BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Date::8/14/2008
Muogeleaji wa Tanzania atupwa nje ya michuano ya Beijing Olimpiki
Khalid Yahya Rushaka,mmoja kati ya wanamichezo wa Tanzania waliowakilisha taifa Olimpiki Beijing ambaye ametupwa nje ya mashindano Jumatano.
Na Mwandishi Wetu
Mwananchi
MUOGELEAJI wa Tanzania, Khalid Yahya Rushaka jana alishika nafasi ya tatu kwenye michuano ya awali ya kuogelea lakini akashindwa kusonga mbele baada ya kumaliza mchezo wa mita 50 akiwa nje ya muda unaotakiwa.
Rushaka, ambaye alishiriki mchezo wa kuogelea wa mita 50 (freestyle) alitumia muda wa sekunde 28.50 ambao ni tofauti ya sekunde 7.04 wa muda wa kufuzu kwenda raundi ya pili na hivyo kutupwa nje ya mashindano hayo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Olimpiki, Rushaka alishiriki mchuano wa mchujo akiwa Kundi la tatu na akashika nafasi ya tatu akiwa nyuma ya muogeleaji wa Malawi, Charlton Nyirenda, aliyetumia sekunde 27.46 na Jackson Niyomugabo wa Rwanda aliyetumia sekunde 27.74.
Kundi hilo halikuweza kutoa muogeleaji wa kwenda raundi ya pili baada ya wote kuwa chini ya muda wa kufuzu.
Muogeleaji wa mwisho kuchukuliwa kwenye kundi hilo alitumia muda wa sekunde 22.17 wakati wa kwanza alitumia muda wa sekunde 21.46 katika makundi yote ya mchezo wa mita 50 (freestyle).
Kuondolewa kwa Rushaka, 28, kunafanya matumaini ya Tanzania kwenye michezo ya bwawani yabakie kwa chipukizi, Magdalene Ruth Alex Moshi, ambaye atashiriki mchuano huo wa mita 50 (freestyle) akiwa katika Kundi la 3.
Magdalene, ambaye kama Rushaka anashiriki kwa mara ya kwanza Michezo ya Olimpiki, ana umri wa miaka 17 na kuvuka raundi ya kwanza itakuwa ni mafanikio makubwa kwa chipukizi huyo.