Bei za maji katika Nyumba za kupanga ni mateso

Bei za maji katika Nyumba za kupanga ni mateso

Kuna mzee wangu mmoja aliwahi kuniambia
Epuka kuonekana mbele za watu kama una maisha mazuri ilhali unateseka moyoni mwako
Yanini ukakae sehemu nzuri wakati bili ya maji ya 15,000 inakufanya ujieleze sana

Nenda kaishi buza,vikindu,kisemvule huko pia ni watz wanaishi
ambapo maji ni Bure sio?
 
Mbona sisi Huku tuna lipa 2600 mzee
Bei ni Tofauti na Mikoa. Na kingine mnapaswa kuelewa tatizo sio bei tatizo ni Upigaji, Utapeli na Ulaghai kwenye bei iliyopo. wewe wa Tsh. 2,600 ukilipia 3,200 baada yake hautakuwa na maswali kwanini?
 
Mamlaka za maji mnaziingiza kwenye shughuli isiyo yao, ndio maana mita zao za maji hukaa nje wao shughuli yao ni extraction,treatment and distribution...humo ndani ya nyumba /uzio ni suala lenu watumiaji..mkiona mboyoyo ni mingi fungeni sub-meters, zitaonyesha nani anatumia kiasi gani ..ingawa Bahati mbaya mifumo ya maji (hata umeme) katika nyumba nyingi za kupanga haipo katika mpangilio mzuri wenye kuwezesha kila mmoja kujitegemea. Ila suluhisho hapo ni sub-meters
 
Daah serikali ina kazi sana, kuna jamaa mmoja nae alileta uzi kua wenyenyumba wasipandishe kodi, serikali iingilie kati.

Huyu nae maji anatumia yeye na familia yake, akija kudaiwa anataka serikali iingilie kati aloo.

Ishu ndogo kama hiyo wala sio ya kupelekana kwa mamlaka eti msuluhishe, ni ninyi wapangaji mjue mnaishi vipi hapo.

Kama mnatoa kweli basi mnaimudu ndo mana anawakamua na sio mda atapandisha iwe Tzs 20,000/= kabisa.
 
Mimi nilikuwa bachela nikaambiwa niwe nalipia 10,000 badala ya 15,000 wanayolipa wenzangu.
Nilikataa nilisema nitakuwa nalipia kadri ninavyotumia yaani 100 kwa ndoo kwa sababu nikioga asubuhi napotea nikirudi saa 9 natumia maji ya bar kisha narudi kulala tu home usiku saa 3.
Ungekuwa umepanga kwangu ningekutimua
 
Pole sana mkuu japo hilo haliwahusu idara ya maji. Mi niliwahi kupanga kwa mama mmoja muhaya wapangaji tulikuwa haturuhusiwi kuchota maji bombani. Maji yakitoka yanajaa kwenye tenki then tunachota kwenye tenki kwa 200 kila ndoo ilibidi nikae pale miezi 3 nikahama.
 
Tsh. 100 ndoo, kwenye unite Moja ya Tsh. 1,663 kuna ndoo 100, ambazo zitakugharimu Tsh. 10,000.. we unaona ni akili hilo?
Mkuu suluhu pekee ya huu mgogoro wa nafsi ni kujenga nyumba yako ili uachane na huu uonevu..
 
Mkuu suluhu pekee ya huu mgogoro wa nafsi ni kujenga nyumba yako ili uachane na huu uonevu..
Watanzania wote wenye kero hii wanaweza kujenga nyumba? au unawaza mtu mmoja tu?
 
Pole sana mkuu japo hilo haliwahusu idara ya maji. Mi niliwahi kupanga kwa mama mmoja muhaya wapangaji tulikuwa haturuhusiwi kuchota maji bombani. Maji yakitoka yanajaa kwenye tenki then tunachota kwenye tenki kwa 200 kila ndoo ilibidi nikae pale miezi 3 nikahama.
Wahaya Wabahaya Hawa jamna! 😂😂🤣🤣
 
Kwani per capita consumption ya maji mtu wa mjini (majiji) ni lita ngapi kwa siku?

According to NAWAPO 2002 ni 100 Liters per Person per Day, kwa Dar es Salaam.

Sasa, kama kila mpangaji mpo watatu (muke, mke na mtoto), ni 300L per day.

Kwa mwezi, ni Lita 9000 tu. Kwa lugha nyepesi, kila mtu atumie Lita 3000 tu kwa mwezi.

Zaidi ya hapo hama. Wajinga sana hawa wenye nyumba.
 
Back
Top Bottom