1.SIKU 50 ZA MWANZO NI MATANGAZO, UHAMASISHAJI NA MAFUNZO YA NGUVU KUANZIA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI, VYUO, MAWIZARANI, KATIKA BUNGE, MAHAKAMA ZOTE, TAASISI, MITAANI NA VIJIJINI KOTE NCHI NZIMA JUU YA UWAJIBIKAJI, UZALENDO, HAKI NA UMUHIMU WA KUPIGA KURA NA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOFAA NA KUPINGA KWA NAMNA ZOTE UTOAJI NA UPOKEAJI WA RUSHWA.
2. KISHA NI MIMI KUJIUZURU NA KUITISHA UCHAGUZI MPYA SIKU YA 100.
Dhanio :
Itakuwa imekubalika kikatiba chini ya Tume huru ya Uchaguzi kuwa tukirudia uchaguzi tuwe tumepunguza sana idadi ya majimbo. Yaani kila Mkoa uwakilishwe na Wabunge wawili tu (Ke & Me) na ni watu wakufanya kweli Bungeni!
Na kutakuwa na punguzo kubwa pia la Wizara kwa kuunganisha Wizara zinazoweza kuwekwa pamoja.na kuimarisha 'appraisal, checks & balance mechanisms' za kuhakikisha uwajibikaji kwa kila Kiongozi na kila Mwananchi.
Baada ya siku 100 Serikali (maana naweza nisichaguliwe mimi) itaenda hatua kwa hatua katika kutekeleza agenda za maendeleo katika kuleta mapinduzi ya sayansi na teknolojia, kiuchumi, kielimu, katika miundo mbinu na kijamii kwa ujumla.