Bei za vitu kushuka Kenya, sisi tunakwama wapi?

Mbona hujatuonyesha mchanganuo wa bei zilivyoshuka badala yake unaongea ujinga ujinga tuu.

Tanzania Huwa haiigi upuuzi, uzalishaji na soko ndio vitaamua bei.
 
Walaji hatuko tayari kuchukua hatua, kwa hiyo tuendelee kuumia wenyewe
 
Jibu hoja usi attack personality. Ubadhirifu ni jambo moja na inflation ni lingine. Tuna kazi kubwa sana kama taifa kuutokomeza ujinga
Sawa ni vitu viwili tafauti ila vinaweza husiana. Sera za fedha zinaendeshwa na serikali na benk kuu. Hizi sera hubadilika mara kwa mara kutokana na mabadiliko ya kiuchumi. Sera za fedha zinazopangwa na serikali huwa zinaegemea aidha katika kutanua au kupunguza matumizi ya serikali na kodi. Sasa kaka anapohusisha mfumuko wa bei na ubadhirifu, nahisi anaona matumizi ya serikali mengi yanaondoa pesa nyingi kwenye uchumi kuliko kuingiza na tatizo ndipo linapoanzia hapo. Mfano ruzuku ni moja kati ya matumizi ya serikali ili kusudu bei kutengemaa, ila unakuta matumizi hayaendi kwenye ruzuku badala yake unakuta mabillion ya pesa yamepotelea kusikojulikana na kuacha uchumi katika hali tata. Hizo pesa zinavuja kwenye uchumi bila mantiki zingetumika kwenye ruzuku kwenye suala la chakula bei zingeshuka.
 
Tatizo ni fita vya ukreini mkuu!!
 
Jibu hoja usi attack personality. Ubadhirifu ni jambo moja na inflation ni lingine. Tuna kazi kubwa sana kama taifa kuutokomeza ujinga
Wewe nawe ni griti thinka ,

Hivi hujui huo ufisadi unaofanywa ndio unaokoleza hali ngumu ,au haujui kwamba serikali inawajibu wa kupunguza tozo za bidhaa ili kuleta ahueni kwa mwananchi,

Chawa mnatia aibu sana
 
Sijui kwanini bado tuna tofautiana mpaka leo, mimi bado naamini, tatizo letu sio viongozi wa kuhamasisha, tatizo letu ni watanzania na uoga wao.

Nilishakuwekea mifano kadhaa, ule wa Lissu aliosema akiibiwa kura atawaambia wafuasi wake waandamane, mbona mwishowe hakuna kilichotokea licha ya Lissu kuibiwa...

Mfano wa pili ni huo ulioleta kwenye mada, kwamba kama bei za juu za vyakula zinatuumiza kwanini bado tumelala ndani mpaka tuamshwe na viongozi? ni uoga wetu tu.

Ukondoo wetu unasababisha viongozi hata kama wakiongea bado tunajifungia ndani, tena tukitishwa na kina Mambosasa ndio tunajifunika mashuka kabisa, tofauti na wakenya ambao wakitishwa wanasema wako tayari kuonja tear gas ya 2023!.

Naamini huo ujasiri hawajafundishwa na Raila, uko ndani ya nafsi zao.
 

Umesema:

"Mkuu haupo sahihi na MIXOLOGIST amekujibu vizuri tu."

Swali ni kuwa, wapi aliponijibu huyo nduguyo unapoparejea? Kwa maana hata wewe umeandika ukiwa unanijibu mimi, kwenye nilichokuwa nimeandika kukazia alichoandika mjumbe Shilingii siyo huyo mburula MIXOLOGIST.

Au ndiyo kuweweseka kwenyewe huku ndugu?

Kwani wale vijana wa hovyo ni mmoja? Kwa mwendo huu usiokuwa na dira Wala mwelekeo Kwa nini na wewe usiwe mmoja wao?

Wapi niliposema Kenya wame handle mfumuko vizuri? Au wapi ninaongelea handling ya mfumuko wa bei for that matter?

Maajabu ya Mussa!

Ruto, Rigathi, Mudavadi get Sh802m for new cars | Business Daily

Kumbe hata huelewi kuna mada gani mezani? Hivi hata umeelewa kuwa bei zinashuka huko kwa shinikizo la wananchi? Unaelewa tofauti ya huko na kwetu kuwa ni uwepo ujuaji uchwara uliopitiliza kama wenu na nduguyo hapo hata Kwa msiyoyajua?

Kwani kwetu hatujui bei za vyakula ziko juu? Hatujui madhara ya wizi au ubadhirifu kuhusiana na bei hizi? Ila kwetu unaona tuko vizuri? Kwenye lipi?



Si kuwa haya yanaendelea na kuathiri uchumi wetu huku yakiwa na baraka zote za wahuni, walamba asali na wale vijana wa hovyo kama ninyi?

Kwa hakika hamna mchango wowote kwa taifa hili.

Bure kabisa!
 
Hivi bei za bidhaa zinawekwa na nguvu ya soko (market forces) au matamko ya kisiasa?

Ni market forces,
Ila inaweza ikawa bei ziko accelerated na tabia na matendo ya politicians including rushwa, mis management kama unavyoona mtu analipwa malipo hewa au kiongozi naye ni mfanyabiashara say wa petrol its likely ata influence bei kwa personal gain tofauti na ambavyo market forces zingepelekea trend ya bei iwe.
 
Wewe nawe ni griti thinka ,

Hivi hujui huo ufisadi unaofanywa ndio unaokoleza hali ngumu ,au haujui kwamba serikali inawajibu wa kupunguza tozo za bidhaa ili kuleta ahueni kwa mwananchi,

Chawa mnatia aibu sana
Shida kubwa ninayoiona kwenu mnadhani ripoti ya CAG ni hukumu ya mahakama. CAG ana ainisha maeneo yenye udhaifu katika matumizi ya pesa za umma na hiyo report yake siyo conclusive proof that pesa za umma zimeibiwa, sometimes, maelezo yakitolewa hizo hoja zina kufa. Tuanzee kutoa huu ujinga kwanza.

Pili, bei ya bidhaa haipungui simply kwa matamko ya kisiasa au kwa kuondoa tozo, inategemea ni bidhaa gani na gharama yake ya kutengenezwa au kuchuuzwa. Ziko factors nyingi zina changia. Tuliza akili, kama unayo, usidangaywe na wanasiasa wenye fishy and unclear agenda.
 
Kuna gap kubwa sana la knowledge kati yangu na yako. Huu mchezo hautaki hasira, nadhani unywe dawa za kupunguza stress and anxiety.
 
Naomba nikuulize swali moja tu, huiamini nguvu ya umma kwenye kuleta mabadiliko?

Unaweza pia kunionesha uhusiano uliopo, kati ya kuwa na pesa ya kulipa mishahara na serikali kupunguza bei ya vyakula?
 
Watanzania %kubwa ni wezi so vikipanda tunaongeza kiasi cha kuiba ila wasio kwenye connections za wizi sasa ndio taaabu kwao
 
Naomba nikuulize swali moja tu, huiamini nguvu ya umma kwenye kuleta mabadiliko?
Mambo ya kitaalamu hayaitaji msuli, umma usiotumia akili, unaweza kutumiwa na wanasiasa for their own political mileage or gain
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…