Bei za magari

Hii ya makampuni madogo madogo ambayo hayafahamiki huku kwetu risk ya kupigwa ni kubwa kumbuka unatuma pesa kwa kuliona gari kwenye picha hawana hata wakala hapa Bongo ndo maana tunang'ang'ania haya makubwa atlest usalama wa pesa yako ni mkubwa
 
Auction sheet ndio muhim.km zitakua za sahih kabla hazijaja kupigwa shoti huku
 
Gari langu la kwanza niliagiza mwenyewe.
Jambo la muhimu/lazima ni kuwa sambamba na mjuzi wa kuagiza pamoja na kutunza picha pamoja na taarifa muhimu.
Kwa kuagiza wewe unaweza kuomba kupunguziwa pesa.
Usiagize bila kuangalia picha nyingi kwa makini.
Pia jiridhishe na ushuru kwa kutumia kikokotoo cha TRA.
 
Uko sahihi kabisa.
 
Asante mkuu kwa maelezo yako mazuri
 
Asante nitazingatia hilo
 

Kwenye Grade R unaweza kupata bei chee zaidi kama ukijua repair ilikua ni nini, pia gari ikiwa repaired Japan inarudi kua nzuri kama imetoka kiwandani.
 

Mkuu naomba msaada wa kujua gharama za kutuma pesa japan wakati unafanya malipo ni USD ngapi?
 
Usiagize gari hasa kama n mara ya kwanza n bora uwape watu wenye uzoefu wakuagizie wewe ukafate,ila ukisema uagize wewe kama wewe nadhani sio Mbaya ukijifunza kitu kwa utakachokutana nacho.
Mwezi Machi mwaka huu nilikuwa ofisi za Beforward kule Chimara St. Walikuja watu kama 5 wakiulizia gari fulani ambayo walimpa mtu pesa awaagizie (kama huu ushauri unaompa mtoa mada).

Walifika pale wakiwa hawajui kinachoendelea kwa sababu huyo mtu hapatikani, ofisi imefungwa, na namba za simu hazipatikani. Wao waliona gari Beforward, wakachukua hadi reference number, ila pesa wakampa huyo mtu mwingine awaagizie.

Kwa ufupi kumbukumbu zilionesha ile gari ilishatolewa mwezi mmoja nyuma kwa jina la mtu mwingine. WAMEPIGWA.

Ushauri kwa mtoa mada, gari langu la kwanza niliagiza mwenyewe Beforward mwaka 2014. Nimelitumia hadi June mwaka huu baada ya kuagiza jingine kupitia Enhance Auto (hawa nilienda ofisini kwao na tukamalizana kila kitu. Muda wa kulipa ushuru walinitafuta, nikalipa kupitia simu, wiki 2 mbele nikapigiwa nikachukue ndinga).

Nenda kwenye ofisi za Autocom mtaa wa Samora. Mengine yatafuata baada ya kufika kwenye ofisi yao. Achana na habari za kumpa mtu akuagizie.
 
Asante sana kwa ushauri mkuu uliyonyooka lakini nilikuwa na swali kidogo je ukienda ofisini kwao wakuagizie wao hakuna charge zozote zinazoongezeka na pia je kuna chance ya kufanya bergaining
 
Asante sana kwa ushauri mkuu uliyonyooka lakini nilikuwa na swali kidogo je ukienda ofisini kwao wakuagizie wao hakuna charge zozote zinazoongezeka na pia je kuna chance ya kufanya bergaining
Ukienda ofisini kwao, hakuna gharama zitakazoongezeka. Na chance ya kupunguziwa ni kubwa. Kuna watu niliwaelekeza wakaenda Jumatatu wiki iliyopita, walikuwa wanataka kuagiza Toyota Rush. Walipunguziwa dola 700 kwenye bei inayoonekana mtandaoni. Binafsi nilipunguziwa kutoka $5127 hadi $4660. Kama ni mtu usiyetaka usumbufu, lipia gharama za gari, inspection, hadi clearance. Wkt wa kulipa ushuru watakutafuta ulipie, baada ya hapo watakutafuta ukachukue gari lako.
 
Hata gari za mkononi kibongo bongo gari bei chee ni mwanzo wa mwaka na mwisho wa mwaka. Maana purukushani za xmass, mwaka mpya na ada za shule huwafanya watu kuchizika na kuuza uza tu chuma kali bei chee! Gari zangu zote nimenunua nyakati hizo...
 
Jamani msiogope

Wajapan wako vizuri sana

Na ni vigumu sana kutapeliwa

Make sure una active whatsapp no+e-mail

That’ll means of communications kwa hawa jamaa
Na namba yao ya whatsapp iko verified kabisa na mjapan on every step lazima aku-consult kwa email na whatsapp.sijui lakini kwanini watu wanatapeliwa.

Ila kiukweli my experience was perfect [emoji1417]
 
Asante sana kwa ushauri mkuu uliyonyooka lakini nilikuwa na swali kidogo je ukienda ofisini kwao wakuagizie wao hakuna charge zozote zinazoongezeka na pia je kuna chance ya kufanya bergaining

Kwanini akuagizie?
Hela yako access ya mtandao unayo chagua lipia gari

Hakuna advantage yeyote ya kuagiziwa na agent tena charges lazima ziongezeke coz nayeye anapata cammisions kwa kila gari atakayoagiza

Hizo negotiations na kupunguziwa bei hata wew unaweza kuzifanya ukapunguziwa.



Kama hutaki kuagiza nenda yard

The only advantage kama labda watu wanaogiza magari mengi hasa wenye yard wao huwa wanapunguziwa ushuru so kama una mtu unamfahau,hapo sawa
 
Nilichomuelekeza ni kwenda kwenye ofisi ya kampuni husika kama Beforward, Enhance Auto, SBT Japan, Autocom, na si kwa third party (commission agents).

Kwa uzoefu wangu, gari la kwanza niliagiza mwenyewe online na bargaining nilifanya. Gari la pili nilienda kwenye ofisi ya kampuni husika (sio commission agent), bargaining tukafanya pale na hakukuwa na extra charge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…