Beki Mpya Simba Aanguka Bafuni

Beki Mpya Simba Aanguka Bafuni

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
14088483_1155702411152835_7452943182995156997_n.jpg

Beki mpya wa Simba Hamad Juma amelazwa wodi namba 5 katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kuanguka bafuni leo asubuhi akiwa nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam. Beki Hamad aliyecheza mechi ya jana dhidi ya Ndanda Fc akiwa anaoga aliangukia kisogo chake na kusababisha kumwaga Damu nyingi na kukimbizwa hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu na kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kuongezwa Damu.

Updates
Beki mpya wa kulia wa Simba, Hamad Juma, jana asubuhi alianguka bafuni akiwa nyumbani kwake na kusababisha achanike kisogoni kwake.

Mara baada ya kutoka kwa taarifa hiyo ambayo siyo nzuri kwa Wanasimba, hofu ilitawala miongoni mwao lakini habari ni kuwa mchezaji huyo anaendelea vizuri na ameshapatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Hamad%2Bsafi1.jpg
 
coastal.jpg

Hamad alipoifunga simba, NAMBA 3 NI DANNY LYANGA
 
Mo bilioni 20 bado tunapeleka wachezaji mwananyamala?
seriously?

kwani hiyo 20b imeshaingia tayari?

Halafu kumbuka kama amepata jeraha kichwani na kuvuja damu nyingi, ilikuwa lazima afikishwe hospitali yoyote ya karibu ili apate msaada wa haraka
 
hoja yako imekaa kishabiki sana

Mimi ni Simba damu.....
wewe kama unaona kupeleka wachezaji mwananyamala hospital ni sawa..haya
mimi naona kwa ukubwa wa timu ya Simba hata kama Mo hajapewa timu
wachezaji wanapaswa kuwa na insuarance ya matibabu ya hospitali yoyote ile Tz...
wachague wenyewe....sio kwenda kugombea vitanda huko mwananyamala hospital
 
ni sawa nikadhani huna hii tafakuri ya pili kwamba mchakato wa MO bado sana kuuwazia kwa sasa....sanjari na kukuunga mkono kwa Hospitali ya Mwananyamala kutokua na hadhi ya SIMBA lakini pia tutafakari kidogo tukio lenyewe na siku ya tukio ingawa pia sina hakika mchezaji huyu anaishi wapi ima ni jirani na hospitali hiyo na huenda hata majirani zake kwani ni mchezaji aliyetokea Tanga..........kiumla hapo nimeoiona solution ya haraka ilikua hapo Mnyamala na ninavyoijua siku hizi pa huduma zimeboreka sana .....kuna mchezji wa Yanga Ladislaus Mbogo sasa hivi yupo Toto alifanyiwa upasuaji wa taya hapo wakiwa na mfadhili Manji.........

Hiyo ni lay thoughts lakini professionally hilo liwe funzo kwa timu yetu pia kwa matukio ya dharura kama hayo na HADHI ya timu nikiunga mkono hoja yako..........
 
Mimi ni Simba damu.....
wewe kama unaona kupeleka wachezaji mwananyamala hospital ni sawa..haya
mimi naona kwa ukubwa wa timu ya Simba hata kama Mo hajapewa timu
wachezaji wanapaswa kuwa na insuarance ya matibabu ya hospitali yoyote ile Tz...
wachague wenyewe....sio kwenda kugombea vitanda huko mwananyamala hospital
kwani mwanaNyamala hawa Bima ya Afya , umekariri mzee
 
Mo bilioni 20 bado tunapeleka wachezaji mwananyamala?
seriously?
Mkuu, wanasema billion 20 wananunua treasury bonds. Zikianza kuzaa after one year ndiyo hela inaweza kutumika kwenye club. Si ajabu (ni maoni yangu) wakati wakisubiri ataikopesha hela club ili bond zikiiva alipwe!

Hamna tofuati na mwenzake anayekodi. Wote wajanja wajanja tu.
 
Hakunaga mhindi 'honest businessman'
 
Back
Top Bottom