Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,258
Beki mpya wa Simba Hamad Juma amelazwa wodi namba 5 katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kuanguka bafuni leo asubuhi akiwa nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam. Beki Hamad aliyecheza mechi ya jana dhidi ya Ndanda Fc akiwa anaoga aliangukia kisogo chake na kusababisha kumwaga Damu nyingi na kukimbizwa hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu na kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kuongezwa Damu.
Updates
Beki mpya wa kulia wa Simba, Hamad Juma, jana asubuhi alianguka bafuni akiwa nyumbani kwake na kusababisha achanike kisogoni kwake.
Mara baada ya kutoka kwa taarifa hiyo ambayo siyo nzuri kwa Wanasimba, hofu ilitawala miongoni mwao lakini habari ni kuwa mchezaji huyo anaendelea vizuri na ameshapatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka hospitali.