Bei za vifurushi kupanda huku waziri mwenye dhamana akikenua meno kwa furaha ni matusi mazito kwa waTanzania

Mbaya zaidi , vifurushi vyenyewe vya data Kama wanaiba vile , hakuna uhalisia kwenye zile mb's zinazotolewa bila Shaka huwa tunauziwa 700MB Kama 1GB
 
Ujue mkuu hili tatizo nimegundua ni la kijamii.

Namaanisha waTz wote kwa ujumla wetu tunakubaliana na kuridhika na huu upumbafu, vjnginevyo isingewezekana.

"The late" hao aliwafukuza kama mbwa kwa kuona mapungufu yao kuwa hawafai hata kwa kulumangila, lakini twashangaa Serikali hiyo hiyo kulamba matapishi yake kwa kasi ya upepo baada ya mwamba kudanja, ni nini kilikuwepo mbele ya pazia!

Hapa nadhani wa kulaumiwa si Nape peke yake, ni cyndcate nzima ya Serikali iliyopo madarakani.

Angalia mgao wa umeme na maji unavyotukaanga!

Bidhaa madukani kupanda kila siku bila ya tamko la Waziri husika ama Rais kukemea!

Maana yake ni kwamba haya yote yanayofanyika sasa hivi kudhalilisha watu kwa kupandisha bei za bidhaa za vitu na mgao wa maji na umeme ni baraka za Serikali iliyopo madarakani.

Kwa yanayoendelea nchini ilitosha kwa waTz kwa ujumla wetu kusema "hapana" kwa serikali iliyopo madarakani, "hapana" kwa Chama tawala na "hapana" kwa vyama vya upinzani, maana navyo kama sauti yetu vimelambishwa asali na kunyamazishwa, sasa ni vya nini na vina msaada gani kwetu?

Navyodhani, tuendelee kukandamizwa sana zaidi ya hapa ili uovu zaidi uliojificha katika nafsi za viongozi hawa mumiani uudhi zaidi na kukera mioyo ya wajinga wenye mahaba niue kwa serikali iliyopo madarakani ili mwisho wa siku wajitambue tuweze kuongea lugha moja na kauli moja kudadadeki.
 
TUNAANDAMANA........LINI MKUU
 
vocha wananunuliwa,umeme wanalipiwa,chakula,usafiri,wasaidizi wa kazi,kodi hawalipi ktk mshahara na marupurupu yao pia huo uchungu wautowe wapi?
 
TUNAANDAMANA........LINI MKUU
Kikawaida maandamano kama hayo huanzishwa na viongozi hasa wa upinzani ama wanaharakati na sisi raia wapenda haki kuwasapoti na kuwapa shime kwa kuunga maandamano!

Lakini sasa viongozi wote kwa ujumla wao tuliowategemea kuwa mstari wa mbele tayari walikwisha lambishwa asali na kuunga juhudi, nikimaanisha hakuna chama chochote cha upinzani Tz chenye mrengo wa kutetea maslahi ya Taifa ama raia wake kwa sasa, hakuna.

Wapenda maendeleo na wapenda haki, kipindi hiki ni kigumu sana kwetu kuwahi kushuhudiwa!
Hakuna kiongozi hata mmoja mwaminifu kuweza kumsadiki na kumwamini kumuuzia imani zetu, ni genge la wababaishaji watupu.

Uzuri ni kwamba Dunia hii ina mfumo rasmi usiobadilika kwa kila jambo hasa jambo ovu huwa halidumu milele, lipo leo na kesho litapita bila kujali litachukua muda gani.
 
Asa na wewe upinzani wapase sauti wakiwa wapi? Ukiachana na hao wala mshahara wa bure (special seatz) kuna wabunge wangapi wa upinzani Bungeni?
 
Asa na wewe upinzani wapase sauti wakiwa wapi? Ukiachana na hao wala mshahara wa bure (special seatz) kuna wabunge wangapi wa upinzani Bungeni?
Mkuu tusiongee mengi.
Sababu ulizoongea ndiyo zilitosha kuchafukwa pasikalike, sababu nchi hii si koloni ama watemi ambao viongozi wanapatikana kwa kurithi, ni ya kidemokrasia.

Serikali kama inaongoza hovyo kwa kukiuka ilani zake na katiba, hata kama ilichaguliwa kihalali, iondolewe tu, haina manufaa kwa watu.

Ukimya wa viongozi(Ccm na upinzani) tayari mie nimewaweka fungu moja.

Hata wewe unayewavumilia ipo siku utawachoka tu, labda wabadilike pakubwa na wajitambue na watambue tunachokitaka wananchi!

Embu kaa utulie uwapime bila mahaba kuanzia ccm na viongozi wa upinzani, kuna yeyote anayekemea uozo tunaofanyiwa raia kwa sasa?

Utetezi kwa viongozi wa upinzani kupigwa tanchi hauna uzito kwa sababu si mikutano pekee ama uwakilishi Bungeni tu, kuna njia nyingi za kuzungumza na umma na kiongozi akaeleweka anakusudia nini na raia tukamsapoti, hasa kwa dunia hii ya kidigital.
 
Naye kaanza kunyoa kipara ngoto!
Basi tumekwishaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…