Mwezi Machi mwaka huu nilikuwa ofisi za Beforward kule Chimara St. Walikuja watu kama 5 wakiulizia gari fulani ambayo walimpa mtu pesa awaagizie (kama huu ushauri unaompa mtoa mada).
Walifika pale wakiwa hawajui kinachoendelea kwa sababu huyo mtu hapatikani, ofisi imefungwa, na namba za simu hazipatikani. Wao waliona gari Beforward, wakachukua hadi reference number, ila pesa wakampa huyo mtu mwingine awaagizie.
Kwa ufupi kumbukumbu zilionesha ile gari ilishatolewa mwezi mmoja nyuma kwa jina la mtu mwingine. WAMEPIGWA.
Ushauri kwa mtoa mada, gari langu la kwanza niliagiza mwenyewe Beforward mwaka 2014. Nimelitumia hadi June mwaka huu baada ya kuagiza jingine kupitia Enhance Auto (hawa nilienda ofisini kwao na tukamalizana kila kitu. Muda wa kulipa ushuru walinitafuta, nikalipa kupitia simu, wiki 2 mbele nikapigiwa nikachukue ndinga).
Nenda kwenye ofisi za Autocom mtaa wa Samora. Mengine yatafuata baada ya kufika kwenye ofisi yao. Achana na habari za kumpa mtu akuagizie.