*Beijing Olympics 2008*

Date::8/14/2008
Muogeleaji wa Tanzania atupwa nje ya michuano ya Beijing Olimpiki

Khalid Yahya Rushaka,mmoja kati ya wanamichezo wa Tanzania waliowakilisha taifa Olimpiki Beijing ambaye ametupwa nje ya mashindano Jumatano.
Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

MUOGELEAJI wa Tanzania, Khalid Yahya Rushaka jana alishika nafasi ya tatu kwenye michuano ya awali ya kuogelea lakini akashindwa kusonga mbele baada ya kumaliza mchezo wa mita 50 akiwa nje ya muda unaotakiwa.

Rushaka, ambaye alishiriki mchezo wa kuogelea wa mita 50 (freestyle) alitumia muda wa sekunde 28.50 ambao ni tofauti ya sekunde 7.04 wa muda wa kufuzu kwenda raundi ya pili na hivyo kutupwa nje ya mashindano hayo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Olimpiki, Rushaka alishiriki mchuano wa mchujo akiwa Kundi la tatu na akashika nafasi ya tatu akiwa nyuma ya muogeleaji wa Malawi, Charlton Nyirenda, aliyetumia sekunde 27.46 na Jackson Niyomugabo wa Rwanda aliyetumia sekunde 27.74.

Kundi hilo halikuweza kutoa muogeleaji wa kwenda raundi ya pili baada ya wote kuwa chini ya muda wa kufuzu.

Muogeleaji wa mwisho kuchukuliwa kwenye kundi hilo alitumia muda wa sekunde 22.17 wakati wa kwanza alitumia muda wa sekunde 21.46 katika makundi yote ya mchezo wa mita 50 (freestyle).

Kuondolewa kwa Rushaka, 28, kunafanya matumaini ya Tanzania kwenye michezo ya bwawani yabakie kwa chipukizi, Magdalene Ruth Alex Moshi, ambaye atashiriki mchuano huo wa mita 50 (freestyle) akiwa katika Kundi la 3.

Magdalene, ambaye kama Rushaka anashiriki kwa mara ya kwanza Michezo ya Olimpiki, ana umri wa miaka 17 na kuvuka raundi ya kwanza itakuwa ni mafanikio makubwa kwa chipukizi huyo.
 
Kila la Heri M.R.A Moshi.. umri bado unakuruhusu kushiriki olimpiki nne zaidi.

Sasa bado saa kadhaa tuanze kuwaona wafukuza upepo ambapo utamu wa michezo hii ufikia kwenye kilele....
 
Bibie akifanya vizuri kweli itakuwa miujiza. Hata hivyo her clocking time is 9 seconds over the world record. Tuombe kalumanzira amtembelee leo usiku ili afanye miujiza.
We need to support our athletes, mwe!!
 
Nimetoka kusoma article moja iliyoandikwa na Charles Onyango-Obbo (Daily Nation Kenya) kuhusu michezo ya jadi ya kiafrika ambayo ingefaa tuwe mstari wa mbele na hatufanyi hivyo na pia olympic zetu za maisha zilipo.

Michezo/shughuli ya/za jadi ambayo tunapswa tuonyeshe uwezo na hatuna uwezo huo ni;
1. Kurusha 'javelin' - inafanana na mkuki.
2. kukimbia - kila leo tunakimbia migomo na kufukuzwa na FFU. Uwezo wetu wa mbio una uhusiano na siasa zetu
3. weight lifting- kumbuka watu wanavyobeba mizigo mizito sana na kwa umbali mrefu, ila ikija mashindano hayo hatuwezi kushinda

4.Uwindaji wanyama kwa mshale- Tunashindwa hata kushinda medali ya 'archery'??🙂

its an interesting article mnaweza kuipata hapahttp://www.nation.co.ke/oped/Opinion/-/440808/455608/-/item/0/-/pvkq70/-/index.html
 
Track and field imeshaanza, siku zote huwa nashangaa kwa nini watz(wamasai) awaendi kurusha mikuki...😀
 
Track and field imeshaanza, siku zote huwa nashangaa kwa nini watz(wamasai) awaendi kurusha mikuki...😀

Yaani rafiki umesema kweli, tuna watu wa kabila nyingi kutokana na kazi zao za jadi tungekuwa mbali sana tukiwaelewesha kuwa kuna michezo na mashindano ya shughuli kama hizo.
Wamasai- Kurusha mikuki
wajaluo, wakwaya, wakerewe, wahaya- canoeing hata uogeleaji maana hatari ni chache mno katik ziwa kuliko pwani
Wakikuyu- weightlifting- you should see the loads wanazobeba wanawake huko Kiambu
 
Bimkubwa...
Kwenye list yako umewasahau Wamakonde na mishale(archery) yao, kwa kumbukumbu zangu hawa ndio walinzi pekee Bongo ambao hutumia zana hizo, tena nasikia wana shabaha ya hali ya juu...!
 
Heat za mita mia moja, karibu zitaanza... ninawekeza kwa Bolt
 
Hapa nilipo Tampere- natizama national TV.. wapo live
 
Hiyo national TV ni sawasawa na PBS? I am using cable naona NBC wanaonyesha Beach volleyball. I really like track and field. Nilikuwa mkimbiza upepo mzuri sana wa mita 100 na 200. Basi tu ndugu wanajua jinsi ya kumlet down mtu....... wewe mtoto wa kike hutakiwi kukimbiakimbia.
 
Jamani, ni heats hizo? what about Asafa? hivi Gatlin yupo this time? Greene naye vipi?
 
Asafa kamaliza heat yake kwa kutumia 10.15s, kidogo kundi lake lilikuwa na upinzani
 
Thats good time. Vipi Tyson Gay? natoka kidogo maana naona siwezi kuziona hizo mbio ngoja nikae niangalie Randy Jackson's best dance crew.
Asante. i appreciate it.
 
Heat ya tatu sasa, macho yangu kwa Thompson Richard wa Tri &Tobago
 
Thats good time. Vipi Tyson Gay? natoka kidogo maana naona siwezi kuziona hizo mbio ngoja nikae niangalie Randy Jackson's best dance crew.
Asante. i appreciate it.
Nimemwona anapashwa misuli moto, atakimbia heat inayofuata.. siku njema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…