Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,193
1.SIKU 50 ZA MWANZO NI MATANGAZO, UHAMASISHAJI NA MAFUNZO YA NGUVU KUANZIA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI, VYUO, MAWIZARANI, KATIKA BUNGE, MAHAKAMA ZOTE, TAASISI, MITAANI NA VIJIJINI KOTE NCHI NZIMA JUU YA UWAJIBIKAJI, UZALENDO, HAKI NA UMUHIMU WA KUPIGA KURA NA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOFAA NA KUPINGA KWA NAMNA ZOTE UTOAJI NA UPOKEAJI WA RUSHWA.
2. KISHA NI MIMI KUJIUZURU NA KUITISHA UCHAGUZI MPYA SIKU YA 100.
Dhanio :
Itakuwa imekubalika kikatiba chini ya Tume huru ya Uchaguzi kuwa tukirudia uchaguzi tuwe tumepunguza sana idadi ya majimbo. Yaani kila Mkoa uwakilishwe na Wabunge wawili tu (Ke & Me) na ni watu wakufanya kweli Bungeni!
Na kutakuwa na punguzo kubwa pia la Wizara kwa kuunganisha Wizara zinazoweza kuwekwa pamoja.na kuimarisha 'appraisal, checks & balance mechanisms' za kuhakikisha uwajibikaji kwa kila Kiongozi na kila Mwananchi.
Baada ya siku 100 Serikali (maana naweza nisichaguliwe mimi) itaenda hatua kwa hatua katika kutekeleza agenda za maendeleo katika kuleta mapinduzi ya sayansi na teknolojia, kiuchumi, kielimu, katika miundo mbinu na kijamii kwa ujumla.
Ningekuwa mimi Rais ningefanya hivi.
1. Msamaha wa mafisadi na wafungwa wote.
2. tunaanza upya kwa kutangaza hali ya hatari.
3. Anayeshikwa kwa rushwa kwa video ama kwa udhibiti ulio wazi hakuna mahakama ni Risasi tu.
4.Mkataba wa migodi siuzi ama kuwadai kodi wawekazi bali nafanya hivi, mfano anayetaka mgodi wa geita jenga tujengee bandari ya kisasa mtwara,tanga na dar. anayetaka buzwag nijengee treni na reli za kasi kama za ujerumani niunganishie mikoa ya tanga,arusha,mwanza,shinyanga hadi mipakani burundi,kongo,rwanda na uganda. anayetaka Nzega mining nijengee Reli za kasi kuunganisha dar mtwara msumbinji,malawi,zambia. Na anayetaka Mwadui nitengenezee vyazo vya umeme vya uhakika .Anayetaka nyamongo nisambazie umeme nchi nzima na anayetaka mafuta ya zanzibar hakikisha unaweka infrastructure za Internet nchi nzima.
5. Naanzisha mashamba makubwa
6.Mvulana anayetia mimba msichana awe anatoa pesa ya matumizi elfu hamsini kila mwezi, kama hana serikali yangu itamlipa msichana huyo fedha hizo kila mwezi na mvulana huyo kupelekwa ktk mashamba hayo kupiga mzigo.
7.Bandari hizo zilizojengwa nitatoza ushuru wa chini kulinganisha nchi zote zinazotuzunguka.
8. Nitajitahidi kudhibiti wizi wa posta ili e-bussiness ipate kufanyika maana tutakuwa na mtandao hadi kijijini.
9.Atakaye taka mgodi wa uranium itabidi atujengee university kila mkoa ,university yenye kiwango cha kimataifa.
10.atakeyetaka mgodi wa gas itambidi awalipe ma polisi na ma lecturers mshahara
11. free working permit kwa ma-lecturer kutoka nchi yoyote duniani.
Hadi hapo nitakuwa nime create ajira milioni 20, kwa hiyo kodi tutapata kutoka kwa waajiriwa na kutumia miundo mbinu yetu.
- Duh! mkuu Mkamap, chonde chonde ndugu yangu kwa mishahara ilivyo hapa kwetu kwenye rushwa si utaua taifa zima, be realistic japo kidogo ndugu yangu, au unasemaje?
Respect.
FMEs!
Ndugu yangu
Nafikiri hiyo ndo reality,watu wanachukuwa rushwa si kwa sababu ya mshahara mdogo bali nikukosa uzalendo.
Sema nitarekebisha kitu kimoja, Tutaunda mbeki za mkopo wenye asilimia ndogo sana ,ili anayeona mshahara mdogo akakope huko. Ktk bank hizo itambidi tu kuonyesha ID yake ya anakofanya kazi na form iliyotiwa mhuri na mwajiri wake anachukua mkopo siku hiyohiyo.
Mkuu mshahara karibu duniani kote haitoshi. Ukiangalia hakuna watu wenye madeni kama wazungu,unamuona anakula good time pale mlimani kilimanjaro kumbe ana madeni zaidi ya bank 5. Nafikiri mshahara ungekuwa unatosha wasingekuwa na madeni namna hii.
- Sawa sawa mkuu, lakini nchi kama US mtu anashindwa kuchukua rushwa kwa sababu anafikiria sana kupoteza pension yake ambayo ni bomba sana, kwa hiyo anaamua kukataa rushwa, sasa bongo ukikataa rushwa itakuwaje mkuu ningeelewa kama ingekuwepo alternative, au?
Respect.
FMEs!