je ni basi gani ni imara ili nisiingie hasara likafa haraka?
3. Kama ni body za kuchonga bei zake zinaendaje na kampuni gani nzuri?
kwa wenye uzoefu je biashara ya mabasi inalipa?
mtaji wangu ni Milion 370. je inaweza nipatia mabasi mawili? maono yangu ni nilitaka kujaribu njia ya DAR -Arusha
370 ni bei ya zhongtong moja...
aff8c0cd4b4f1fb8228828b6caa93a2a.jpg
 
Mkuu,achana na biashara ya mabasi,kama kweli una mkwanja huo biashara nzuru hapo nunua malori ya mchanga kama sita hv kwa bei ya around mil 300 kwa mil 50 kwa kila moja,hapo agizia befoward n.k,hapo utabakiwa na mil70 yako kibindoni mkuu,hiyo bei ya kuagizia ya mil 50 mkuu unalipia hadi bima kubwa kabisa,hayo malori utayatumia ktk biashara ya kubeba mchanga ambapo kwa dar kwa lori moja la ukubwa wa wa wastani hukosi laki 150 kwa siku,kwa malori 6 unaongelea laki 9 kwa siku,kwa mwezi kama mil27 hv mkuu,ukitoa matumizo ya service za hizo gari zote kwa mwezi bado utabakiwa na mkwanja mrefu sana,kila la heri mkuu ,biashara hii mkuu hutojutia uwekezaji wako,ni biashara nayoitamani sana kuifanya sema sina mtaji tu mkuu,biashara ya magari inahitaji usimamizi wako wa karibu sana ili muda wote yawe imara barabarani,kwa ushauri huu si vibaya ukinitumia hata kilo moja tu kwa majadiliano mapana zaidi mkuu
 
Hesabu ya bosi kwa bus la tata au eicher kwa siku ni 300,000
Kama kwa mwaka gari inafanya kazi siku 300 inakuwa 300,000*300=90,000,000.
Hizo siku 66 zilizobaki gari inakuwa mapumziko au service.

300000 kwa route ndefu au dala dala
 
Chukua robo ya pesa yako invest katika forex trading, robo Tatu nunua mabasi.
 
Marcopolo 700Mil

Youtong 250 - 300 mil

Marcedes 800 Mil

Nakushauri nunua youtong, hela yako itarudi mapema.

Kwa hiyo budget sidhan kama utaweza hii biashara kwasababu utatakiwa kulipa insuarance ambayo si ya kitoto, kuna vipesa vitakutoka hapo vingivingi.

Kwa hiyo pesa nakushauri ununue Min buses za TATA au EICHER kama ma4 hivi yanauzwa 70Mil. Upige rote za mbezi - kkoo au mbezi - mwenge. Kwa mwaka unarudisha hela yako na mtaji utakuwa mkubwa na utakuwa umepata experience ya jinsi ya kufanya biashara ya mabus.

Updates:

Kutokana na kuwepo kwa mabus ya mwendokasi, route za mwenge na kkoo ni kama hazipo.

Kwahiyo, nunua Eicher moja na nyingine unakopeshwa, zipeleke mikoani ambapo utapata routes mfano, moro-dom au dom-singida au moro-mvumero etc.

Ukiziweka dar kwa usawa huu itakula kwako. Biashara utaiona chungu.

Nimejifunza kitu hapa Thanks.
 
Mkuu, hapa inabidi uwe specific. Kwanza, Marcopolo si aina ya basi, bali ni kampuni ya kutengeneza bodi za mabasi yenye makao yake makuu nchini Brazil. Mabasi yanayotumika Tanzania yakiwa na bodi za Marcopolo ni Scania, Mercedes-Benz na Tata. Pili, Yutong ina aina (model) nyingi za mabasi ingawa aina inayotumika sana Tanzania ni ZK6116D (yenye injini mbele).
VERY NICE UNDERSTANDING
 
Marcopolo 700Mil

Youtong 250 - 300 mil

Marcedes 800 Mil

Nakushauri nunua youtong, hela yako itarudi mapema.

Kwa hiyo budget sidhan kama utaweza hii biashara kwasababu utatakiwa kulipa insuarance ambayo si ya kitoto, kuna vipesa vitakutoka hapo vingivingi.

Kwa hiyo pesa nakushauri ununue Min buses za TATA au EICHER kama ma4 hivi yanauzwa 70Mil. Upige rote za mbezi - kkoo au mbezi - mwenge. Kwa mwaka unarudisha hela yako na mtaji utakuwa mkubwa na utakuwa umepata experience ya jinsi ya kufanya biashara ya mabus.

Updates:

Kutokana na kuwepo kwa mabus ya mwendokasi, route za mwenge na kkoo ni kama hazipo.

Kwahiyo, nunua Eicher moja na nyingine unakopeshwa, zipeleke mikoani ambapo utapata routes mfano, moro-dom au dom-singida au moro-mvumero etc.

Ukiziweka dar kwa usawa huu itakula kwako. Biashara utaiona chungu.

mkuu hapo ukiwa umelipia gharama zote?, na mimi nataka nianze
 
mrejesho huwa ni jambo jema sana hasa kwa uzi ka hizi ambazo zimehusisha watu wa kila aina na walojitokeza kuchangia kadri walivyoweza kwa maslahi yake alouliza pia kwa maslahi yao binafsi, nategemea sasa mtoa uzi aje aeleze alichokifanya baada ya maoni na mitizamo ya wengi wadau
 
Hizo 370mil umezipataje? Sidhani mtu mwenye uwezo wa kupata mil 370 ashindwe kujua bei za yutong au Scania Marcopolo...Biashara ya magari kichaa
Acha mawazo ya kipumbavu wewe kwan kila mwenye hela nyingi lazima ajue bei za kila kitu. Fikra finyu!
 
Back
Top Bottom