Bei za nauli za treni za kwenda Morogoro na Dodoma zinatakiwa ziwe juu zaidi ili kuweka uwiano wa biashara kati ya mabasi na treni

Bei za nauli za treni za kwenda Morogoro na Dodoma zinatakiwa ziwe juu zaidi ili kuweka uwiano wa biashara kati ya mabasi na treni

Katika kuhakikisha kwamba sekta ya usafirishaji wa abiria nchini inakuwa na uwiano mzuri wa kibiashara kati ya mabasi na treni, kuna haja ya kuangalia upya bei za nauli za treni kwa safari za kwenda Morogoro na Dodoma.

Ili kuboresha uwiano wa biashara na kutoa nafasi kwa mabasi kuendelea kushindana, napendekeza nauli za treni ziwe juu zaidi. Hatua hii itasaidia kuimarisha sekta ya mabasi na kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya usafiri vinaweza kuendelea kutoa huduma kwa tija, huku abiria wakipata uhuru wa kuchagua usafiri kulingana na vipaumbele vyao bila kuathiriwa sana na tofauti kubwa za bei.

Kwa kuongeza nauli za treni, sekta ya mabasi itapata nafuu ya ushindani na hivyo kusaidia kudumisha watoa huduma wengi kwenye soko. Hii siyo tu kwamba itachochea ukuaji wa sekta zote mbili bali pia itahakikisha huduma za usafiri zinapatikana kwa wingi na kwa ubora zaidi kwa wasafiri.
Huyu ndio familia ilitoa fedha kumsomesha, wewe mbona umeshindwa kuendesha ile gas yenu ya M-Gas??

Moja ya mtu mpumbavu wa fikra tokea dunia iumbwe
 
Huyu ndio familia ilitoa fedha kumsomesha, wewe mbona umeshindwa kuendesha ile gas yenu ya M-Gas??

Moja ya mtu mpumbavu wa fikra tokea dunia iumbwe
Kinacho wavutia watu kwenye treni ni speed ya treni ili wafike haraka. Kwa hiyo unataka watu wa mabasi waongeze speed kama ya treni. Watu wa mabasi hawawezi kuboresha speed ya mabasi kufikia ya treni.
 
Wabongo njia pekee sahihi kwao ya kukabiliana na ushindani wa kibiashara ni kumpiga vita mshindani huyo na ikiwezekana kumpoteza kabisa na Wala hawanaga muda wa kuangalia mapungufu yaliyopo kwenye biashara zao au vitu vya kuongezea Hili kumaintain customerbase.

Mimi naamini light kama muanzilishi wa kampuni ya NOKIA angekuwa ni mbongo basi leo tusingekuwa na makampuno mengine yanayotengeneza simu kama Samsung,Tecno,Iphone n.k.. maana mtanzania ni mtu mwenye roho mbaya sana linapokuja suala la biashara na ni mvivu wa kufikiria maarifa mapya
Kinacho wavutia watu kwenye treni ni speed ya treni ili wafike haraka. Kwa hiyo unataka watu wa mabasi waongeze speed kama ya treni. Watu wa mabasi hawawezi kuboresha speed ya mabasi kufikia ya treni.
 
Mwili unaupa mzigo kubeba kichwa kilicho jaa upumbavu
Kinacho wavutia watu kwenye treni ni speed ya treni ili wafike haraka. Kwa hiyo unataka watu wa mabasi waongeze speed kama ya treni. Watu wa mabasi hawawezi kuboresha speed ya mabasi kufikia ya treni.
 
Wapuuzi wachache kama wewe ndio mlifanya hadi sasa watanzania walio wengi waone kupanda ndege ni anasa na ndege ni usafiri wa kitajiri.
Nauli za ndege huwa ni kubwa duniani kote.
Kinacho wavutia watu kwenye treni ni speed ya treni ili wafike haraka. Kwa hiyo unataka watu wa mabasi waongeze speed kama ya treni. Watu wa mabasi hawawezi kuboresha speed ya mabasi kufikia ya treni.
 
Siungi MKONO hoja yako..mbona bado kuna route nyingi tu wanaweza kwenda kuhudumia?..nadhani USHAURI ungekuwa ni kwa namna gani treni iweze kuoperate 24 hrs

Mimi nashauri TRC wafanye michakato treni ya MCHoNGOKO iwe inatumia Masaa mawili na nusu tu, Dar - Dom
 
Katika kuhakikisha kwamba sekta ya usafirishaji wa abiria nchini inakuwa na uwiano mzuri wa kibiashara kati ya mabasi na treni, kuna haja ya kuangalia upya bei za nauli za treni kwa safari za kwenda Morogoro na Dodoma.

Ili kuboresha uwiano wa biashara na kutoa nafasi kwa mabasi kuendelea kushindana, napendekeza nauli za treni ziwe juu zaidi. Hatua hii itasaidia kuimarisha sekta ya mabasi na kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya usafiri vinaweza kuendelea kutoa huduma kwa tija, huku abiria wakipata uhuru wa kuchagua usafiri kulingana na vipaumbele vyao bila kuathiriwa sana na tofauti kubwa za bei.

Kwa kuongeza nauli za treni, sekta ya mabasi itapata nafuu ya ushindani na hivyo kusaidia kudumisha watoa huduma wengi kwenye soko. Hii siyo tu kwamba itachochea ukuaji wa sekta zote mbili bali pia itahakikisha huduma za usafiri zinapatikana kwa wingi na kwa ubora zaidi kwa wasafiri.

Uwiano mzuri ungekuwa kwenye kuondoa usumbufu hasa wa polisi barabarani.

Ieleweke wote wanaohojiwa kuhusu ufanisi wa polisi, hadharani nani atawananga?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Nauli za ndege huwa ni kubwa duniani kote.
Una uhakika?

Umetembea na kuishi nchi ngapi tuanzie hapo.

Maana naweza kuwa nadebate na mtu aliyesafiri kutoka Tanzania kwenda China ndio safari yake kubwa.
Kinacho wavutia watu kwenye treni ni speed ya treni ili wafike haraka.
Na kinachowavutia watu kwenye basi ni nini?
Kwa hiyo unataka watu wa mabasi waongeze speed kama ya treni. Watu wa mabasi hawawezi kuboresha speed ya mabasi kufikia ya treni.
Watu wa mabasi wanatakiwa waboreshewe miundombinu watembee kwa speed ya juu.

Kwa miundombinu mibovu ya barabara Tanzania haiingia akilini kilometa 192 watu wasafiri saa 4-5 barabarani huo ni uwendawazimu.
 
Sehemu ya kwanza ......01
HOJA YAKO
Hofu ya biashara ya mabasi ya usafirishaji abiria kushindwa kihilimili soko la ushindani ulioletwa kutoka kwa treni ya abiria ya mwendo kasi ya umeme sgr,
hivyo hofu yako kubwa abiria wa mabasi watapungua kupelekea mapato /faida ya biashara ya mabasi kupungua na kutishia ustawi uhai wa biashara ya mabasi.

SABABU PEKEE KUU uliyoifikiria itakayopekea kupungua abiria wa mabasi ni NAULI ya treni kuwa ya kizalendo ambayo ni himilivu kwa watanzania walio wengi .

NJIA SULUHISHO PEKEE ULILOFIKIRIA
Ili kunusuru biashara ya mabasi ya usafirishaji abiria hivyo umeshauri njia pekee ni KUPANDISHA NAULI za treni ,ili watanzania walio wengi masikini washindwe kuhimili kumudu gharama za treni halafu wakishindwa kulipia gharama ghali za juu sana za nauli za treni endapo zikipandishwa kama unavyoshauri sasa, basi wajaze katika mabasi wapande mabasi ya abiria waache kupanda treni kwa kushindwa kumudu gharama,
tena kama ingewezekana UNGEPENDA wasipande kabisa treni ili wajazane kwenye mabasi kwa kiasi kikubwa .HIVYO NDIVYO ULIVYOFIKIRIA.
part two ..02
SI KWELI KAMA BIASHARA YA MABASI ITAKUFA
1)sababu ratiba ya treni inakulazimisha wakati mwingine upange safari kwa kufuata ratiba maalumu.
Kwa wale ambao tunasafiri kwa kushtukiza bila kufuata ratiba ya kipangiwa muda maalumu wa safari kama kudamka alfajiri sana.
saa 10 usiku,bado tunaweza kuchagua usafiri mwingine mbadala wa treni.
2)TRENI haipiti maeneo yote ,mabasi bado yana nafasi yake katika maeneo hayo ambayo treni haipiti.Kwa sisi tubaosafiri maeneo ambayo treni haina kituo au haipiti kabisa bado tinaweza kutumia usafiri mbadala mwingine.
3)Kwa mabasi yanayosafiri eneo moja na treni kama wanahisi ushindani,WABWINU BWINU Ubunifu wa kibiashara waboreshe huduma zao ili kuvutia abiria si kufikiria kuathiri bei za washindani wao,pasipo kuingiilia uhuru wa biashara ya mwengine.
MFANO
Mnashindana mbio marathoni kama mshindani wako ana mbio kukushinda sio sahihi kumwambia refa au mashabiki wamwambie mshindani wako apunguze mbio ili wote mshinde.USHINDANI WA KIBIASHARA ni kitu ambacho sisi wateha tunakifurahia kwa sababu kinasaidia kuwaamsha waliolala waimize kichwa waje na ubunifu wankuboresha huduma zao kutuvutia sisi wateja,..IKIWEMO KUSHUSHA BEI pia ni mbinu ya kibiashara na sinkupandisha bei,bora ungeshauri wenye mabasi washushe bei ili kutivutia abiria.
AU BORA UNGEOMBA USHAURI WA MAWAZO YA NAMNA GANI YA KUVUTIA ABIRIA wapande mabasi ili hapa penye wengi upate mawazo mazuri ya wadau,bila kiathiri biashara ya mwenzio ,fikiria biashara yako wewe ufanye nini kuvutia wateja usifikirie ya mwenzio.Na kama ni lazima kufikiria ya mwenzio basi usimpangie namna mshindani wako namna ya kufanya biashara yake ili kukunufaisha wewe.WHY DO YOU THINK MSHINDANI WAKO ANA WAJIBU WA KUKUFIKIRIA WEWE why shoul he care about you badala ya watanzania walio wengi tena masikini,tena ni mtaji mzuri wa kisiasa mwenzio aache kuuza sera zake apate kura za wananchi wanyonge WALIO WENGI kwa ajili afikirie matajiri WACHACHE wa mabasi ,atakuwa ana akili???
 
Bei za nauli za treni za kwenda Morogoro na Dodoma zinatakiwa ziwe juu zaidi ili kuweka uwiano wa biashara kati ya mabasi na treni
Umekengeuka, siyo bure!
Kwamba unataka Watanzania wenye vipato vya chini mnaoita wanyonge wanyang'anywe haki ya kupanda treni ya SGR kuwahi shughuli zao kwa maslahi ya matajiri wa mabasi?!!
 
Meneja wa Makampuni? Makampuni gani hayo?
Bado una mengi ya kujifunza kuhusu mbinu za kisasa za kufanya biashara katika ulimwengu wa sasa wenye ushindani mkubwa wa kufanya biashara.

Back
Top Bottom