Manyema
JF-Expert Member
- Sep 2, 2010
- 683
- 1,801
Huyu mama ni clueless kwa kweli, infact hakuna anachokijua mwanzoni nilikuwa na matumainai naye sana ila kadri siku zinavyokwenda nazidi kujiridhisha kwamba uwezo wake ni mdogo sana. Kibaya zaidi ni kama ameshikiwa akili na kina Mwigulu na genge lake na kwa kuwa wameshajua udhaifu wake wanamchezesha ngoma wanavyotaka mara matozo yasiyo na kichwa wala miguu kwenye miamala, makodi kwenye mafuta etc... Aliyesema rais angalau awe na degree moja aliona mbali sana at least anakuwa na uwezo wa kupambanua mambo kwa kina. Bado anafanya makosa ambayo ni very obvious kwenye teuzi zake yaani amepwaya sana, seems hasomi documents akajiridhisha kabla ya kusign. Ila wacha kazi iendelee tuone...