Beki bora zaidi kuwahi kumshuhudia!

Beki bora zaidi kuwahi kumshuhudia!

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
Kwa miaka mingi Dunia ya soka imekuwa ikiwatukuza wachezaji wanaocheza nafasi za mbele au kwa kifupi Washambuliaji huku ikiwasahau kama si kuwatupa kabisa wachezaji wanaocheza nafasi ya Ulinzi ( Mabeki ). Na ndio maana haishangazi takribani miaka 40 iliyopita ni Fabio Cannavaro ndio beki pekee kuwahi kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa Dunia.

Katika idara ya ulinzi, kuna mabeki mahiri wamewahi kucheza katika nafasi hiyo. Kuanzia nafasi za mabeki wa pembeni mpaka wale wa kati ambao licha ya jukumu lao la kukaba pia husifika katika kupandisha mashambulizi kwa timu zao.

Naamini kuna mabeki wanastahili zaidi sifa kwa uhodari wao kuliko hata washambuliaji tanaowatukuza kila siku, karibuni mtiririke wadau
 
Puyol Mascherano Pique Umtiti Abidal na wengineo ila waliopitia Barcelona
 
Sasa hv anayechipukia ni John Stones beki katulia sana yule. Akiendelea vile atakuja kuwa beki bora sana
 
Mu uruguay mmoja mkatili sana Paolo Montero huyu alikuwa anatumia mguu wa kushoto,ana uwezo wa kukokota mpira na kutoa pass murua kwa ufasaha ,halafu alikuwa kisiki linakaba balaaa


Sema tatizo lake alikuwa mhuni sana ,rafu za kijinga anacheza na kadi nyekundu nyingi alikuwa anapata ,

Juventus hiyo Montero akisaidiana na Brindelli au Tudor mpk 2005


Paolo Montero
Roberto Ayala
Diego Godin

[emoji115] [emoji115] [emoji122] [emoji122]
 
Maldini
Cafu (a man with 2 hearts)
Aldair
Kasongo Athumani
Steven Keshi
Ken Mkapa
Said Kolongo
Method Mogella
Msudani ninja
Jembe Ulaya
Sammy Onyango
Marcio Santos
Lothar Matteus
Oscar Ruggeri
Mark Fish
Tony Adams
Alesandro Costacurta
Ciro Ferara
Zanetti
Thuram
Marcelo
Roberto Carlos
Baresi
Sammy Hyppia
 
Franz Beckenbauer
Paolo Maldini
Bobby Moore
Franco Baresi
Franco Alberto Torres
Daniel Passarella
Taribo West - Eagles Nigeria
Gerome Boateng
Jella Mtagwa
John Terry
Sergio Ramos
Thiago Silva
Alessandro Nesta
Fabio Cannavaro
Cafu
Roberto Carlos
Lothar Matthaus
Lilian Thuram
Laurent Blanc
 
Gianluca zambrotta alikuwa anapiga beko zote za pembeni..

Cafu sijapata ona beki 2 mstaarabu, kupandisha mashambulizi na nidhamu kama yeye. Dani Alves nidhamu mbovu inamuharibia. Humu pia huwasahau bixente lizarazu, lilian thuram na michel salgado babu gary neville nae kwa krosi si haba.

Beki tatu, roberto carlos was a legend
 
Back
Top Bottom