Bei za magari

Bei za magari

Wakuu poleni na majukumu, leo niliingia mtandaoni kidogo kucheki magari ambapo nimepitia kampuni mbalimbali za uuzaji magari lakini katika kampuni zote kuna kampuni moja "Autocom Japan" naona bei zao ziko cheap sana hadi nikashangaa labda magari yao yana shida maana variation na kampuni nyingine ni kubwa

Hali kadhalika nikaingia kwenye kikokotoo cha TRA nione hadi gari inafika bongo itacost kiasi gani then nikalinganisha na price kwenye show room zetu au kuagiza kupitia makampuni ya uagizaji kitu nilichokigundua ukiagiza mwenyewe price inashuka sana kuna gari unapata different ya milioni 5 nikasema hii hapana labda nakosea ngoja niwaulize wadau wa mandinga kuona kama ni kweli different iko hivyo.

Pia nimegundua kama gari ni ya miaka ya zamani let say 2010 kodi yake TRA ni kubwa kuliko gari ya 2011 au 2012.

Lakini kama ni kweli why watu hawaagizi wenyewe wana opt kununua show room au kuagiza kupitia kampuni wakati price variations ni kubwa coz kama unaweza ku save not less than 3M why usiagize? Na bado hapo hujafanya bergaining na kampuni husika

Soon nitaagiza gari yangu pendwa "Subaru Forester SH5" maana kwa bajeti niliyokuwa nayo niliona kama sitoboi lakini baada ya leo kujipa muda wa kupitia kampuni mbalimbali za magari na kikokotoo nimeona nipo ndani ya bajeti

Nawasilisha.
Kwa bei gani mpaka likufikie
 
Mkuu kwa ushauri mzuri agiza Gari mwenyew tu tena ni rahisi haina complications Sana Tumia hata siku 2 kusearch mtandaoni mfano mm niliagiza Toyota ist Japan nikawa napitia Karibu magari 40 then nkachagua Moja zuri ambalo limo ndani ya uwezo wangu nikamcontact seller moja kwa Moja akanitumia bei kwa profoma nikaomba na discount mwenyew nikapewa nikalipia kwa kutumia NMB bank (nilienda physically bank kabsa) then Gari ikatumwa gari ikikaribia TZ hua wanatuma documents za Gari kwa ajili ya Ku clear bandarini then utamkabidhi agent unayemuamini atakutolea Gari Yako so haina haja yakutumia third party kilak2 kiko wazi Kama Una swali ulizia Hapa Hapa Ili wengne nao wapate elimu wasiwe waoga, hizi showroom wamezidisha janja janja Sana na kutuuzia Gari zilizoshushwa km
Documents wanatuma kwa njia ipi mkuu. Unazipokelea posta?
 
Ukienda ofisini kwao, hakuna gharama zitakazoongezeka. Na chance ya kupunguziwa ni kubwa. Kuna watu niliwaelekeza wakaenda Jumatatu wiki iliyopita, walikuwa wanataka kuagiza Toyota Rush. Walipunguziwa dola 700 kwenye bei inayoonekana mtandaoni. Binafsi nilipunguziwa kutoka $5127 hadi $4660. Kama ni mtu usiyetaka usumbufu, lipia gharama za gari, inspection, hadi clearance. Wkt wa kulipa ushuru watakutafuta ulipie, baada ya hapo watakutafuta ukachukue gari lako.
Hiyo discount unapewa hata ukiagiza mwenyewe maana wote si mtapewa retail discount.
 
Hiyo discount unapewa hata ukiagiza mwenyewe maana wote si mtapewa retail discount.
Yes unapewa pia. Wakisema hii gari ni $3000 wewe utasema una $2400. Mta bargain hadi kufikia makubaliano.
 
Back
Top Bottom